Magazeti yote ya leo hakuna lililoandika habari za Waraka wa TEC

Magazeti yote ya leo hakuna lililoandika habari za Waraka wa TEC

Mkuu wewe mwenyewe upo mtandaoni na habari zote unazi pata kutoka mtandaoni bado tu unaamini magazeti yananafasi katika ulimwengu wa sasa😵

Nyakati hizi tulizopo ninyakati ambazo watu wanapata habari kwa haraka zaidi kwa kupitia mitandao kuliko wakati wowote kawahi kutokea, hivyo magazeti kutokuandika habari ya waraka wa baraza la maaskofu hiyo haipunguzi chochote
Nyie pelekeni kijiwaraka chenu social media zote pia piteni kila nyumba mnasoma huo waraka Ila nothing will change DP world must come soon.
 
Hawajawahi kukaa kimya labda kama umezaliwa jana, Askofu aliyenyanganywa pasport hivi alikuwa nani? aliyekemea utumbuaji usio na staha unakumbuka alikuwa nani? Vuta kumbukumbu Mkuu utanipa jibu, Askofu Bagonza umemsahau mara hii? Unakumbuka walimuita magufuri kupa honyo kuhusu mauaji horela akagoma kwenda huko tec.
Mimi ni msahaulifu hebu naomba tamko la TEC kwenye wizi wa Uchaguzi wa 2020
 
Jana kulikuwa na tetesi kuwa vyombo vyote vya habari vimepewa amri ya kutoandika habari za waraka wa TEC.
Haiwezi kuwa coincidence, yoooote yasiandike. Ni kweli Nape aliyapa maagizo ya kutoandika.
Inamana mpaka magazeti ya Vatican na Pengo hayajaandika?
 
Yamenunuliwa Unajua Kanisa Lina Akili
Lenyewe Linaupeleka Waraka Mpaka Kijijini Ambako Mwananchi Hawezi Kupata Gazeti
Hizo gharama za kusambaza waraka ni Bora wangenunua mvinyo wachanganye kwenye divai ili walewe vizuri, Tec ni taasisi ya ajabu kabisa yaani imejiingiza mkenge na kuanza kupinga maendeleo waziwazi.
 
Jana kulikuwa na tetesi kuwa vyombo vyote vya habari vimepewa amri ya kutoandika habari za waraka wa TEC.
Haiwezi kuwa coincidence, yoooote yasiandike. Ni kweli Nape aliyapa maagizo ya kutoandika.
Tanzania hamna vyombo huru vya habari na waadnidhi wote wamegeuka kuwa madalali.

Waandishi wapo lakini waliamua miaka mingi ilopita kuachana na kanuni kuu au misingi ya uandishi wa habari.

Kinoendelea sasa hivi ni "Chequebook Journalism" na bahasha za khaki.
 
Jana kulikuwa na tetesi kuwa vyombo vyote vya habari vimepewa amri ya kutoandika habari za waraka wa TEC.
Haiwezi kuwa coincidence, yoooote yasiandike. Ni kweli Nape aliyapa maagizo ya kutoandika.
Hata mimi kwenye kagazeti changu cha matching guy sikuandika lolote juu ya waraka wa tec. Kwa ukapa huu nani anataka kufungiwa biashara yake?
 
Msigwa alishawapa mgao, sio ishu...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ā€˜Makubaliano’ na ā€˜Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ā€˜Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Jana kulikuwa na tetesi kuwa vyombo vyote vya habari vimepewa amri ya kutoandika habari za waraka wa TEC.
Haiwezi kuwa coincidence, yoooote yasiandike. Ni kweli Nape aliyapa maagizo ya kutoandika.
Waandike ile takataka ya TEC ?
 
Nape kasahau kwamba kuna watsap fcbk twitter na redio za Kanisa ambazo zinatangaza habari hizoo
 
Jana kulikuwa na tetesi kuwa vyombo vyote vya habari vimepewa amri ya kutoandika habari za waraka wa TEC.
Haiwezi kuwa coincidence, yoooote yasiandike. Ni kweli Nape aliyapa maagizo ya kutoandika.
Msema kweli nali halijaandika!?..anyway,lile ni suala la kanisani,magazeti hayawezi andika mambo ya nyumba za Ibada,tamko la maaskofu,hotuba ya ijumaa nk
 
Kanuni kuu ya kuhabarisha ni kuwa, kwa kadri unapozuia habari ya muhimu isiwafikie watu, ndivyo habari hiyo inavyokuwa bidhaa muhimu ya kutafutwa na watu wengi zaidi na mwisho wa siku watu wengi wataipata.
Hii imeonesha nani mfuga mbwa na nani ni mbwa tu,tofauti na walivyodhani
 
Jana kulikuwa na tetesi kuwa vyombo vyote vya habari vimepewa amri ya kutoandika habari za waraka wa TEC.
Haiwezi kuwa coincidence, yoooote yasiandike. Ni kweli Nape aliyapa maagizo ya kutoandika.
Siku hz hatusomi magazeti yalishapitwa na wakati
 
Back
Top Bottom