Maghorofa Magomeni kumbukumbu inayoishi ya John Pombe Magufuli

Maghorofa Magomeni kumbukumbu inayoishi ya John Pombe Magufuli

Screenshot_20220323-144154_Instagram.jpg
Screenshot_20220323-144209_Instagram.jpg

Kwanza ulikua unatuletea habari za upande wa pili zilizojaa propaganda za westerns. Leo umenifurahisha.....
 
Azory na Ben wamefanyaje?
Na wanahusikaje na Magomeni flats
Know the base of the story, kumbukumbu nyingine Ni watu aliowaua Jiwe. It is not maghorofa only to remember! Chawa watakumbuka maghorofa, watetezi wa haki za binadamu watawakumbuka watu/maiti waliokufa kwenye mikono yake
 
Know the base of the story, kumbukumbu nyingine Ni watu aliowaua Jiwe. It is not maghorofa only to remember! Chawa watakumbuka maghorofa, watetezi wa haki za binadamu watawakumbuka watu/maiti waliokufa kwenye mikono yake
Unajua ni watu wangapi wameuwawa kisiasa tangu tupate uhuru mwaka 1961?. JPM alikuwa ni rais wa awamu ya tano, zipo nne zilimtangulia.

Ukitaka kufanya tathmini ya kina rudi nyuma awamu zilizopita ili utoe hukumu au malalamiko yako kwa haki zaidi.
 
Nilikuwa nafuatilia runingani namna Rais Samia anavyowakabidhi majengo wale wananchi walioahidiwa kujengewa na hayati JPM. Alipoanza kuongea yule Bibi aliyekuwa ameongozana na Babu kama ndio wawakilishi wa wakazi 644 akawa mzalendo katika kutoa shukrani zake.

Kasimama mbele ya Rais SSH lakini akaanza kwanza kumshukuru JPM kwa maamuzi ya kizalendo ya kuamua kutumia kodi za wananchi kwa faida yao wenyewe ya kuwajengea majengo yatakayowasitiri wao na familia zao na yatakayokuwa ni sehemu ya mapambo ya kisasa ya jiji la Dar.

Kwamba Mungu amemchukua, ni maamuzi ya Mungu mwenyewe hakuna mwenye jeuri ya kuyapinga siku yake ikifika. Lakini kushukuru aliyekuwa na ujasiri wa kuyafanya ni deni ambalo bibi ameweza kulilipa vyema mbele ya Rais wa sasa.

JPM angeweza kutumia pesa iliyotumika katika kuhudumia anasa za tabaka la wenye vyeo, akaona hapana, ni lazima awajengee wakazi wa Magomeni makazi ya maana yatakayodumu kwa miaka mingi ijayo.

Angeweza kabisa kutumia pesa zilizotumika pale Magomeni katika kulipia safari za anasa za kwenda Dubai na kurudi kila mwisho wa wiki, angeweza kabisa kuzitumia zile pesa katika kuendeleza matanuzi yasiyodumu ya kibinadamu yanayofanywa kila siku na viongozi wengi wa kiafrika wa mataifa ya bara hili na hakuna mtu ambaye angeweza kumfanya lolote.

Kivitendo ilikuwa ni vigumu sana kwake kumtimizia kila aliyekuwa akimlilia njiani ili aweze kumtatulia shida zake mbalimbali, asingeweza kuwa na uwezo wa kufanya yote ya wasaidizi wake kwa wakati wote akiwa pale ikulu. Lakini hili la nyumba za kisasa kwa kaya 644 ni kielelezo au ni ishara ya utayari wake wa kuwasaidia wote wenye shida mbalimbali aliokuwa akikutana nao kila mara safarini.

Jukumu la kijasiri la kuyajenga makazi lilifanywa na JPM lakini jukumu la kuyatunza makazi hayo yasigeuke kuwa ni uchafu ulio karibu kabisa na katikati ya jiji, ni la wakazi wenyewe wa Magomeni wakiongozwa na yule Bibi aliyemshukuru hayati JPM mbele ya SSH.

Kimwili JPM alitutoka mwaka mmoja uliopita na siku chache. Lakini kila tutakapokuwa tukikatiza tukiwa ndani ya vyombo vya usafiri maeneo yale ya Magomeni tutakuwa tukimkumbuka hayati. Ataendelea kuishi kupitia ujasiri wa maamuzi ya kujenga makazi ambaye kila mtazamaji atakuwa akimkumbuka.

Alichokifanya JPM ni sawa na kile alichokifanya Hayati Karume kule Michenzani Unguja. Kwamba alikwisha kuondoka duniani tangu april 1972 lakini ushahidi wa upendo aliokuwa nao bado upo hai mpaka leo hii.

JPM alikuwa ni populist leader, na alitamka wazi bungeni siku ya kwanza kabisa alipohutubia. Kwamba anajivunia wingi wa wapiga kura waliompigia kura na atakuwa nao bega kwa bega. Ni maamuzi magumu sana kujenga majengo ya kisasa, kwani ni kama amekubali kuziba riziki nyingi za wasomi wenye kumsaidia kazi mbalimbali.

Ni kama alijua kuwa hana muda mrefu juu ya uso wa dunia, hivyo akaamua kuacha amejenga makazi kwa wakazi wa Magomeni. Ni maamuzi ya kizalendo ambayo siku zote hayawezi kukosa wa kuyapinga.

Ulale pema peponi JPM.
 
Kwani mabarabara, madaraja, nyumba,n.k hayakuwepo enzi za Mkapa,JK,Mwinyi,na Nyerere?

Huyu nyerere kitu gani cha maana amefanya? Huwa mnamtukuza sana lakini hana alichokifanya zaidi ya kutaifisha mali za watu na ukandamizaji...in short hamfikii magufuli hata kidogo though kuna mambo yamefanana kiasi flani......

SSH is the best president ever.....japo kuna mambo flani hivi hayako sawa, ila naamini ataweka sawa na kuendelea kufanya mazuri......abarikiwe mama.
 
Unapoongea hivi unakuwa huna tofauti na wale jamaa wanaoitwa kwa kingereza motivational speakers.

Wanapangilia hoja mpaka kilimo cha bagamoyo kinaonekana kina manufaa sana, sasa ingia ulime uone muziki wake.
Sio hadithi that is what has transpired so far with physical evidence nyumba za TBA si hizo zimezinduliwa leo na gharama ya mradi tumepewa.

Na plan tunaambiwa ni hiyo part buy, part rent kwa watakao bahatika kupata hizo nafasi. Provided TBA wanasema ukweli motisha yao sio profit but return on investment hizi nyumba zitakuwa affordable.

Just quick maths given the average unit cost waki demand 15% to 20% percent kama down payment ya kununulia nyumba na rent ya laki 3 tu kwa mwezi + services charges, na serikali wakishauriwa VAT kwenye rent iwe 5% tu; wafanyakazi wengi wa serikali wanazimudu na ndani ya 25 years inakuwa mali zao.

Na kwa upande wa TBS ukifanikiwa kupata 15% to 20% ya mradi wote jumlisha una income ya rent kila mwezi unaanza kabisa ujenzi mpya eneo lingine kulenga watu hao hao wenye shida zaidi ya makazi.

Sio nyumba million 200 halafu uweke deposit 30%, baada ya hapo kilichobaki ulipe kwa mortgage ya 15% interest annually for the remainder of the years.

Nyumba kama hizo bora uwe na cash ya kununua, lakini kuchukua mortage nyumba wewe ni hamnazo kweli kweli; ndio maana zimedoda project zao zote expensive nyumba wanapangisha awajauza hakuna mtu timamu atanunua nyumba zile.

Baada ya kuona biashara imedoda wakaanza kulia ohoo waachieni wageni wamiliki ardhi ili wawe comfortable kununua nyumba za NHC. Sasa uliambiwa ujenge nyumba za wageni au watanzania wa kawaida, huyo dogo Ridhiwani anatakiwa amrudie baba yake amwambie kamuingiza cha kike kwa Nehemia he just doesn’t have the business acumen.
 
Waliompiga risasi ndio hao unaowasifia hapa eti maghorofa
Alipigwa risasi bosi wa zamani wa usalama wa Taifa na kuuwawa tena akiwa amenyoosha mikono juu, sembuse huyo mheshimiwa mbunge!.

Haya mambo kama wewe ni mgeni wa taifa hili unaweza kueleweka namna unavyolialia.
 
Back
Top Bottom