Maghorofa Magomeni kumbukumbu inayoishi ya John Pombe Magufuli

Maghorofa Magomeni kumbukumbu inayoishi ya John Pombe Magufuli

Unajua imetumika kiasi gani cha pesa kujenga yale maghorofa?. Unajua kuwa angeweza kuzitumia pesa hizo kwa matumizi ya anasa tu?.

Shame on you kwako wewe ambaye unajua kulaumu tu.
Hizo billioni hamsini ni sawa na barabara kutoka Dar hadi kwa mfipa tu. Sasa hujiulizi waliomtangulia hawakuweka miradi ya Bilioni hizo? Mradi upi ni gharama na manufaa zaidi katika ya Bilioni 50 za nyumba Dar na Bilioni zaidi ya 400 za barabara ya Dodoma Arusha? Hakuna legacy unique kwa Magufuli.
 
Alipigwa risasi bosi wa zamani wa usalama wa Taifa na kuuwawa tena akiwa amenyoosha mikono juu, sembuse huyo mheshimiwa mbunge!.

Haya mambo kama wewe ni mgeni wa taifa hili unaweza kueleweka namna unavyolialia.
Issue sio wadhifa wa mtu, issue Ni uhai wa mtu
 
Huyu nyerere kitu gani cha maana amefanya? Huwa mnamtukuza sana lakini hana alichokifanya zaidi ya kutaifisha mali za watu na ukandamizaji...in short hamfikii magufuli hata kidogo though kuna mambo yamefanana kiasi flani......

SSH is the best president ever.....japo kuna mambo flani hivi hayako sawa, ila naamini ataweka sawa na kuendelea kufanya mazuri......abarikiwe mama.
Ulikuwa hujazaliwa wakati wa utawala wa Nyerere so sio kosa lako kuona hakuna la maana alilowahi kufanya. Na ulikuwa hujazaliwa mwaka 2020 wakati Anthony Diallo alipoyaorodhesha mambo aliyofanya Nyerere kwa kulinganisha na yale ya Magufuli.

Maana Magufuli alinunua ndege, Nyerere hakununua hata moja. Magufuli alianzisha mradi wa umeme wa Stiglers ilhali yale mabwawa ya umeme ya Mtera,Ruvu,nk anayojivunia Nyerere hakuyajenge yeye bali yalishuka kutoka Mbinguni kama Qur'an.
 
Hizo billioni hamsini ni sawa na barabara kutoka Dar hadi kwa mfipa tu. Sasa hujiulizi waliomtangulia hawakuweka miradi ya Bilioni hizo? Mradi upi ni gharama na manufaa zaidi katika ya Bilioni 50 za nyumba Dar na Bilioni zaidi ya 400 za barabara ya Dodoma Arusha? Hakuna legacy unique kwa Magufuli.
Cha muhimu amefanya alilolifanya kwa vitendo na leo mradi umefunguliwa utaanza kutumiwa na wakazi waliokuwa wakiishi hapo. Hicho ndicho cha muhimu, hizo habari nyingine za bilioni sijui mia sijui hamsini ni mbwembwe tu.
 
Ulikuwa hujazaliwa wakati wa utawala wa Nyerere so sio kosa lako kuona hakuna la maana alilowahi kufanya. Na ulikuwa hujazaliwa mwaka 2020 wakati Anthony Diallo alipoyaorodhesha mambo aliyofanya Nyerere kwa kulinganisha na yale ya Magufuli.

Maana Magufuli alinunua ndege, Nyerere hakununua hata moja. Magufuli alianzisha mradi wa umeme wa Stiglers ilhali yale mabwawa ya umeme ya Mtera,Ruvu,nk anayojivunia Nyerere hakuyajenge yeye bali yalishuka kutoka Mbinguni kama Qur'an.

Wananchi wanahitaji maendeleo, kwa nyerere hii kitu haikuwepo....labda ungesema mwinyi hapo sawa.
 
Nikiweka ushabiki pembeni, SSH ni jembe kweli kweli kamanda wangu....though magufuli nae nilimkubali kwa kiasi flani....sisi wa kanda ya ziwa tunamshukuru kwa machache aliyotuachia kama vile barabara za lami, taa, traffic lights, daraja la busisi na mengineyo baadhi.

For me, mama huyu bado naimani nae.
Mama she is okay, tatizo ni kule kwenye pesa ! Watu wakiziona pesa akili zinaruka madudu yanaanza !! Let's wait and see !!
 
John Pombe Joseph Magufuli - Rais anayeendelea kuishi mioyoni mwa Watanzania hata baada ya kututoka kimwili. Aendelee kupumzika kwa amani. 🙏
 
Nyerere labda haumfahamu. Viwanda vyote vya awamu ya kwanza vilivyotaifishwa awamu ya tatu ni kazi ya Nyerere.
Kumbe humu jf vijana ni wengi sana !! Nyerere wakati anang'atuka aliacha viwanda zaidi ya 400 na tukisema viwanda wajue vilikuwa viwanda kweli kweli ! Hayati Mkapa aliwahi kukiri kwamba katika uongozi wake kitu anachojutia sana kukifanya ni kubinafsisha vile viwanda !! Mzee Mwinyi alichofanya ni kuachia watu waingize bidhaa kutoka nje kiholela na ndipo maadili yote yalianza kuporomoka yakaanza madili !!!
 
Magu wataishi miaka mitano buree........vs 3months za Samia...............
 
Hivi UDSM, Mloganzil, uwanja wa michezo wa Mkapa, mabwawa ya maji ya umeme Kidatu, Ntera, Nyumb ya Mungu, sokoine university, university of Dofoma, viwanja vya ndege vyote kama Kia n.k alijenga Magu?
Mbona mnataka kilazimisha kutusahaulisha maiti zilizookotwa kwenye mifuko, kupotea kwa wapinzani kuliko kithiri, kushambuliwa risasi na kutekwa kwa wapinzani kusiko mithirika wakati wowote?
Jamani hakuna mtoto wa kumdanganya kwa pipi, ukatili tutaukumbuka tu!
 
Cha muhimu amefanya alilolifanya kwa vitendo na leo mradi umefunguliwa utaanza kutumiwa na wakazi waliokuwa wakiishi hapo. Hicho ndicho cha muhimu, hizo habari nyingine za bilioni sijui mia sijui hamsini ni mbwembwe tu.
Wazee wa legasi kazi mnayo
 
Nilikuwa nafuatilia runingani namna Rais Samia anavyowakabidhi majengo wale wananchi walioahidiwa kujengewa na hayati JPM. Alipoanza kuongea yule Bibi aliyekuwa ameongozana na Babu kama ndio wawakilishi wa wakazi 644 akawa mzalendo katika kutoa shukrani zake.

Kasimama mbele ya Rais SSH lakini akaanza kwanza kumshukuru JPM kwa maamuzi ya kizalendo ya kuamua kutumia kodi za wananchi kwa faida yao wenyewe ya kuwajengea majengo yatakayowasitiri wao na familia zao na yatakayokuwa ni sehemu ya mapambo ya kisasa ya jiji la Dar.

Kwamba Mungu amemchukua, ni maamuzi ya Mungu mwenyewe hakuna mwenye jeuri ya kuyapinga siku yake ikifika. Lakini kushukuru aliyekuwa na ujasiri wa kuyafanya ni deni ambalo bibi ameweza kulilipa vyema mbele ya Rais wa sasa.

JPM angeweza kutumia pesa iliyotumika katika kuhudumia anasa za tabaka la wenye vyeo, akaona hapana, ni lazima awajengee wakazi wa Magomeni makazi ya maana yatakayodumu kwa miaka mingi ijayo.

Angeweza kabisa kutumia pesa zilizotumika pale Magomeni katika kulipia safari za anasa za kwenda Dubai na kurudi kila mwisho wa wiki, angeweza kabisa kuzitumia zile pesa katika kuendeleza matanuzi yasiyodumu ya kibinadamu yanayofanywa kila siku na viongozi wengi wa kiafrika wa mataifa ya bara hili na hakuna mtu ambaye angeweza kumfanya lolote.

Kivitendo ilikuwa ni vigumu sana kwake kumtimizia kila aliyekuwa akimlilia njiani ili aweze kumtatulia shida zake mbalimbali, asingeweza kuwa na uwezo wa kufanya yote ya wasaidizi wake kwa wakati wote akiwa pale ikulu. Lakini hili la nyumba za kisasa kwa kaya 644 ni kielelezo au ni ishara ya utayari wake wa kuwasaidia wote wenye shida mbalimbali aliokuwa akikutana nao kila mara safarini.

Jukumu la kijasiri la kuyajenga makazi lilifanywa na JPM lakini jukumu la kuyatunza makazi hayo yasigeuke kuwa ni uchafu ulio karibu kabisa na katikati ya jiji, ni la wakazi wenyewe wa Magomeni wakiongozwa na yule Bibi aliyemshukuru hayati JPM mbele ya SSH.

Kimwili JPM alitutoka mwaka mmoja uliopita na siku chache. Lakini kila tutakapokuwa tukikatiza tukiwa ndani ya vyombo vya usafiri maeneo yale ya Magomeni tutakuwa tukimkumbuka hayati. Ataendelea kuishi kupitia ujasiri wa maamuzi ya kujenga makazi ambaye kila mtazamaji atakuwa akimkumbuka.

Alichokifanya JPM ni sawa na kile alichokifanya Hayati Karume kule Michenzani Unguja. Kwamba alikwisha kuondoka duniani tangu april 1972 lakini ushahidi wa upendo aliokuwa nao bado upo hai mpaka leo hii.

JPM alikuwa ni populist leader, na alitamka wazi bungeni siku ya kwanza kabisa alipohutubia. Kwamba anajivunia wingi wa wapiga kura waliompigia kura na atakuwa nao bega kwa bega. Ni maamuzi magumu sana kujenga majengo ya kisasa, kwani ni kama amekubali kuziba riziki nyingi za wasomi wenye kumsaidia kazi mbalimbali.

Ni kama alijua kuwa hana muda mrefu juu ya uso wa dunia, hivyo akaamua kuacha amejenga makazi kwa wakazi wa Magomeni. Ni maamuzi ya kizalendo ambayo siku zote hayawezi kukosa wa kuyapinga.

Ulale pema peponi JPM.
Kule Mbeya ameacha kumbukumbu gani?
 
Ww ndio huna akili ,kwa kuwa huwezi kujenga hoja.Unabaki kuongea upuuzi tupu.Magufuli atabaki kuwa Rais aliyefanya mengi Sana kuliko Rais yeyote.

Alikuwa Rais wa kuhudumia watu.

Na kazi zake zinaendelea.

Sio Rais wa kuchekacheka tu.
MKIRU ALIUA WATU ZAIDI YA 400, RUBBISH
 
Kama alipata neema ya kuungama kabla ya mauti basi ana heri.

Mungu huwa anasamehe bila kujali udogo au ukubwa wa dhambi.
Stupid unaua watu kwa jeuri ya kutaka kutawala milele eti utaungama. Achà.life likandamizwe na shetani Mkuu.
 
Back
Top Bottom