Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Silinde anaweza akachaguliwa halafu mleta maji akapigwa chiniMagufuli: Msipomchagua Silinde sileti maji Tunduma
Huyu sio Raisi kabisaaa!!!
Hii inaitwa kuku akinya sawa ila bata.......Dr Mahera ana maoni gani?
Aache kukusanya kodi ya wakazi wa Tunduma pia. Asiwatolee VITISHO ili wampe kura na pamoja na VITISHO vyake Silinde njeeeee
Unawaongelea wana Tunduma gani Wa Chato au?Chadema mnadaiwa 2.5billion za miradi ya maji, hatuwezi kuendelea kupoteza pesa za umma kwa kupalilia majizi. Tumbua chadema lete SILINDE ili tuweke maendeleo zaidi. Msema kweli mpenzi wa Mungu, Tunduma wameamua kuokoka, leo wamebatizwa kwa moto na wamepokea upako. Wewe unadai wamefokewa hahahahah tulia ubatizo uzame
Halafu utamuona yule kinyamkera mahera mwenye rangi ya kenya kakaza uso wa nyani kwa Tundu Lissu. Huu sio udhalilishaji wa taasisi ya Urais? Au kuna maadili zaidi ya haya?Kuna methali ya kiswahili inasema mfupa wa kulazimisha ukivunja chungu. Kwa kila aliyefatilia hotuba ya Dr. Magufuli pale Tunduma atagundua kuwa CCM haikubaliki kama Chadema, mbaya zaidi ni kutokana na mgombea ccm inayomnadi, maana haaminiki tena kwa wananchi wa Tunduma, kwa tabia yake ya usaliti. Ndio maana kwenye kura za maoni ndani ya chama wajumbe walimpiga chini. Sasa Dr. Magufuli analazimisha wananchi wamchague mtu ambaye siyo chague lake. Inawezekana mzee Magu anampango wa kumpa uwaziri au unaibu kama wote wawili watapita maana bado ni kitendawili.
Sasa kwa tabia ile ya kulazimisha wananchi wamchague Silinde itachochea uvunjifu wa amani maana wananchi hawatamchagua, na kwa kuwa yeye anamtaka, itabidi vyombo vya dola vilazimishe kama kawaida, hapo ndio hofu yangu kuwa kunaweza kutokea uvunjifu wa amani.
Mh. Magufuli kama unataka nchi yetu ibaki salama uwe makini kwa kauli zako na pia acha kulazimisha ili wananchi wafanye maamuzi yao.
Maendeleo yanachama kwa mtazamo wa DR Magufuli.
======
DKT. MAGUFULI: MKINICHANGANYIA SILETI MRADI WA MAJI
Dkt. John Magufuli, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM amesema katika muhula ujao ameshaweka mipango ya kupeleka maji Ireje yaweze kufika Tunduma.
Amesema wakimchanganyia wabunge, yaani wakimchagua mbunge asiye wa CCM basi hatopeleka miradi ya maji Tunduma.
Amesema miaka mitano iliyopita aliwabembeleza na hii ni mara ya mwisho yeye kuwaomba watu wa Tunduma. Amesema hawatishi ila moyo unauma kuona wanamchanganyia.
Amesema ili wapate maji ni lazima wamchague David Silinde, mgombea ubunge wa Tunduma kwa tiketi ya CCM ambaye ni mbunge wa Momba anayemaliza muda wake kwa tiketi ya CHADEMA.