Magufuli alifariki miezi 3 iliyopita lakini unaweza kudhani alifariki kabla ya Nyerere

Magufuli alifariki miezi 3 iliyopita lakini unaweza kudhani alifariki kabla ya Nyerere

Juzi nilikuwa nimekaa sehemu kimya, nikakumbuka kifo cha Magufuli. Nikajiuliza hivi kafa lini? Nikagundua ni miezi 3 tu iliyopita. Nikashtuka, ashaanza kupotea kwenye kumbukumbu zangu zaidi hata ya Nyerere aliyefariki miaka 22 iliyopita.
Post yako hii inadhihirisha jinsi ilivyo ngumu kumsahau JPM, umeshindwa kuvumilia kivuli chake hadi umepost humu!

Ni hivi, hata mama hataweza kufuta mwelekeo wa Tanzania mpya iliyoanza kujengwa na JPM, kwa visera vyake vya kufurahisha watu flan flan vinavyojaribu kuirudisha Tanzania misri. Na mioyo yetu ikimkataa atapata tab sana.
 
Kufa ni kupotea...

Siku zote story huisha na kumbukumbu husahaulika, hii inamisha sisi sote tunapita...
 
Mwandishi wa post unateseka ukiwa wapi. Shujaa amezaliwa tena kwenye moyo mamilion ya watanzania.
 
Kuwa president wa nchi hata kaa asahaulike kwenye historia ya nchi hii labda nchi hii ije ifutwe
Mimi nikiwa rais nitamfuta Magufuli kwenye kumbukumbu za nchi,nikiwa mbunge ntapeleka hoja binafsi. futa kabisa ameacha kumbukumbu mbaya.
 
Si kweli hasa. Kwa tuliyoyapitia chini ya utawala wake sio rahisi kumsahau mapema! Tulijawa woga uso kifani. Tulikosa uhuru. Ni Rais pekee ndiye alikuwa mtu mwenye busara na akili kuliko watanzania wote. Pathetic!

Huwa nafikiri kuwa pengine urais wa Samia sasa unaonekana "mzuri" kwa kuwa tu urais wa JPM ulikuwa wa hovyo!
 
Nyerere alikuwa mioyoni,magufuli alikuwa kwenye media
Si kweli hasa. Kwa tuliyoyapitia chini ya utawala wake sio rahisi kumsahau mapema! Tulijawa woga uso kifani. Tulikosa uhuru. Ni Rais pekee ndiye alikuwa mtu mwenye busara na akili kuliko watanzania wote. Pathetic!

Huwa nafikiri kuwa pengine urais wa Samia sasa unaonekana "mzuri" kwa kuwa tu urais wa JPM ulikuwa wa hovyo!
Ubabe ulitawala
 
Kashasahaulika mazima
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Hakuna mwenye akili timamu akamkumbuka dikteta, aliyebariki utekaji na kupigana risasi,maiti kutupwa kwenye viroba, kauli za ovyo Kama "BAKINI NA MAVI YENU MAJUMBANI"
Kukumbukwa maana yake nini, si ndio kama hivi kutajwa tajwa iwe mazuri au mabaya. Mfano wa mtu ambaye amesahaulika ni kama Maalim seif ambaye hausikii akitajwa tajwa kama ambavyo alivyokuwa hai, ila Magufuli kutwa anatajwa ni ngumu kuacha kutajwa Magufuli hasa katika uongozi wa Mama samia maana hata jana Rais Samia alifikisha hizo siku zake 100 pia Magufuli katajwa sana tu na humu JF ndio hapiti siku bila kutajwa Magufuli.
 
Back
Top Bottom