Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Maamuzi yanayotolewa yanaonyesha kabisa hakuna mawasiliano kati ya Raisi na watendaji wake Kwa nini Raisi asiwe anafanya vikao na watendaji wake kuwaonyesha/kuwaeleza anachokitaka kuliko kusubiri wanavyokosea na kuwatumbua ?
Unafikiri huu utaratibu wa kuwavizia wanapokea na kuwatumbua utamsaidia Raisi ?
Kwahio kwa mfano kama Mramba aliambiwa asiendelee na mkataba na Symbion ambao wanataka pesa yao iwe wamezalisha umeme au hawajazalisha.
Je ameshauriana vipi na waziri kuhusu hili la kuongeza bei ya umeme hata baada ya kupeleka maombi EWURA?
Inaonekana amekikuka maagizo ya raisi kwa kwenda EWURA moja kwa moja kwamba liwalo na liwe licha ya kuagizwa pale Kinyerezi mwaka jana.
Au wewe umeelewaje kwenye hili?