Kuhusu huyu wa NHC Serikali itakuja kushtuka wakati Mabenki yatakapo kuja kupiga mnada Nyumba za biashara alizo jenga kiholela na kwa gharama lukuki, nina uhakika NHC haitamudu kurudisha mkopo on time kutokana na Mashirika mengi na watu binafsi kujiingiza katika biashara ya Real Estate, hilo litakapo tokea yeye atakuwa amekwisha sepa!!
Kwa bahati mbaya Wizara mama wala hawajalishtukia hili, wanamsifia sifia tuu - wanampa passport ya kuchukua mikopo Benki kiholela mradi kaamua yeye kujingiza kwenye projects ambazo nyingine ni highly questionable wanaona sawa tu.
Wakati mwingine aliwahi kupendekeza eti baadhi ya majengo ya Shirika anayojenga City Center na nje eti wawauzie wageni!! - Kasahau kwamba unapo uza nyumba kwa mgeni unamuuzia na aridhi indirectly!!
Binafsi sina tatizo na jamaa as a person hisipo kuwa modus operandi yake ndiyo yenye walakini mkubwa sana, atakuja kulitia hasara ya matillioni Taifa Serikali hisipo kuwa makini/ku-regulate ma Mega Project ya jamaa huyu - yanatisha sana na hayana mwelekeo mzuri.