Uchaguzi 2020 Magufuli kakosea sana kampeni zake mkoani Mara. Je, haujui mkoa ule au hapendi watu wake?

Yaani ni sawa na watoto wako badala ya kuwafugia kuku ili waje wale mayai tunawafugia chatu waje waliwe wao.
#CHAGUACCMKOMESHAWANAO
Na kwa nini dola inamshikilia huyu jamaa asiyefaa..

Si waache adondoke kwenye sanduku la kura. Ndio njia rahisi kumpumzisha..

Anaharibu hata umoja walioujenga kina Nyerere
 
Mgombea wa aina hii hatufai wa Tanzania, Hayupo kujenga umoja wa watu bali kubomoa miaka yote CCM imekuwa madarakani waseme ni sehemu gani ndani ya hii nchi inakila kitu

Kwa kifupi Ni aibu tokea Uhuru Hadi Leo bado watu wanashida ya maji, huduma za afya duni, makazi mabovu nyumba za udongo au nyasi, elimu duni, umasikini, hakuna ajira... Nk.
 
Huyo jamaa inawezekana nae ni kundi moja na Bashite i.e wote kichwani ni sifuri.
 
Mkuu, nilidhani kimeandikwa "Sasa unaingia Mkoa wa Mara". Neno KARIBU hakuna. Wanaume wale. Ukiingia jiaminishe. Hakuna aliyekukaribisha. Acha kulialia. Hahaha, kumbe Magu hawajui.
SASA UNAINGIA MKOA WA MARA.

Hakuna karibu.
 
Kwa kifupi Ni aibu tokea Uhuru Hadi Leo bado watu wanashida ya maji, huduma za afya duni, makazi mabovu nyumba za udongo au nyasi, elimu duni, umasikini, hakuna ajira... Nk.
Toka 1961 bado tunazungumza kujenga ZAHANATI na kuchonga MADAWATI????

CCM pumzikeni.
 
Asilimia 100 ya majimbo yote Tanzania ni masikini wa kutupwa. Sema mengine yamezidi umasikini.
hasa ya vijijini, hili huchagizwa sana na wadau wa maendeleo kutopenda kuwekeza miradi yao vijijini, pia hata wasomi hawapendi kuishi vijijini laiti wadau na wasomi wangewekeza maeneo wanakotoka nadhani vijijini pia pangekua na neema bt kwa hili serikali huwezi kuilaumu.
 
Usiseme kinadharia wewe. Umefika Mara? Kibao chao kimeandikwa "SASA UNAINGIA MKOA WA MARA". Neno KARIBU halipo.
Haya bwana na kibao chao. Nimekuelewa lakini Nungunungu na miba zake bado wachumba wanamjia na mimba wanamdunga.
 
Kama aliyasema hayo amekosea sana tena sana, akumbuke sio kila mtu ni mfatiliaji wa siasa hilo kundi linaumizwa na hao wapenda siasa lakini pia anatakiwa ajue maendeleo ni HAKI ya kila Mwananchi wa nchi husika, Siasa zisiifanye serikali kushindwa kutimiza majukumu yake, kama waliruhusu mfumo wa vyama vingi basi hawana budi kutenda mema kwa kila raia haijalishi ni chama gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…