Magufuli na Lissu kukutana Kigoma kwa mara ya kwanza leo

Magufuli na Lissu kukutana Kigoma kwa mara ya kwanza leo

Shida iliyopo ni rais kuwa pia mgombea.
Leo kabaki Kigoma kuzindua jengo la Mahakama Kama rais wa nchi sio Kama mgombea hivyo NEC hawahusiki na mambo ya ratiba ya rais.
Ingawa ratiba ya uzinduzi itaisha mapema Sana.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
Magufuli asitufanye wajinga sana, anatumia mbinu ya kufanya kazi za serikali ili kuhalalisha matumizi ya fedha anazochota hazina. Ni kwamba msafara wake wote utatumia fedha za serikali kwa mafuta ya magari na posho za wote alioambatana nao.
 
Chonde chonde Lissu, ... yasije yakatokea ya mgongano wa msafara wa Bob Wine na Museven, yaliyoleta tafrani huko Uganda!
NB: Kuna watu wanatafuta fursa tu waweke mpira kwapani!
😅
👊 ✌️✌️✌️💥
 
Hii kama siyo fujo ni nini.

Ratiba ya NEC inasoma Lissu atakuwa Kigoma,Magufuli ndiye kaingilia kalazimisha kubaki Kigoma,

Kabaki kupokea wageni na kuzindua jengo la mahakama tangu lini wageni wakapokewa uwanja wa mpira na tangu lini jengo la mahakama likazinduliwa uwanja wa mpira.
"Ratiba ya NEC iheshimiwe"
 
Kila mtu aachwe afanye mambo yake hakuna habari za kuingiliana.

Lissu apige kampeni na Magu ampokee mgeni wake.
Ni kweli kila mtu aendelee na ratiba yake. Ila naamini Lissu katika kampeni zake ataondokana na uzushi kuwa Rais Magifuli ameharibu uhusiano wa kimataifa na hata nchi za jirani. Leo Rais wa Burundi kaja. Hivi karibuni Uhuru na Kagame wamekuja Tanzania, tena Chato.
 
Kwa mjibu wa ratiba Tundu Lissu atakuwa na kampeni Kigoma mjini leo jioni katika maeneo ya Mwanga center. Wakati huohuo Mh Magufuli atakuwa Lake Tanganyika, atakuwa na rais wa Burundi ambaye amealikwa katika uzinduzi wa jengo la mahakama.

Hofu yangu ni, je, CHADEMA wataruhusiwa kufanya maandalizi mazuri kwa kumpokea mgombea wao wa uraisi? Police wajipange kukabiliana na vurugu zinazoweza kutokea kwa mashabiki Hawa wa vyama.
CCM akili zao zipo Likizo
 
Tundu Lisu itabidi apishe shughuli ya kitaifa kwanza.

Yeye aendelee ni mkutano wake kesho maana hawezi kuingilia shughuli mahsusi ya mkuu wa nchi ambaye tayari yuko Kigoma!
Kwani yeye ndiye anayejipangia ratiba? Tume ya uchaguzi ilipanga leo Tundu Lissu afanye kampeni mkoani Kigoma. Sasa ni yeye au huyo aliyemualika rais wa nchi jirani ndiye aliyeingilia ratiba?
Toa hoja kwa kufikiria kimapana kwanza
 
Naombea siku moja magufuli na tundu lissu wakutane watoe tofauti zao wasemehane tujenge nchi kwa furaha
 
Ratiba ya NEC inaelekeza hivyo, Anaeingilia ratiba za tume ni Magufuli sababu uzinduzi wa jengo la Mahakama haufanyiki katika kiwanja bali katika Jengo lenyewe. Huyo mrithi wa Nkuruzinza na M7 wanaingilia uchaguzi wa ndani Tanzania, Hii haikubaliki hata kidogo, Kama ni ziara za kiserikali kwanini Magu asiwaalike viongozi wa nchi zilizo na demokrasia kama Marekani Ufaransa na Ujerumani?
 
Hii kama siyo fujo ni nini.

Ratiba ya NEC inasoma Lissu atakuwa Kigoma,Magufuli ndiye kaingilia kalazimisha kubaki Kigoma,

Kabaki kupokea wageni na kuzindua jengo la mahakama tangu lini wageni wakapokewa uwanja wa mpira na tangu lini jengo la mahakama likazinduliwa uwanja wa mpira.
Mkuu kuna vitu vingine ni sawa na matapishi ya akili kwamba hata mtoto mdogo anajua kabisa kuwa haya ni matapishi. Alafu mbaya zaidi unakuta mtu anasema eti Lissu asimamishe kampeni leo mpaka kesho huku akijua kabisa ratiba inapangwa na Tume ya uchaguzi.
Maajabu haya uzinduzi wa jengo kufanyika uwanja wa mpira na si kwenye jengo husika! Tuseme tu wazi kuwa kuna kitu kimepangwa hapo Kigoma leo ili ionekane kampeni za Chadema zimesababisha fujo.
 
Watulie kwanza mkuu wa nchi amaliza shughuli za muhimu za Kitaifa izo kampeni za Lissu zipo tu ziwe postponed
 
Back
Top Bottom