Mahakama Kuu yafuta mashtaka 14 kati ya 25 ya Masheikh wa Uamusho

Mahakama Kuu yafuta mashtaka 14 kati ya 25 ya Masheikh wa Uamusho

Mnazunguka zunguka tu.

Masheikh wa UAMSHO wako ndani sababu ya MUUNGANO!

WALIUGUSA VIBAYA MUUNGANO!

Fuatilia video zao utaelewa.

Walikuwa wanawaamsha Wazanzibar kuachana na SIASA za u-CCM na u-CUF ambazo zilikuwa zinawagawa na kwamba adui wa kweli wa Taifa lao ni MUUNGANO!

Na Wazanzibari kwa wingi wao walianza kuwaelewa.
Yaani wasingewekwa ndani; pengine hivi tunavyoongea huu MUUNGANO, hata Kama ungekuwepo, usingekuwa hivi ulivyo!

Dini ilitumika Kama kiungo tu kwavile majority ya Wazenji ni Muslims. Ukiwakusanya Kama waislam inakuwa rahisi kuzungumza 'lugha' moja!
We kweli umewafuatilia vyema uamsho, mimi ni mznz na kipindi cha harakati za uamsho nilikuwepo zenji kdg nikaenda zangu chuo bara, niliporudi kutoka chuo nikakuta harakati zimepamba moto na posters za Zanzibar yenye Mamlaka kamili zikiwa zimeenea kila kona...nikasema ohoo tunakoelekea moja wapo litatokea ama muungano kuvunjika au masheikh yatawakuta yaliyomkuta hayati Aboud Jumbe Mwinyi, Rais mstaafu wa Zanzibar alipojaribu kuuchokonoa Muungano.

Hawa watu nimeshaeleza humu hawakuwa na shida na dini ya mtu ila Zanzibar kamili kwa sababu kwa maono yao waliona Zanzibar inabinywa na Tanganyika, hivyo walikuja kama wakombozi.
 
Watanzania ni watu wa mikumbo sana unaweza ukamjua mtu A ni mwizi wa miaka mingi ila huna ushahidi kumkamata mtu na ushahidi wa ugaidi sio rahisi mpaka leo hii MAREKANI hawana ushahidi kama Osama alihusika moja kwa moja Sept 11 Ndio mana hawakumbeba kumpeleka mahakamani ... ngoja yaanze tena ndio mtakumbuka nini kiliwaweka ndani

Hawana ushahidi wa Osama kwa kua alikua ni planner lakini wafanyaji wa matukio waliwakamata na kuwajuwa, Sasa hizi kesi tunazoambiwa zimefanywa na uamsho mbona hakuna wafanyaji matukio waliokamatwa? Eti makanisa yaliochomwa yote hakuna hata mchomaji mmoja aliekamatwa? watiaji Tindi kali wote hakuna hata mmoja aliekamatwa?

Mkuu Yale matukio yalifanywa na TISS ili kujitengenezea mazingira ya kuwakamata hawa mashehe, mana jamaa walikua ni pain in the Ass kwa CCM.
 
Siwezi kuamini unachokisema.

Ingawa matukio yamekuwa ni ya siku nyingi lakini kumbu kumbu bado tunazo.

Yule aliyempiga risasi padre na baadaye kukamatwa nadhani baada ya kuminywa ndiye aliyataja 'cindykate' nzima.

Hizo chuki za kidini zilionekana wazi Zanzibar enzi hizo na tangia wakamatwe pakawa shwari mpaka leo.

Haki inayosemwa wamenyimwa ni ya kutokufikishwa mahakamani kwa muda unaotakiwa na kuhukumiwa kisheria na siyo kwamba wote hao wanaotuhumiwa hawajatenda moja kwa moja waliyoshitakiwa nayo na wanapakaziwa.
 
Kwa ili mnamuonea mwenda zake, hao wamekamatwa wakati wa Jk..

Walikamatwa na Jk ana nangwa mwendazake kwa nini hanangwi mama Samia?

Wamekaa korokoroni kwa miaka mingi wakati wa JK? Wakati wa JPM je? Unadhani watakaa muda gani wakati wa SSH?

Dhamira ya kuwapa viongozi hawa watatu kuwapa wengine haki ungali huioni?

Tofauti ya mwendazake na Samia kuhusiana na mwendazake kutoiona, labda kama umetupia miwani ya mbao.

Kwa maana nyingine mwendazake angesalia madarakani hawa jamaa wangeozea jela.
 
Yule aliyempiga risasi padre na baadaye kukamatwa nadhani baada ya kuminywa ndiye aliyataja 'cindykate' nzima.

Aliyekamatwa kwa kumpiga risasi Padri yupo huru mkuu, walimuachia baada ya kukosa ushahidi wowote, Na alikua mgombea wa ACT kwenye jimbo Fulani safari hii.
 
Ukiona hadi Habari kama hii imepewa maombi ya baraka kutoka kwa wakristo basi amini kuwa Mungu yupo!! Tupendaneni wanandugu...
Inshaallah Wapate kuachiwa huru [emoji120]
 
Siwezi kuamini unachokisema.

Ingawa matukio yamekuwa ni ya siku nyingi lakini kumbu kumbu bado tunazo.

Yule aliyempiga risasi padre na baadaye kukamatwa nadhani baada ya kuminywa ndiye aliyataja 'cindykate' nzima.

Hizo chuki za kidini zilionekana wazi Zanzibar enzi hizo na tangia wakamatwe pakawa shwari mpaka leo.

Haki inayosemwa wamenyimwa ni ya kutokufikishwa mahakamani kwa muda unaotakiwa na kuhukumiwa kisheria na siyo kwamba wote hao wanaotuhumiwa hawajatenda moja kwa moja waliyoshitakiwa nayo na wanapakaziwa.
Afu kinano cha hawa jamaa kimetoa somo kubwa sana kwa wananchi wengine walio salia zanzibar kuwa ujinga ule haitakiwi kabisa
 
Labda ungeniuliza nchi ya zanzibarrrrrrr IPO wapi.
Naomba unitajie hiyo Tanganyika iko wapi hapa duniani na inatumia bendera ipi kiuwakilishi halali kimataifa kwa mwaka huu 2021
 
Back
Top Bottom