Mahakama Kuu yafuta mashtaka 14 kati ya 25 ya Masheikh wa Uamusho

Mahakama Kuu yafuta mashtaka 14 kati ya 25 ya Masheikh wa Uamusho

Ukiona wameachiwa... Ujuwe washadhibitiwa!!!..

Mda utaongea....

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
Nlichokisikiaga mimi ni kuwa hao jamaa hawajasingiziwa kabisa.

Kumbuka walianza toka awamu ya Jk na Shein kule Zanzibar.

Jk akashauriwa na kupewa maelezo yote vile jamaa walivyohusika, na bila kutafakar mara mbili akaamua awaweke ndani.

Jk hakuwa mdini, kumbuka hata Shekh Pondo alkuwa akipambana na Utawala wa Jk na alikuwa akisulubiwa mno Shekh Ponda.

Hayat Magufuli alipokea tu kijiti kwa kuelezwa uhalisia wa hawa mashekh.

Sijajua hasa Rais Samia ni kitu amekiona ama kimepangwa juu ya hili jambo.
 
Kesi na kushikiliwa kws masheikh wa uamsho kunafikirisha sana (iwe Wana hatia au hawana). Iweje baada ya hao masheikh kukamatwa na kuhamishiwa Bara, Zanzibar kumekuwa shwari, yale mashambulio ya tindikali na risasi kwa wageni yamekoma kabisa.

Vv
Kaka, hawa jamaa walikutwa na hatia.

Kama sikosei ktk upelelezi wa hawa watu, Tz tulipata msaada nje ya nchi chini ya utawala wa Jk.

Na wale jamaa walitaka hawa wahukumiwe moja kwa moja wakae ndani ama wapotezwe mazima.

Kama sikosei baadhi yao walishatangulia.

Jk alipewa each n everthing kuhusu hawa watu, akaona ni sahihi wakae ndani.
 
Sio wanasheria ni maelekezo toka juu kwan? Hao wanasheria miaka yote walikua wap?
 
Hawa watu wako ndani toka 2014. Tuache kuishi uongo uongo

Wako ndani toka 2014.

Kipindi chote cha awamu ya mwendazake kaziba masikio na hakuona kuwa hawatendewi haki pamoja na makelele yote yaliyokuwapo?

Wangapi wengine zaidi mwendazake alihakikisha wanaendelea kuozea jela na kuishi kama mashetani?

Hiiiiii bagosha!
 
Wakikutwa hawana hatia watalipwa fidia ya kupotezewa muda kwa miaka waliyokaa ndani?
Kutolewa ndani ni fidia tosha! Wakileta zengwe warudishwe kula ugali wa serikali na kulima migomba na machungwa ya serikali huku wakifuga samaki
 
Bismillahir Rahmaanir Rahiim

SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

LEO TAREHE 23/04/2021, MAHAKAMA KUU AMEFUTA MASHTAKA 14 YA MASHEIKH.

Mawakili wanaowatetea Masheikh wamezoa ushindi mkubwa leo Mahakani katika mapingamizi waliyoweka dhidi ya upande wa Jamhuri.

Mapingamizi hayo yalikuwa dhidi ya ukiukwaji wa sheria ulio wawezesha upande wa Jamhuri kufungua kesi nzito (Criminal Session Na. 121/3020), dhidi ya Masheikh hao.

Katika shauri hilo la Jinai Mahakama imekubaliana na hoja zilizojengwa na Mawakili hao kutoka katika katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na pia Katiba ya Zanzibar na sheria nyingine ikiwemo sheria ya Kuzuia Ugaidi.

Kwa muktadha huo Mahakama Kuu imeyafuta mashitaka 14 kati ya mashitaka 25 yanayowakabili Masheikh hao.

Mashtaka 11 yaliyobaki yataanza kusikilizwa Mahakama Kuu Dar es Salaam jumanne tarehe 27.4.2021.

Wananch mnaombwa kuwa karibu na kesi hizi ambazo zina mafundisho na mambo mengi ya kuzingatiwa.

Ibrahim Z. Mkondo
Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania.
0713118812

Wewe ni Wakili, naona umechemka kweli kweli! Unatulazimisha kusikiliza kesi ya Masheikh tu? Why! Kesi ni kesi tu haijalishi wewe ni nani! Kuwekwa kwao ndani kuna sababu!
 
Jf inadhihirisha kuwa siku hizi ina wapuuzi wengi mno.

Upo sahihi mkuu, hao jamaa waliwekwa ndani na Rais Kikwete pamoja na Shein.

Na ieleweke kuwa hao jamaa mpaka wanakamatwa walikamatwa kabisa na vielement vyote vya Ugaidi.

Hata Maguful na Mwinyi mdogo hawakuweza kuwatetea, waliwaacha washikiliwe na dola.

- Inasemakana Jk na Shein pia kama sio kupata msaada kutoka nchi za Magharibi kuwatambua watu hao, basi ni order kutoka huko kuwa wawashikilie watu hao.

Mungu irehemu Tz, kama hili jambo limefanyika kisiass km lile la babu seya basi nalaani hili jambo.

Vyombo vya Usalama vingeachwa vifanye kazi yake.
Mnazunguka zunguka tu.

Masheikh wa UAMSHO wako ndani sababu ya MUUNGANO!

WALIUGUSA VIBAYA MUUNGANO!

Fuatilia video zao utaelewa.

Walikuwa wanawaamsha Wazanzibar kuachana na SIASA za u-CCM na u-CUF ambazo zilikuwa zinawagawa na kwamba adui wa kweli wa Taifa lao ni MUUNGANO!

Na Wazanzibari kwa wingi wao walianza kuwaelewa.
Yaani wasingewekwa ndani; pengine hivi tunavyoongea huu MUUNGANO, hata Kama ungekuwepo, usingekuwa hivi ulivyo!

Dini ilitumika Kama kiungo tu kwavile majority ya Wazenji ni Muslims. Ukiwakusanya Kama waislam inakuwa rahisi kuzungumza 'lugha' moja!
 
Dare to Struggle and dare to Win [emoji123][emoji106]
 
Acha wewe kuongea kiebrania kama unaona ni utumwa...mwenzako akiongea kiaraabu usiumie hayo ni maamuzi yake kwani hajavunja sheria yeyote.
Nikuulize Ndugu kweni Mungu ni Kabila gani?
 
Kwi hao mashehe wa uamsho wamejifunza mengi kwa kukaa rumande hata wakiachiwa huru leo hatutasikia tena watu wakipigwa risasi na kuuawa ovyo ovyo kama wakati ule walipoanzisha uamsho wao
Kwani wao walihusika? Je huo ushahidi Polisi haina wakatiwa hatiani na kuhukumiwa ?

Hanna kesi palé, ni kesi ya kisiasa tu .
 
Uko sahihi kabisa na umetoa hoja muhimu sana. Inauma sana kuwatesa watu pasipo kuwafungulia mashitaka ili wakipatikana na hatia wafungwe kwa mujibu wa sheria na kama hawana watolewe. Tusiwageuze mahabusu kuwa wafungwa. Ni kosa, ni dhambi na ni dhuluma kubwa!
Jf inadhihirisha kuwa siku hizi ina wapuuzi wengi mno.

Upo sahihi mkuu, hao jamaa waliwekwa ndani na Rais Kikwete pamoja na Shein.

Na ieleweke kuwa hao jamaa mpaka wanakamatwa walikamatwa kabisa na vielement vyote vya Ugaidi.

Hata Maguful na Mwinyi mdogo hawakuweza kuwatetea, waliwaacha washikiliwe na dola.

- Inasemakana Jk na Shein pia kama sio kupata msaada kutoka nchi za Magharibi kuwatambua watu hao, basi ni order kutoka huko kuwa wawashikilie watu hao.

Mungu irehemu Tz, kama hili jambo limefanyika kisiass km lile la babu seya basi nalaani hili jambo.

Vyombo vya Usalama vingeachwa vifanye kazi yake.
 
Lakini ingefaa zaidi washtakiwe rasmi na kufungwa kama wana hatia, kuliko kuwasotesha tu mahabusu pasipo kuhukumiwa

Back
Top Bottom