Mimi siwezi kuumizwa na dini hizi ambazo zina maswali yasiyojibika na yeyote.ukigoogle ni kwamba dunia Ina watu billion 7.Dini inayoongoza kwa kuwa na wafuasi wengi ni budha watu 1.7billion ya pili ni christian 1.3billion ya tatu ni Islam 1.1billion. Mi nimetaja hizo tatu ambazo zinaongoza kuwa na waumini wengi kuliko zote.Ila zimeororodheshwa nyingi. Utata mwingine kila dini ina Mungu wake, na misaafu ya hizo dini inatofautiana baina ya dini moja na nyingine. Na kila misaafu unadai Mungu wake ndiye muumba. Na baadhi ya maandishi ndani ya misaafu hiyo hayawatambui wafuasi wa dini nyingine kama waumini wa Mungu. Maswali ya kujiuliza ambayo hayana majibu ni: Kama yule anayeabudiwa na wabudha mwenye wafuasi wengi duniani1.7bil ndiye muumbaji iweje watu bil5.3 wamponyoke? Nadhani kila misaafu umemtaja kuwa ni muweza wa yote, huyo aliyempokonya hao 5.7bilion alipata wapi hayo manlaka na uwezo. Ni kiumbe wake kweli aliweza kupata hayo maarifa na kumnyang'anya hao 5.7bil? Lingine ina maana karuhusu viumbe alivyoviumba vijitangaze miungu na kumpora wafuasi makundi kwa makundi huku yeye akitazama tu? Najua maswali ya msingi kama haya hayana majibu. Kwa muhtasari huo mfupi, siwezi kukasirika hata kidogo kwa kauli yako kuwa, katika dunia hii yenye watu bilion7 mchangayiko dini tofauti,na hakuna dini hata 1 iliyoweza kucover hata theluth ya watu duniani ya kuwa "ili mtu asikilizwe na Mungu lazima atumie lugha ya kiarabu kumwomba." Na badala yake nimejikuta nafurahi na kucheka kwa jinsi walivyofanikiwa kutuaminisha hayo mambo.