Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Mahakama haikutengua hukumu bali imetengua uamuzi; soma vizuri; fatuma hakuwa kuhukumiwa popote. Alikuwa anakibiliana na maamuzi ya kamati ya mawakili, na maagizo ya jaji kiongozi.Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia muda huu kutoka Mahakamani .
Taarifa inaeleza kwamba Mahakama kuu imeona kwamba Fatuma Karume alihukumiwa bila kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya Kamati ya maadili ya Mawakili , hivyo imetengua hukumu yake na kuitaka Kamati hiyo kumaliza jambo hilo kwa haki
Ikumbukwe kwamba Mlalamikaji kwenye hili Sakata la Wakili Msomi Fatuma Karume lililojaa chuki , Wivu na uzandiki alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Je unadhani bado anafaa kukalia ofisi hiyo ?
View attachment 1825533
Mahakama imesema kuwa kamati iliyomvua uwakili haikuwa na mamlaka hayo, na ilikuwa inakiuka maagizo ya jaji kiongozi aliyekuwa ameshamsimamisha kwa muda Fatma Karume. Mahakama kuu imefuta uamuzi wa kamati hiyo ya mawakili, lakini maagazo ya jaji kiongozi bado yako pale pale. Fatma hawezi kuwa wakili mpaka akajitetee mahakamani kuhusu agizo hilo la Jaji kiongozi.