Kuna wakati huwa natafakari, sipati jibu kuhusu marehemu. Najiuliza:
1) Alikuwa ni mtu ambaye kwa asili yake alikuwa ni mtu tu wa roho mbaya?
2) Alikuwa ni mtu wa kawaida lakini baadaye shetani akaingia ndani yake, na hivyo alikuwa ni shetani katika umbile la mwanadamu?
3) Au alikuwa ni mtu wa kawaida, lakini alikuwa na tatizo la afya ya akili kiasi cha muda mwingine kuwa wa kawaida, na muda mwingine akili kukengeuka?
Maana kuna uovu mwingine aliowafanyia watu, unazidi hata ule wa watu katili.
Kwa kweli marehemu alikuwa katili na roho ya ajabu:
Kufilisi watu
Kuteka watu
Kuua watu
Kubambikia watu kesi
Kupora pesa za watu
Yaani alitaka usipomwabudu, basi ukose na fursa nyingine zote za maisha ya hapa Duniani.