Mahakama Kuu Zanzibar yaamuru Cryprian Musiba kumlipa Fatma Karume Tzs 7.5 bilioni

Mahakama Kuu Zanzibar yaamuru Cryprian Musiba kumlipa Fatma Karume Tzs 7.5 bilioni

Atazitoa wapi hizo pesa huyo kumbafu wakati pesa ya kulipa mishahara ya wafanyakazi wawili tu wa lile gazeti lake chafu kakosa...
 
Hukumu imetoka Zanzibar eeeh?

Hamna kesi hapo,wachache sana wataelewa ninachokisema.Wale waliojaa mihemko na kudhani kuwa hii nchi bado ipo kwenye msingi ya sheria ndio pekee watakai bisha.

Kuna maswala kama haya muda mwingine unajikuta unaona wazo la katiba mpya ni zuri sema tu utafutwaji wa hiyo katiba ndo changamoto, yes of course labda hiyo katiba ingesaidia kuondoa kile ninachokiaona kwenye hiyo kesi.

Aliyewahi kusoma kisa cha SAMAKI MTUNGONI, atakuwa anaelekea kuwa Watz wengi (wakiwemo wanajf na twitter) ni SAMAKI wakati wale wachache waliobakia ndiyo WAVUVI wenyewe.
 

1628685500480.png

ALIYEKUWA mwandishi Mwandamizi wa Televisheni ya Channel Ten, Cyprian Musiba (34), amechukuwa fomu ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa (NEC), na Mkutano Mkuu wa chama hicho ngazi ya taifa wilayani Bunda mkoani Mara.
Musiba ambaye amechukua fomu hizo juzi mchana na kuzirudisha jana asubuhi Makao Makuu ya Ofisi ya CCM Bunda, amesema dhamira yake ya kuomba nafasi hizo mbili ni kwenda kukijenga chama katika nyanja zote
za kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Alisema atapambana kwa nguvu zake zote kudhibiti rushwa, siasa za chuki, fitna na makundi ndani ya chama chake hicho tawala.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukuwa fomu hizo, Musiba alisema moja ya mambo yanayokichafua chama chake mbele ya umma wa Watanzania, ni vitendo vya rushwa, siasa chafu yakiwemo makundi na fitna.
Musiba alimuomba Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Dk. Edward Hoseah kuwapanga vema makamanda wake kwa ajili ya kuwakamata wagombea na watu watakaobainika kutoa rushwa ili wachaguliwe kwenye ngwe hiyo ya kuwania uongozi.
"Nimechukua fomu hii kwa lengo la kwenda kupigania maendeleo ya
chama changu tawala. Nitapambana kuhakikisha rushwa, siasa chafu ndani ya CCM vinaondoka, maana ndiyo vitu vinavyokiharibu kabisa chama.
"Kwa maana hiyo, kuanzia sasa naiomba TAKUKURU ianze kuwafuatilia na kuwakamata wagombea wote watakaoonekana kutoa rushwa
wakati huu wa uchaguzi," alisema Musiba.
Musiba ni miongoni mwa wanachama 13 waliochukuwa fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya U-NEC kupitia wilaya hiyo.
 
Ina jurisdiction Tz Bara? Kwanini hakufungua Bara?
Siyo lazima.Unaweza kufungua kesi mahara popote duniani.Kinachohitajika Ni vigezo na masharti kuzingatiwa. Fatuma angalia uwezokano wa kuuza whatever he has as fixed ili lijamaa lyende kuchunga ng'ombe kwao
 
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Wakili msomi, Fatma Karume aka Shangazi, ameandika hivi;

Hamjambo? Mnaomjua Cyprian Musiba mwambieni Mahakama Kuu ya Zanzibar, ndio pale VUGA, yametoa HUKUMU leo. Yamesema ni yeye na GAZETI lake wameandika UONGO dhidi yangu.
Sasa anatafute 7.5 billion za kunilipa!. Namshukuru sana Advocate Wangu!.


Billion 7.5 ilihali sponsor ameshakufa na kwa upande mwingine biashara zake zimemuendea kombo hadi kushindwa kuwalipa Wafanyakazi mbona atajua hajui!.

Watu wa karibu wa Musiba mnaweza kumpa hizi habari maana ni kitambo hatujamuona huko Twitter republican huyo aliyekuwa "Mwanaharakati huru" wa kumtetea hayati Magufuli.
Ama kweli kuna mambo huwa yana mwisho, namkumbuka Rashid wa KULI alisema kwa unyonge, “Yana Mwisho Haya”. Mwisho wa enzi wa Mwanaharakati Huru Bw Cyprian ‘Nyamanani sijui’ Musiba umekuwa mbaya mno! Hizo billion atazitoa wapi? Huku wafanyakazi wanamdai, huku Shangazi kapewa tuzo; watauza kila kitu na mwisho wa siku watamuuza Musiba mwenyewe!!!
 
Kwani Musiba Ni raia wa Nchi ya Zanzibar? Ninachojua ukitaka ku practice uwakili Zanzibar lazima usajiliwe upya kwao

Hiyo kesi wakaisajili mahakama ya kimataifa kunenforce sababu Zanzibar Ni nchi kamili kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar.

Musiba si raia wa Nchi ya Zanzibar na Hana mpango wa kuomba uraia Zanzibar
Wewe mpuuzi CCM mnasema nyinyi na hao Zanzibar ni nchi moja sasa huo upupu hapa wa nini??
 
Kwa kweli katika watu ambao waliguswa na kifo cha Sponsor huyu ndie aliyepaswa kujifinya ili ajue kama yuko hai.............. Musiba amefikwa na msiba
 
Pacha, Cyprian Musiba akishindwa kulipa hio hela yatapelekwa maombi mahakamani ya;

1) kukamata mali zote za Gazeti na za kwake binafsi ziuzwe ili alipwe Fatma Karume.

2) Kufungiwa account zake zote za bank.

Deni lisipowezekana kulipwa kabisa kutokana na mali kutofikia kiasi anacho daiwa, basi maombi ya kumfunga yanaweza kufanywa mahakamani (Civil Jail Term, sio Criminal Jail) na kama maombi yatakubaliwa na mahakama basi itapigwa hesabu ya deni na kifungo atakachotakiwa kufungwa kwa gharama za Fatma Karume (Yani Fatma Karume atakua akimhudumia lishe yake Cyprian Musiba kwa kipindi chote atakachofungwa).

In short, Cyprian Musiba safari hii anaweza akatolewa marinda.
[emoji23][emoji23][emoji23]hapo mwisho[emoji119][emoji119]

Sent from my TECNO P701 using JamiiForums mobile app
 
Kwani Musiba Ni raia wa Nchi ya Zanzibar? Ninachojua ukitaka ku practice uwakili Zanzibar lazima usajiliwe upya kwao

Hiyo kesi wakaisajili mahakama ya kimataifa kunenforce sababu Zanzibar Ni nchi kamili kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar.

Musiba si raia wa Nchi ya Zanzibar na Hana mpango wa kuomba uraia Zanzibar
Kwa hiyo Rais mama Samia aliomba uraia wa Tanganyika? Tunataka katiba mpya.
 
Hiyo kesi hatakiwi hata kuhangaika nayo Musiba atulie tu

Ni sawa tu na kuandikwa vibaya na gazeti la the Economist la Nchi ya marekani halafu unaenda mahakama ya kisutu kudai mumiliki akulipe fidia aliyeko Nchi ya Marekani wakati sio raia wa Nchi yako.Mahakama Local uwezo huo hawana .Ndio maana serikali iliishia tu kusema marufuku Hilo gazeti kukanyaga Nchi yetu

Hiyo kesi ya Musiba mahakama ya kuu ya Nchi huru ya Zanzibar kufuatana na katiba yao hawana ubavu huo.

Fatma Karume apeleke hiyo kesi mahakama ya kimataifa sio Vuga Zanzibar!!!
Zanzibar ni nchi mkuu?
 
Hiyo kesi hatakiwi hata kuhangaika nayo Musiba atulie tu

Ni sawa tu na kuandikwa vibaya na gazeti la the Economist la Nchi ya marekani halafu unaenda mahakama ya kisutu kudai mumiliki akulipe fidia aliyeko Nchi ya Marekani wakati sio raia wa Nchi yako.Mahakama Local uwezo huo hawana .Ndio maana serikali iliishia tu kusema marufuku Hilo gazeti kukanyaga Nchi yetu

Hiyo kesi ya Musiba mahakama ya kuu ya Nchi huru ya Zanzibar kufuatana na katiba yao hawana ubavu huo.

Fatma Karume apeleke hiyo kesi mahakama ya kimataifa sio Vuga Zanzibar!!!
Hichi kiburi kitawaponza
 
Back
Top Bottom