Mahakama Kuu Zanzibar yaamuru Cryprian Musiba kumlipa Fatma Karume Tzs 7.5 bilioni

Atazitoa wapi hizo pesa huyo kumbafu wakati pesa ya kulipa mishahara ya wafanyakazi wawili tu wa lile gazeti lake chafu kakosa...
 
Hukumu imetoka Zanzibar eeeh?

Hamna kesi hapo,wachache sana wataelewa ninachokisema.Wale waliojaa mihemko na kudhani kuwa hii nchi bado ipo kwenye msingi ya sheria ndio pekee watakai bisha.

Kuna maswala kama haya muda mwingine unajikuta unaona wazo la katiba mpya ni zuri sema tu utafutwaji wa hiyo katiba ndo changamoto, yes of course labda hiyo katiba ingesaidia kuondoa kile ninachokiaona kwenye hiyo kesi.

Aliyewahi kusoma kisa cha SAMAKI MTUNGONI, atakuwa anaelekea kuwa Watz wengi (wakiwemo wanajf na twitter) ni SAMAKI wakati wale wachache waliobakia ndiyo WAVUVI wenyewe.
 


ALIYEKUWA mwandishi Mwandamizi wa Televisheni ya Channel Ten, Cyprian Musiba (34), amechukuwa fomu ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa (NEC), na Mkutano Mkuu wa chama hicho ngazi ya taifa wilayani Bunda mkoani Mara.
Musiba ambaye amechukua fomu hizo juzi mchana na kuzirudisha jana asubuhi Makao Makuu ya Ofisi ya CCM Bunda, amesema dhamira yake ya kuomba nafasi hizo mbili ni kwenda kukijenga chama katika nyanja zote
za kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Alisema atapambana kwa nguvu zake zote kudhibiti rushwa, siasa za chuki, fitna na makundi ndani ya chama chake hicho tawala.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukuwa fomu hizo, Musiba alisema moja ya mambo yanayokichafua chama chake mbele ya umma wa Watanzania, ni vitendo vya rushwa, siasa chafu yakiwemo makundi na fitna.
Musiba alimuomba Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Dk. Edward Hoseah kuwapanga vema makamanda wake kwa ajili ya kuwakamata wagombea na watu watakaobainika kutoa rushwa ili wachaguliwe kwenye ngwe hiyo ya kuwania uongozi.
"Nimechukua fomu hii kwa lengo la kwenda kupigania maendeleo ya
chama changu tawala. Nitapambana kuhakikisha rushwa, siasa chafu ndani ya CCM vinaondoka, maana ndiyo vitu vinavyokiharibu kabisa chama.
"Kwa maana hiyo, kuanzia sasa naiomba TAKUKURU ianze kuwafuatilia na kuwakamata wagombea wote watakaoonekana kutoa rushwa
wakati huu wa uchaguzi," alisema Musiba.
Musiba ni miongoni mwa wanachama 13 waliochukuwa fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya U-NEC kupitia wilaya hiyo.
 
Ina jurisdiction Tz Bara? Kwanini hakufungua Bara?
Siyo lazima.Unaweza kufungua kesi mahara popote duniani.Kinachohitajika Ni vigezo na masharti kuzingatiwa. Fatuma angalia uwezokano wa kuuza whatever he has as fixed ili lijamaa lyende kuchunga ng'ombe kwao
 
Ama kweli kuna mambo huwa yana mwisho, namkumbuka Rashid wa KULI alisema kwa unyonge, “Yana Mwisho Haya”. Mwisho wa enzi wa Mwanaharakati Huru Bw Cyprian ‘Nyamanani sijui’ Musiba umekuwa mbaya mno! Hizo billion atazitoa wapi? Huku wafanyakazi wanamdai, huku Shangazi kapewa tuzo; watauza kila kitu na mwisho wa siku watamuuza Musiba mwenyewe!!!
 
Wewe mpuuzi CCM mnasema nyinyi na hao Zanzibar ni nchi moja sasa huo upupu hapa wa nini??
 
Kwa kweli katika watu ambao waliguswa na kifo cha Sponsor huyu ndie aliyepaswa kujifinya ili ajue kama yuko hai.............. Musiba amefikwa na msiba
 
[emoji23][emoji23][emoji23]hapo mwisho[emoji119][emoji119]

Sent from my TECNO P701 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo Rais mama Samia aliomba uraia wa Tanganyika? Tunataka katiba mpya.
 
Zanzibar ni nchi mkuu?
 
Hichi kiburi kitawaponza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…