Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kama wengi mnavyofahamu, Tanzania imekuwa ikishtakiwa na makampuni ya madini kwenye mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara, ICSID kwa kosa la kufuta leseni za makampuni ya kigeni yaliyokuwa yameingia nchini kwa kufuata sheria zote, kisha yakafanya utafiti, na baadaye kupewa Retention Licenses, halafu kwa ubabe, Serikali ikazifuta leseni hizo.
Kampuni zilizokuwa zimefanyiwa uhuni huo ni takribani 6, mpaka sasa kampuni 3 zimefikisha malalamiko yake kwenye mahakama ya ICSID. Shauri la kwanza lilikuwa ni la kampuni ya Indiana, limekwisha, kama ilivyotegemewa, Tanzania tumeshindwa, na tumeamriwa kuilipa fidia kampuni ya Indiana ya Australia AUD 127m (zaidi ya shilingi bilioni 210). Montero ya Canada inadai fidia ya CAD 90m (zaidi ya shilingi bilioni 170), na Winshear ya Canada inataka fidia ya CAD 124m (zaidi ya shilingi bilioni 230).
Kesi ya pili inaendelea sasa, ikiwa kwenye hatua ya mwisho, na hakuna dalili yoyote ya Tanzania kushinda. Kesi ya 3, kati ya Montero v. Tanzania nayo inaendelea.
Kesi ya pili ni:
Winshear Gold Corp. V. United Republic of Tanzania (ICSID Case No. ARB/20/25).
Kesi hii ipo chini ya Rais Gabrielle Kaufmann Hohrer kutoka Uswizi.
Mashahidi wetu huko ni Prof. Mruma na Mwanasheria wa Serikali bwana Igenge.
Nimesikiliza mahojiano kati ya Wakili wa Winshear bwana Fordin na Prof. Mruma na mwanasheria Igenge, kwa kweli ni aibu tupu. Mapungufu yapo kuanzia kuonekana mtu unasema uwongo, kushindwa kuelewa maswali yanayoulizwa, kutoa majibu ya kujichanganya, kushindwa kuelewa hata sheria zetu, mpaka kushindwa kuongea Kiingereza vizuri. Igenge muda mwingine akabakia kusema tu yes, lakini akimaanisha no. Ni aibu tupu.
Nadhani hawa mashahidi walichokuwa wanaangalia zaidi ni kupata tu posho zao lakini siyo kufanya chochote cha maana. Fikiria mtu kama Igenge, eti ni mwanasheria, halafu hazielewi hata sheria zetu. Yaani mawakili wa Winshear ambao siyo Watanzania, inaonekana wanazijua vizuri zaidi sheria zetu kuliko wanasheria wetu.
USHAURI KWA SERIKALI:
Kama hatuna mashahidi kwa sababu utetezi wa kimaandishi tulioutoa ni wa uwongo, au tunaona hatuna utetezi, si afadhali tuwaite hao wanatushtaki, tukubaliane kuwalipa hiyo fidia wanayotudai kuliko kuendelea kuongeza hasara kwa kuwalipa watu kwenda huko Marekani wakati tunajua hawana msaada wowote, na wala hawawezi kubadilisha chochote?
Yaani tuwalipe hawa walioenda kutalii Marekani, halafu tuwalipe tena wanaotudai, hasara mara mbili, na wala hatujifunzi chochote.
Viongozi wa Serikali ni watu wa ajabu ajabu sana. Ni watu wanaopenda kutumia zaidi nguvu kuliko akili. Hawawezi hata kuelewa kwa nini tembo pamoja na ukubwa wote, na nguvu zote, lakini anaishi mwituni, na mwanadamu ana uwezo wa kumwua wakati wowote. Binadamu asiyetumia akili lakini anajivunia mabavu, hana utofauti na mnyama. Anaweza kufanywa chochote na wanaotumia akili. Usiyetumia akili, wakati ukifika utanyolewa na wanaotumia akili.
Nchi hii ni masikini sana katika kutumia akili, ndiyo maana kidogo tunachokipata kinachukuliwa na wenye akili. Sasa zile tozo za kwenye miamala ya akina mama nitilie zinaenda kuwalipa matajiri wa Indiana Resources, Winshear Corp na wengineo wanaotushtaki.
Kama una muda na bando la kutosha sikiliza mashahidi wetu Prof. Mruma na Igenge wanavyonyolewa bila maji na mawakili wazungu.