Mnakumbuka Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya kwenye mkutano wa kampeni ya kuwaomba ridhaa Watanzania ya kuwaongoza katika awamu ya tano.
Dkt Magufuli aliwaeleza wananchi kuwa iwapo watampa ridhaa ya kuiongoza Tanzania,atahakikisha anaanzisha mahakama maalumu ya Mafisadi na Wala rushwa.
Baada ya kuingia ikulu ikaanzishwa mahakama ya mafisadi sambamba ya sheria yake.
Rais mwenyewe amekuwa akilia kwamba awamu ya nne ilijaa mafisadi chungu mzima. Wakati wa kampeni tukaambiwa mafisadi wamekimbilia UKAWA. Tukaambiwa CCM mpya.
Sasa ni miaka hakuna kinachoendelea zaidi ya kesi za tudagaa. Huku wanaotajwa kuwa mafundi wa ufisadi wakiendelea kula mema ya nchi.
Hivi kuna hata FUNDI mmoja wa ufasadi ametolewa kama mfano? Huu ndio wakati sasa wa kufanya remix ya song la mafisadi na sio kuwapiga madodoki mafisadi