Mahakama yaamuru Eng. Hersi aachie ngazi Yanga!

Potelea mbali. Guede aende tu. Maana hakuna namna nyingine. Na huyo Magoma hana uwezo wa kushindana na wananchi wote. Ni suala tu la muda kabla ya kumshughulikia ipasavyo. 😑
Hapo swala ni Magoma au katiba? Unamuonea bure mzee Magoma yeye anataka katiba ifatwe hata wananchi wote mnamkubali hersi. Vinginevyo malizeni transformation
 
Hapo swala ni Magoma au katiba? Unamuonea bure mzee Magoma yeye anataka katiba ifatwe hata wananchi wote mnamkubali hersi. Vinginevyo malizeni transformation
Simba ilimaliza transformation? Mbona Mo alisema kainunua Simba na wala hatujaona mahakama ikilishupalia? Serikali ilishasema kuwa lazima kuwe na wawekezaji wasiopungua watatu je kuna namna imetokea kwa Mo kuvuliwa kitengo Simba? Katiba ya Simba haikupitishwa na Mo anaendesha Simba kama kawaida kama mwekezaji. Hapa kilichopo ni siasa ya kuifanya Yanga ipoteane baada ya kuona mambo magumu ndani ya uwanja.
 
Yaani unachojaribu kufanya hapo ni kulikimbia tatizo nyumbani kwako na kushupalia matatizo ya jirani. Hapa hoja ni zee magoma na sakata la hersi kuipora utopolo nje ya katiba ya utopolo. Ya simba waachioe simba, zimeni moto wa nyumbani kwenu kwanza.
 
Wakitokea watu wa kushtaki Mahakama itafuata sheria,Mahakama haiwezi kuendesha kesi isiyo na msingi kutoka kwa walalamikaji
 
MAULID KITENGE ALIVYOMUHOJI MZEE MAGOMA

Kwa Mujibu wa Mzee Magoma amesema ameamua kuwa mstari wa Mbele kutafuta Haki ya Klabu ya Yanga Kwa sababu anaona inaendeshwa kishkaji na Wanachama wengi wapo kimya hawalioni Hilo Kwa Sasa

Follow ukurasa wetu wa Instagram kuisoma zaidi hukumu hiyo ya mahakama πŸ‘‡

.
@followers
#followers
#followers
#yangasc
#Wazee
#mzeemagoma
#HABARI
#Halisimediatz
#genzmemes
 
Hukumu hii haiwezi kuwa ni "final & binding" pasipo uwepo na nafsi ya kukata rufaa.
 
Yanaanzaga hivi hivi hizi timu mbili zina siasa sanaaaaa , ngoja uone hapo linatengenezwa zengwe timu isitawalike wakati wa Yanga kuhenya unakaribia ,
Hapo simba nae atatambaaa weeee wakati ukifika zengwe tena hahahaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…