Mahakama yaamuru Eng. Hersi aachie ngazi Yanga!

Mahakama yaamuru Eng. Hersi aachie ngazi Yanga!

Serikali ishajua kivuli chake ni simba na Yanga, ndo mambo yanayowapumbaza wananchi wake, baada ya Simba kutawala soka miaka minne ikaja zamu ya yanga, kwa mwendo wa eng hersi wanaona kabisa huyu anaweza kutawala soka hata miaka 10, makolo wapate depression waingie mtaani kama gen Z wa kenya, Bora wamtoe makolo wapate hata ahueni kidogo, and the circle goes on
Kwahiyo Hersi anasepa kweli?🥹
 
Mahakama na Mpira? Tusije tukafungiwa.

Lakini pia kila siku tunachangia hapa kufuata sheria na naunga mkono sheria zifuatwe.

Ila sema hao wazee ni kama wanga vile , wananchi tumeshazoea furaha wao togwa wanatia nzi.
Mkuu RITA waliitwa wakatoa ushahidi wao wanatambua katiba ya 2010 sio 2020 😂😂😂 kama hata RITA hawatambui sawa 😂😂
 
Taarifa toka saa 8 ziko mtaani jamaa wamejaribu sana kuizima ila Mwamba EDO KUMWEMBE akajibika mabomu wengine wakafuata includeing Millard Ayo na wengine
Mbona unaifurahia sana hii taarifa yote hii ni furaha ya Eng Hersi aondoke na wasaidizi ake ili simba mpate nafasi ? Au kuna kingine.?
 
Serikali ishajua kivuli chake ni simba na Yanga, ndo mambo yanayowapumbaza wananchi wake, baada ya Simba kutawala soka miaka minne ikaja zamu ya yanga, kwa mwendo wa eng hersi wanaona kabisa huyu anaweza kutawala soka hata miaka 10, makolo wapate depression waingie mtaani kama gen Z wa kenya, Bora wamtoe makolo wapate hata ahueni kidogo, and the circle goes on
Umeandika ujinga
 
changaml5
View attachment 3044226

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, imeamuru Uongozi wa Club ya Yanga ukiongozwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Saidi na wenzake, kuachia ngazi na kuondoka kwenye Club hiyo kwakuwa Katiba ya Yanga haitambui uwepo wao.

Imedaiwa kuwa uamuzi huu wa Mahakama umekuja baada ya Kundi la Wazee wachache waliowahi kuwa Wazee wa Yanga kipindi cha nyuma, kushitaki Mahakamani likidai uwepo wa Viongozi wa sasa wa Yanga (Injinia Hersi na wenzake) ni batili na haujafuata Katiba ya Club hiyo.

Kutokana na Wazee hao kushinda kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inamaana kuwa Rais wa Yanga Injinia Hersi na Viongozi wenzake wanatakiwa kuachia ngazi na kukabidhi Ofisi kuanzia sasa.

Injinia Hersi alianza kuiongoza Yanga kama Rais miaka miwili iliyopita baada ya kushinda nafasi hiyo akiwa ni Mgombea pekee July 2022 na kumfanya kuwa Rais wa kwanza wa Yanga SC toka kuanza kwa mfumo mpya wa mabadiliko ambapo alitangazwa kuwa atakuwa madarakani kwa miaka minne ( hadi 2026 ) kwa mujibu wa Katiba ya Club hiyo.

Source: #MillardAyoUPDATES
PIA SOMA
- Yanga: Mkutano na wanahabari tar 17.07.204

====

Source nyingine:
Wanachama wawili wa Yanga SC JUMA MAGOMA na GEOFREY MWAIPOPO walishinda kesi waliyofungua katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar mwaka jana mwezi Agosti. Kesi yao ilikuwa dhidi ya Baraza la wadhamini la klabu hiyo kuikabidhi klabu kwa mtu wasiyemjua wala asiyekuwa Mwanachama wakati kesi inafunguliwa mwezi Mei mwaka 2022 siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa klabu uliomuweka madarakani Rais wa Yanga Eng Hersi Said. Awali walifungua kesi hiyo Mahakama ya Wilaya ya Ilala iliyopo Kinyerezi jijini Dar, kabla ya kushauriwa kuihamishia katika Mahakama ya Kisutu.

Walipinga kutumika kwa katiba ya mwaka 2020 ambayo ilitumika kwenye uchaguzi Mkuu uliouweka uongozi uliopo madarakani wakisema katiba hiyo sio halali. Inasemekana RITA waliitwa kutoa ushahidi na wakasema wanaifahamu katiba ya mwaka 2011 ambayo ipo ofisini kwao na hiyo ya mwaka 2020 hawaitambui.

Baada ya kupata hukumu yao mwezi Agosti mwaka 2023 JUMA MAGOMA NA GEOFREY MWAIPOPO wameona hakuna utekelezaji wa hukumu hiyo hata baada ya kuwasilisha kwa wahusika wakaamua kufungua kesi ya kukazia hukumu ambapo itatolewa maamuzi mwezi Agosti tarehe 5 mwaka 2024, ili hukumu hiyo ianze kufanya kazi. Ambapo inategemewa Mkutano Mkuu wa Yanga kuitwa ambao utajumuisha WANACHAMA WOTE HAI sio wawakilishi wa matawi pekee (kama ilivyo sasa) na kwenda kwenye uchaguzi mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa klabu kwa kufuata katiba ya mwaka 2011.

Kama hili litatokea manake Eng Hersi na timu yake watakuwa wameondoshwa madarakani kwakuwa watakuwa wameingia isivyo halali.
 
Rufaa itakatwa tu hatoko mtu hao ni. Wahuni hizi ni propaganda tu mahakama hairuhusiwi kuingilia mpira kwanza
Kama mahakama hairuhusiwi kuingilia mpira , Hao mawakilI wa "Yanga haramu" walitakiwa waweke pingamizi la awali kuwa mahakama haina mamlaka, kama imesikiliza means ina mamlaka.

Kwa akili zako za kuiba mitihani, unataka kusema hakuna kesi zinazohusu timu zilizopo mahakamani.?
 
Back
Top Bottom