Simba imeona imeshindwa katika uwanja kuing'oa Yanga sasa wameamua kutumia wazee wahuni wanaojiita wana yanga kuudhofisha uongozi bora wa timu ya Yanga.
Wazee walipeleka shauri lao mahakamani la kupinga uwepo wa viongozi pale Yanga yaani injinia na wenzake huku wakidai eti hawatambui uwepo wala upatikanaji wao katika timu.
Swali ni je? Wakiachia ngazi wametuandalia viongozi watakaoweza kufanya kazi kama waliyokuwa wanaifanya akina Herisi?
Je timu ikifeli wataturuhusu tuwapige mawe hadi wafe?
Hapa busara inahitajika sema sijui sheria za FIFA kama zinaruhusu dola kuingilia michezo