Mahakama yaamuru mwili wa aliyefia Polisi ufukuliwe, uchunguzwe

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Uamuzi umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga, baada ya kukubaliana na maombi ya familia ya Marehemu Stella Moses aliyefia katika kituo Cha Polisi Mburahati Desemba 20, 2020.

Hakimu Kiswaga ametoa Amri hiyo kwa maelezo kuwa Polisi hawakutekeleza Wajibu wao Kisheria ikiwemo kuweka wazi taarifa za uchunguzi ili kuonesha Chanzo cha Kifo na hawakuwasilisha taarifa hizo Mahakamani.

Katika majibu yao Polisi walidai Marehemu alijinyonga, maelezo ambayo yalipingwa na wanafamilia hukui Jeshi la Polisi likionesha kutofuata matakwa hayo na badala yake lilishinikiza mwili wa Marehemu uzikwe.

=================

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni (Kinondoni) Dar es Salaam imeamuru kufanyika kwa uchunguzi wa chanzo cha kifo cha Stella Moses aliyefia mahabusu katika kituo Cha Polisi Mburahati mwaka 2020,

Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 19, 202 na Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga, baada ya kukubaliana na maombi ya wanafamilia katika shauri la maombi walilolifungua mahakamani hapo.

Stella alifariki dunia usiku wa Desemba 20, 2020, akiwa mahabusu kituoni hapo alikojisalimisha baada ya kupata taarifa kuwa alikuwa anahitajika, tukio ambao lilizua mvutano mkubwa baina ya Polisi na ndugu wa marehemu kwa kile walichodai kuwa ni mazingira tata ya kifo hicho.

Polisi walidai kuwa alijinyonga, maelezo ambayo wanafamilia hawakukubaliana nayo badala yake wakaomba ufanyike uchunguzi huru kujiridhisha na chanzo cha kifo chake, lakini Jeshi la Polisi halikuwa tayari na badala yake lilishinikiza mwili wa marehemu uzikwe.

Hivyo mapema mwaka huu ndugu wa marehemu walifungua shauri la maombi dhidi ya viongozi wa Jeshi la Polisi na uongozi wa hospitali ya Muhimbili kwa kutokutimiza wajibu wao.

Shauri hilo lilifunguliwa na shemeji wa marehemu, Emmanuel Ernest Kagongo, kwa niaba ya familia ya marehemu dhidi ya dhidi ya Jeshi la Polisi akiwakilishwa na wakili Peter Madeleka.

Katika hati ya maombi hayo ya jinai mchanganyiko namba 3 ya mwaka 2022, aliomba mahakama hiyo iridhie kufanya uchunguzi huru ili kujua ukweli wa mazingira ya kifo cha ndugu yao.

Wajibu maombi katika shauri hilo ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (Inspekta Jenerali wa Polisi – IGP), Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam (ZPC) na Kamanda wa Polis Mkoa wa Kipolisi Kinondoni (RPC).

Wengine ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Mburahati (OCD), Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akitoa uamuzi wake baada ya kusikiliza hoja za upande mmoja wa mwombaji kutokana na wajibu maombi kushindwa kuwasilisha hoja zao za maandishi, Hakimu Kiswaga amesema kuwa anakubaliana na maombi hayo.

Hakimu Kiswaga amesema kwamba kutokana na hoja za mwombaji na viapo kinzani vya wajibu maombi watu waliowasilisha viapo kinzani kati ya sita hakuna ubishi kuwa Stella alifariki dunia katika mazingira tata akiwa katika kituo Cha Polisi Mburahati.

Amesema kuwa kwa kuwa wajibu maombi hususan Polisi hawakutekeleza wajibu wao wa kisheria yaani kutoa taarifa na hakuna taarifa zozote za uchunguzi uliofanyika kuonesha chanzo cha kifo hicho, zilizowasilishwa mahakamani basi mahakama hiyo ina jukumu la kuamuru ufanyike uchunguzi huo.

"Hivyo mahakama hii inaamuru ufanyike uchunguzi wa kifo cha Stella Moses ambaye mahakama hii inaona kwamba alifariki unnatural death (kifo kisicho cha kawaida) akiwa chini ya Jeshi la Polisi Mburahati, Desemba 20, 2020," amesema Hakimu Kiswaga na kuongeza:

"Taarifa (ya uchunguzi) itolewe mahakamani na ipelekwe kwenye vyombo husika ili aliyehusika na kifo hicho achukuliwe hatua za kisheria."

MWANANCHI
 
Ila hatuna utaalamu wa kujua chanzo cha kifo baada ya miaka miwili
 
Askali ni wauaji inafahamika

sasa kifo cha kujinyonga kitapimwaje baada ya miaka 2 kaburini wakati steki zote zimemomonyoka...

"Hapo walimpiga virungu hadi kupoteza maisha"
Inasikitisha sana!!!

Na imesemwa marehemu alijipeleka kituoni mwenyewe,hawa jamaa ni katili sana.
 
Alijipeleka mwenyewe na halafu eti akajinyonga!!--- huo muda na hizo nyenzo za kujinyongea alizipata wapi huko mahabusu??!!, huko mahabusu alikuwa peke yake??!!, kama alikuwa na nia ya kujinyonga kwanini kwanza asijinyonge badala ya kwenda huko polisi??!!

Hapo Kuna maswali kibao ya kujiuliza.
 
Uamuzi umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga, baada ya kukubaliana na maombi ya familia ya Marehemu Stella Moses aliyefia katika kituo Cha Polisi Mburahati Desemba 20, 2020.

Hakimu Kiswaga ametoa Amri hiyo kwa maelezo kuwa Polisi hawakutekeleza Wajibu wao Kisheria ikiwemo kuweka wazi taarifa za uchunguzi ili kuonesha Chanzo cha Kifo na hawakuwasilisha taarifa hizo Mahakamani.

Katika majibu yao Polisi walidai Marehemu alijinyonga, maelezo ambayo yalipingwa na wanafamilia hukui Jeshi la Polisi likionesha kutofuata matakwa hayo na badala yake lilishinikiza mwili wa Marehemu uzikwe.

=================

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni (Kinondoni) Dar es Salaam imeamuru kufanyika kwa uchunguzi wa chanzo cha kifo cha Stella Moses aliyefia mahabusu katika kituo Cha Polisi Mburahati mwaka 2020,

Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 19, 202 na Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga, baada ya kukubaliana na maombi ya wanafamilia katika shauri la maombi walilolifungua mahakamani hapo.

Stella alifariki dunia usiku wa Desemba 20, 2020, akiwa mahabusu kituoni hapo alikojisalimisha baada ya kupata taarifa kuwa alikuwa anahitajika, tukio ambao lilizua mvutano mkubwa baina ya Polisi na ndugu wa marehemu kwa kile walichodai kuwa ni mazingira tata ya kifo hicho.

Polisi walidai kuwa alijinyonga, maelezo ambayo wanafamilia hawakukubaliana nayo badala yake wakaomba ufanyike uchunguzi huru kujiridhisha na chanzo cha kifo chake, lakini Jeshi la Polisi halikuwa tayari na badala yake lilishinikiza mwili wa marehemu uzikwe.

Hivyo mapema mwaka huu ndugu wa marehemu walifungua shauri la maombi dhidi ya viongozi wa Jeshi la Polisi na uongozi wa hospitali ya Muhimbili kwa kutokutimiza wajibu wao.

Shauri hilo lilifunguliwa na shemeji wa marehemu, Emmanuel Ernest Kagongo, kwa niaba ya familia ya marehemu dhidi ya dhidi ya Jeshi la Polisi akiwakilishwa na wakili Peter Madeleka.

Katika hati ya maombi hayo ya jinai mchanganyiko namba 3 ya mwaka 2022, aliomba mahakama hiyo iridhie kufanya uchunguzi huru ili kujua ukweli wa mazingira ya kifo cha ndugu yao.

Wajibu maombi katika shauri hilo ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (Inspekta Jenerali wa Polisi – IGP), Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam (ZPC) na Kamanda wa Polis Mkoa wa Kipolisi Kinondoni (RPC).

Wengine ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Mburahati (OCD), Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akitoa uamuzi wake baada ya kusikiliza hoja za upande mmoja wa mwombaji kutokana na wajibu maombi kushindwa kuwasilisha hoja zao za maandishi, Hakimu Kiswaga amesema kuwa anakubaliana na maombi hayo.

Hakimu Kiswaga amesema kwamba kutokana na hoja za mwombaji na viapo kinzani vya wajibu maombi watu waliowasilisha viapo kinzani kati ya sita hakuna ubishi kuwa Stella alifariki dunia katika mazingira tata akiwa katika kituo Cha Polisi Mburahati.

Amesema kuwa kwa kuwa wajibu maombi hususan Polisi hawakutekeleza wajibu wao wa kisheria yaani kutoa taarifa na hakuna taarifa zozote za uchunguzi uliofanyika kuonesha chanzo cha kifo hicho, zilizowasilishwa mahakamani basi mahakama hiyo ina jukumu la kuamuru ufanyike uchunguzi huo.

"Hivyo mahakama hii inaamuru ufanyike uchunguzi wa kifo cha Stella Moses ambaye mahakama hii inaona kwamba alifariki unnatural death (kifo kisicho cha kawaida) akiwa chini ya Jeshi la Polisi Mburahati, Desemba 20, 2020," amesema Hakimu Kiswaga na kuongeza:

"Taarifa (ya uchunguzi) itolewe mahakamani na ipelekwe kwenye vyombo husika ili aliyehusika na kifo hicho achukuliwe hatua za kisheria."

MWANANCHI
Kwa wazee wakuchanganya akili hapa tayr kuna walakin
Mtu aloko mahabusu anajinyongaje au walimpa kamba/kanga
Hii inauma sana asee pale chombo cha haki kinaposhindwa kutenda haki kwa ufasaha n Uwazi
 
Mda mrefu umepita; mifupa haiwezi kutoa majibu sahihi; kwa kifupi tu ni kuwaridhisha ndugu pamoja na kufunga mjadala.
 
Actually this depends on the the type of soil in which the person was buried.
Kwa wakristo (marehemu Stella), soil has got nothing to do with body decomposition.

Maana wanazikwa ndani ya jeneza la mbao.

Angekua Muislamu sawa.
 
Back
Top Bottom