Mahakama yaamuru mwili wa aliyefia Polisi ufukuliwe, uchunguzwe

Mahakama yaamuru mwili wa aliyefia Polisi ufukuliwe, uchunguzwe

Kwahiyo hata mimi hapa tumboni ninao bacteria 🦠 ambao nikifa wataanza kunishambulia?


Kila kiumbe hai kinao Bacteria, hata katika hewa, maji, udongoni nk, kote humo wamejaa bacteria, kwenye matumbo ( intestines) kumejaa bacteria kibao, kwanini mtu ukiwa hai bactetia wanakuwa hawana madhara??!--- Kwasababu mwili unayokinga dhidi ya hao bacteria na tunapokufa kinga nayo inakufa hapo ndipo bacteria huanza kuula (decomposition) mwili hasa kuanzia ndani ya matumbo (intestines) kuja nje, kutokea nje kwenda ndani sio sana kwani bactetia wa nje mara nyingi sio wengi kama wale waliomo ndani.

Ukinunua samaki mbichi na ukitaka kumsafirisha kwa masaa kama 8 na zaidi ili asiharibike haraka mtoe matumbo yote kisha mpakaze chumvi na umning'inize ili apate hewa, kumtumbua maana yake ni kuondoa wale bacteria wa tumboni ambao ndio very active kuozesha samaki akiwa mbichi.
 
hio ni kiini macho tu hakuna kitu Ndugu wa marehemu wataambulia watapigishwa zogo mpaka basi maana Polisi na Mahakama ni kitu kimoja hakuna lolote hapo.

unakuta kuna watu wanaamini Mahakamani kuna haki ila ukweli ni kwamba hakuna haki wala nini
 
Kila kiumbe hai kinao Bacteria, hata katika hewa, maji, udongoni nk, kote humo wamejaa bacteria, kwenye matumbo ( intestines) kumejaa bacteria kibao, kwanini mtu ukiwa hai bactetia wanakuwa hawana madhara??!--- Kwasababu mwili unayokinga dhidi ya hao bacteria na tunapokufa kinga nayo inakufa hapo ndipo bacteria huanza kuula (decomposition) mwili hasa kuanzia ndani ya matumbo (intestines) kuja nje, kutokea nje kwenda ndani sio sana kwani bactetia wa nje mara nyingi sio wengi kama wale waliomo ndani.

Ukinunua samaki mbichi na ukitaka kumsafirisha kwa masaa kama 8 na zaidi ili asiharibike haraka mtoe matumbo yote kisha mpakaze chumvi na umning'inize ili apate hewa, kumtumbua maana yake ni kuondoa wale bacteria wa tumboni ambao ndio very active kuozesha samaki akiwa mbichi.
Mungu fundi sana Mwaisa…
 
Sikiliza wewe....

Kwa wakristo, Huwa wananazikwa ndani ya jeneza la mbao.

Rate of decomposition ni very slow.

Nyama zinaanza kugeuka udongo labda kuanzia miaka mitano huko.

We unadhani mpaka zile mbao zioze ni leo.
Hata nyama haziwagi udongo huwa zinasinyaa,kama ulivosema mtu akizikwa kwenye jeneza decomposition inachelewa, mara ya mwisho nilifuatilia YouTube wazungu walishafanya hadi research hii hata hiyo miaka 5 bado mtu anakuwa na nyama
 
Kama ni fuvu au mifupa imegongwa hadi kupinda itaonekana. Issue sio nyama. Ndio maana mammoth wanaweza kujulikana maisha yao
Yah,kuna maiti ya mtu aliishi miaka zaidi 1500 iliyopita,walipompata huko kwenye milima walichunguza hadi chakula alichokula mara ya mwisho

Mwingine aliishi zama za Yesu walipata maiti yake jangwani hapo Egypt na kufanya utafiti waligundua kifo chake kilitokana na kupigwa kichwani na mtu aliyetokea nyuma
 
watakuta nin zaid ya mifupa tu miaka miwil imepita!

ingekuwa mie ningeroga kituo kizima kila wakiamka wanajikuta wapo selo humohumo kituon!

wakilala wanakuwa wanaota wanasikomezwa dushe na kukuta pameloa wakiamka!
Mwili bado upo vizuri tu ila sasa wataalam wa hayo mambo kama wapo hap kwetu
 
Dah
Iliniuma. Mtu unaemfahamu kapatwa na vitu kama hivi. Imebaki kumbukumbu kichwani kuwa alikuwepo.
 
watakuta nin zaid ya mifupa tu miaka miwil imepita!

ingekuwa mie ningeroga kituo kizima kila wakiamka wanajikuta wapo selo humohumo kituon!

wakilala wanakuwa wanaota wanasikomezwa dushe na kukuta pameloa wakiamka!
Kama mwili ulifanyiwa Ile treatment kabla ya mazishi wataukuta ukiwa intact.
 
nimeandika nimefuta nimeandika nimefuta tena ila nimekaa kile kituo cha mburahati kwa siku sita kama mahabusu

kujinyonga...????
mwanamke...????
umbali kutoka ktk vile vidirisha mpaka ktk sakafu doesn't make sense
 
Uamuzi umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga, baada ya kukubaliana na maombi ya familia ya Marehemu Stella Moses aliyefia katika kituo Cha Polisi Mburahati Desemba 20, 2020.

Hakimu Kiswaga ametoa Amri hiyo kwa maelezo kuwa Polisi hawakutekeleza Wajibu wao Kisheria ikiwemo kuweka wazi taarifa za uchunguzi ili kuonesha Chanzo cha Kifo na hawakuwasilisha taarifa hizo Mahakamani.

Katika majibu yao Polisi walidai Marehemu alijinyonga, maelezo ambayo yalipingwa na wanafamilia hukui Jeshi la Polisi likionesha kutofuata matakwa hayo na badala yake lilishinikiza mwili wa Marehemu uzikwe.

=================

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni (Kinondoni) Dar es Salaam imeamuru kufanyika kwa uchunguzi wa chanzo cha kifo cha Stella Moses aliyefia mahabusu katika kituo Cha Polisi Mburahati mwaka 2020,

Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 19, 202 na Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga, baada ya kukubaliana na maombi ya wanafamilia katika shauri la maombi walilolifungua mahakamani hapo.

Stella alifariki dunia usiku wa Desemba 20, 2020, akiwa mahabusu kituoni hapo alikojisalimisha baada ya kupata taarifa kuwa alikuwa anahitajika, tukio ambao lilizua mvutano mkubwa baina ya Polisi na ndugu wa marehemu kwa kile walichodai kuwa ni mazingira tata ya kifo hicho.

Polisi walidai kuwa alijinyonga, maelezo ambayo wanafamilia hawakukubaliana nayo badala yake wakaomba ufanyike uchunguzi huru kujiridhisha na chanzo cha kifo chake, lakini Jeshi la Polisi halikuwa tayari na badala yake lilishinikiza mwili wa marehemu uzikwe.

Hivyo mapema mwaka huu ndugu wa marehemu walifungua shauri la maombi dhidi ya viongozi wa Jeshi la Polisi na uongozi wa hospitali ya Muhimbili kwa kutokutimiza wajibu wao.

Shauri hilo lilifunguliwa na shemeji wa marehemu, Emmanuel Ernest Kagongo, kwa niaba ya familia ya marehemu dhidi ya dhidi ya Jeshi la Polisi akiwakilishwa na wakili Peter Madeleka.

Katika hati ya maombi hayo ya jinai mchanganyiko namba 3 ya mwaka 2022, aliomba mahakama hiyo iridhie kufanya uchunguzi huru ili kujua ukweli wa mazingira ya kifo cha ndugu yao.

Wajibu maombi katika shauri hilo ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (Inspekta Jenerali wa Polisi – IGP), Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam (ZPC) na Kamanda wa Polis Mkoa wa Kipolisi Kinondoni (RPC).

Wengine ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Mburahati (OCD), Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akitoa uamuzi wake baada ya kusikiliza hoja za upande mmoja wa mwombaji kutokana na wajibu maombi kushindwa kuwasilisha hoja zao za maandishi, Hakimu Kiswaga amesema kuwa anakubaliana na maombi hayo.

Hakimu Kiswaga amesema kwamba kutokana na hoja za mwombaji na viapo kinzani vya wajibu maombi watu waliowasilisha viapo kinzani kati ya sita hakuna ubishi kuwa Stella alifariki dunia katika mazingira tata akiwa katika kituo Cha Polisi Mburahati.

Amesema kuwa kwa kuwa wajibu maombi hususan Polisi hawakutekeleza wajibu wao wa kisheria yaani kutoa taarifa na hakuna taarifa zozote za uchunguzi uliofanyika kuonesha chanzo cha kifo hicho, zilizowasilishwa mahakamani basi mahakama hiyo ina jukumu la kuamuru ufanyike uchunguzi huo.

"Hivyo mahakama hii inaamuru ufanyike uchunguzi wa kifo cha Stella Moses ambaye mahakama hii inaona kwamba alifariki unnatural death (kifo kisicho cha kawaida) akiwa chini ya Jeshi la Polisi Mburahati, Desemba 20, 2020," amesema Hakimu Kiswaga na kuongeza:

"Taarifa (ya uchunguzi) itolewe mahakamani na ipelekwe kwenye vyombo husika ili aliyehusika na kifo hicho achukuliwe hatua za kisheria."

MWANANCHI
Kwahivyo, watajichunguza wenyewe hapa. Eh!
 
Yaani hata wiki aijapita natoka kusoma mahakama imeamuru maiti ifukuliwe kwa uchunguzi, dah!

Leo tena naona mwili wa Stella, J wa Mburahati kufukuliwa alifia kituo cha polisi 2020 kwa kujinyonga.

Hii story ndugu walilia kila magazeti kuomba msaada kuchunguza ndugu yao amejiuaje.

Embu tuwe na ubinadamu jamani. Huyu ndugu zake waliomba sana uchunguzi, sijui iliishia wapi wakaamua kuzika. Leo hii 2 yrs kweli mnaenda kumfukua kuchukua nini huko?

Kama mlishindwa uchunguzi alipofia kituoni leo kuna imani ipi kujua yatakayojiri baada ya uchunguzi nini tofauti na mliyoyasema amejiua?

Tusitiri marehemu wapendwa.

Ombi langu.
 
Anakufa x 2. Tapeli wa kike aliyekuwa amekubuhu. Mungu amhurumie kwa kufanya kazi za kudhurumu na utapeli. Devil
 
Back
Top Bottom