Mahakama yaamuru wabunge 4 wa CHADEMA wakamatwe kwa kukiuka masharti ya dhamana

Mahakama yaamuru wabunge 4 wa CHADEMA wakamatwe kwa kukiuka masharti ya dhamana

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru wabunge wanne wa CHADEMA wakamatwe na kufikishwa mahakamani hapo kwa kukiuka masharti ya dhamana.

Wabunge hao ambao ni washtakiwa katika kesi ya uchochezi namba 112ya mwaka 2018 ni Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini, John Heche mbunge wa Tarime Vijijini, Christopher Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini na Halima Mdee Mbunge wa Kawe.

Amri hiyo imetolewa leo Novemba 15, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kufuatia washtakiwa hao kutofika Mahakamani hapo wakati kesi yao ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa bila ha kuwepo taarifa zozote kutoka kwao wala wadhamini wao.

Michuzi Blog
 
Na Ndugai naye anawaita watoro Bungeni...!!

Mahakamani wanahitajika, Bungeni Ndugai naye anawahitaji.. wakiwepo anatishia kuwafukuza, michango yao anakataa kuisoma kwa madai wameandikiwa..!! Huku nako sasa Hakimu anajimwambafai maadamu tu kumfurahisha mtu mmoja katili sana mwenye roho mbaya shetani akasome..!!

Haki nawaambia Watawala wa zama hizi mshauri wenu ni Mbaya.. Rwanda haiwezi kuwa Tanzania hata siku moja... Nakilini haya!!

BACK TANGANYIKA
 
Chadema hawajifunzi kwa yaliyompata Mh. Mbowe pamoja na Mh. Matiko?? hawakujua kama huu ni mwezi wa 11, na kwa kumbukumbu mwezi wa kumi na moja ndiyo mwezi uliomuumiza Mh Lema (Mbunge wa Arusha mjini), ndiyo uliomuumiza Mh Mbowe pamoja na Mh. Matiko?? Chadema kwa nini mnaruhusu mchawi wenu awafikie mapema???
 
Sasa hawa waende bungeni wasiitwe watoro?

Au waende mahakamani kuhudhuria kanda ya kesi zisizo na mwisho.
Watoe taarifa sehemu moja wapo ,sio kukaa kimya ,

Halafu ionekane wameonewa


Wakati wanavunja sheria , wakienda mahakaman ,watoe taarifa bungeni ,vivyo hivyo waki attend bungeni watoe taarifa mahakaman , kukauka ni kuvunja utaratibu
 
Chadema hawajifunzi kwa yaliyompata Mh. Mbowe pamoja na Mh. Matiko?? hawakujua kama huu ni mwezi wa 11, na kwa kumbukumbu mwezi wa kumi na moja ndiyo mwezi uliomuumiza Mh Lema (Mbunge wa Arusha mjini), ndiyo uliomuumiza Mh Mbowe pamoja na Mh. Matiko?? Chadema kwa nini mnaruhusu mchawi wenu awafikie mapema???

Mtesi hakosi sababu
 
Wanasheria mpo humu tupeni elimu kidogo ikitokea nimekiuka masharti ya dhamana mahakama huwa inapaswa kunichukulia hatua gani? Nasubiri maelekezo.
Ni jambo la kwaida katika mashauri ya jinai. Mahakama hutoa arrest warrant pale mshtakiwa anapokiuka masharti ya dhamana. Mshakiwa hukamatwa ili aje aieleze mahakama kwa nini dhamana isifutwe kwa kukiuka masharti
 
Chadema hawajifunzi kwa yaliyompata Mh. Mbowe pamoja na Mh. Matiko?? hawakujua kama huu ni mwezi wa 11, na kwa kumbukumbu mwezi wa kumi na moja ndiyo mwezi uliomuumiza Mh Lema (Mbunge wa Arusha mjini), ndiyo uliomuumiza Mh Mbowe pamoja na Mh. Matiko?? Chadema kwa nini mnaruhusu mchawi wenu awafikie mapema???
Wanafanya mambo kihuni sana ,

Kuna ubaya gani kutoa taarifa

Mbona wengine hapo inaonesha wametoa taarifa


Wanalalamika uvunjaji wa sheria na taratibu , cha ajabu na wao wamekuwa wanakiuka hata sheria ndogo ndogo

Haya ndio yamesababisha lissu apoteze ubunge,

Kuna tatizo gani kutoa taarifa kwa email , simu, au barua ,?
 
Back
Top Bottom