Mahakama yadaiwa kuamuru Mwanamitindo Noel na Mpambaji Kelvin Events wapimwe endapo wanafanya mapenzi ya jinsia moja

Mahakama yadaiwa kuamuru Mwanamitindo Noel na Mpambaji Kelvin Events wapimwe endapo wanafanya mapenzi ya jinsia moja

Mimi ninamtizamo tofauti, ingawa labda tafsiri au tunavoelewa kila mtu atasema vyake. Mimi wao kupimwa na polisi sioni shida kwani ndio kazi ya jeshi la polisi, watu wanapimwa ulevi, madawa ya kulevya, mimba, DNA nk. Issue inakukuja kwa kuwa waliokamatwa ni watu maarufu na wanapimwa nini. Tusubiri, kama hawafanyi wataachiwa huru kama wanafanya sheria za nchi zinasemaje juu ya tukio hilo.

Mimi najua sheria za nchi hazijabadilishwa na zinakataza mwanaume au mwanamke kuingiliwa kinyume cha maumbile au mwanaume kujifanya mwanamke kwa namna ya maumbile na vitu vinavyofanana na hivyo. Cha msingi kama mnataka kuwatetea mpige kelele sheria ibadilishwe au irekebishwe, vinginevyo tuache polisi wafanye kazi yao kwa mujibu wa sheria. Kwa wanaosema kuhusu ripoti ya CAG kuwa kuna mafisadi na hawashughulikiwi, nimegundua Watanzania kuna vitu vingi hawaelewi wala hawasomi.

Ripoti ya CAG/Auditor huwa inatoa uchambuzi/findings zao kwa hoja ambazo hazikuwa na viambatanishi kwa wakati huo mpaka wanafunga ukaguzi. Wahusika wanapewa muda wa kujibu hoja na kutekeleza mapendekezo ya CAG/Auditor, so huwezi kumpeleka mtu mahakamani au kumwita fisadi kwa ripoti ya auditor inatakiwa iende hatua ya pili ya uchunguzi (TAKUKURU, POLISI kwa ajili ya uchunguzi nk) ndio useme hii ilikuwa ufisadi, wizi nk.

Kuna kipengele kwenye ukaguzi kinachosema "sio kazi ya auditor kugundua udanganyifu" lakini anaweza kusema hapa tunamashaka na taratibu za kisheria na za uchunguzi zikafuatwa, wahusika wakawajibishwa. Shida ya sisi Watanzania tunakurupushwa na matukio bila kuhoji taratibu na sheria zinasemaje na tuko busy kulaumu tu.
 
Back
Top Bottom