Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Haya mambo ya kupima watu wanavyofanyana kuna kipindi tutayaangalia kama kipindi cha kuonea aibu kabisa katika taifa letu.Katika kipande cha amri inayodaiwa kutolewa na mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kivukoni iliyopo Kinondoni inaonesha Mwanamitindo Noel Ndale Mushi maarufu kama Noel ambaye ni mbunifu wa mavazi ya wasanii , Kelvin Maliki Ngao maarufu kama Kelvin Events na Mzungu Mmoja anauejulikana kama David wameamriwa wapimwe endapo wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja yaani ushoga na mpaka sasa bado wanashikiliwa na polisi Oysterbay.
Ikibainika wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja watakabiliwa na kifungo cha miaka 30 jela kwa mujibu wa Sheria za Tanzania.
View attachment 2594881View attachment 2594882
Kwanza unampimaje mtu kwenye hili? Unatumia kipimo gani? Unajiridhishaje mtu yuko alivyo kwa maumbile yake tu au kwa ushoga?
Na kama yeye mtu mzima kaamua kumpa kinyeo chake mtu mwingine kwa hiyari yake, wewe inakuhusu nini?
Halafu basha naye unampimaje? Au yeye hapimwi?