Mahakama yakana kuandika Barua kuzuia mjadala wa Tegeta Escrow Account bungeni

Mahakama yakana kuandika Barua kuzuia mjadala wa Tegeta Escrow Account bungeni

Kuna ambae amekaa kidogo na kujiuliza kwa nini Ndugai hajakalia kiti leo???? Every conspiracy has a theory and any theory can have a conspiracy.
 
Akina Mbatia walitaka kujichukulia umaarufu kwenye jambo hili. Hongera Mahakama kwa kuweka wazi
Yaani Lizabon na wapambe wako ni kama Mende. hamjielewi na mko kizombie zombie tu. masuala muhimu yanayohusu taifa mnafanya mizaha ya kipunguani mkijua fika mnatetea uovu na us..ceng.e wa CCM kukwapua kila kitu . mnaona wezi ni mashujaa misahau majukumu yenu ya kutetea taifa hili linaliwa wa mafisadi (CCM Heros). Huelewi kesho yako wala ya familia yako wa ndugu zako achilia mbali vizazi vijavyo. CCM hamna aibu na sasa mko uchi mnajitetea kujifunika kwa mikono isiyositiri. Mnatumia maneuvers kuhadaa uma ila mtaumbuka tu kwa ushe...nz.. i wenu na ulafi. Kila kitu mmeiba na kujimilikishia kana kwamba taifa halina wananchi. Na kwa taarifa yenu mtaumbuka tu. Walio wengi sasa wanazidi kuamini wapinzani wa kweli ila hao mliowafanya vilaza kama vijana wengi wa CCM walivyo ndo mtawadanganya. Majority of Tanzanians are hating you much .
 
Ndugai alitaka kuosha jina ndo maana akaruhusu mjadala apate sifa za jf,lakini sidhani kama kuna barua
 
hahaha! Ukweli ni kwamba barua hiyo ulishapelekwa ofisi za bunge na ilishapokelewa na mkakati ilikuwa ni kuzuia mjadala kwa kisingizio kuna case mahakamani!

Mh pinda alikuwa ana andaa mazingira ya kuwasilishwa rasmi hiyo barua..hali ya Jana na umoja walio uonesha wabunge umefanya barua hiyo hikanwe!
 
Mh kumbe wote tumelogwa na Marehemu.

Hivi Pida kwa nafsi yake aliyonayo katika nchi naye alikua anajibu issue ya barua ambayo haipo? Mbon nashindwa kuelewa hapa.Pnda si ndio President Kwasasa?

who is fooling who?

Da kweli anaweza kuwa Rais Pinda kwa sasa wakati JK yupo hospitalini!
Je kwa mujibu wa katiba yetu ya sasa ni nani ameshikia usukani ama nchi inaendeshwa kutokea Marekani?



Sent from my iPad using JamiiForums
 
Majibu ya Mtoto wa mkulima ndo yaliibua hasira za wabunge... perception ikabadili hali ya hewa kila mtu akahisi kuwepo barua.

Mjadala ukiwapo, aibu yao itakuwa haisemeki... Andaa pop corn na juice ya ukwaju tu FaizaFoxy

Nnautamani huu mjadala wa escrow uwe leo kabla ya kesho.
 
Akina Mbatia walitaka kujichukulia umaarufu kwenye jambo hili. Hongera Mahakama kwa kuweka wazi

Kweli ukubwa wa kichwa sio wingi wa akili, sasa akina Mbatia wanaingiaje hapa? Jana wabunge wote walisimama kidete kwenye jambo hili mpaka spika mwenyewe ila wewe umewaona kina Mbatia? Stupid, shameless and nonsense person I have never seen in social media.
 
FaizaFoxy;

Ukweli ni kwamba barua ya Mahakama ilishaandikwa na ilikuwa imepokelewa ofisi ya Spika. Baada ya joto kupanda kutoka kwa Wabunge wa kutokubaliana na upuuzi huo wa kutaka kulizuia Bunge kujadili hoja ya Escrow wameamua kui-withdraw hiyo barua.

Watakuwa wamepima upepo wa Bunge wakaona itakuwa soo. Kwa hiyo mama usikurupuke kuwa hakukuwa na barua. Tunajua siasa za ma-CCM za kukanusha kila kitu hata kama kipo na kinaonekana wazi. Usifikiri kuwa watu wote wanakubaliana na upuuzi wa CCM wa kulinda ufisadi. Nina hakika kuna watu ndani ya Bunge walishaiona hiyo barua na kuwatonya baadhi ya Wabunge wa upinzani.

Porojo hizo.
 
Hivi huyu Lizaboni ninani, ni Mtanzania? Manake sijawahii kuona hata siku moja akichangia hoja yeyote positively.

Si ajabu ukimwambia anakunya atakataa akuambie yeye hanyagi?

This is very serious. He is always negative in everything!

Lizaboni ni Kuchi wa CCM
 
Wakati Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakichachamaa wakisema hawatakubali Bunge hilo kuingiliwa na mhimili wa Mahakama, Mahakama hiyo imejiweka kando na tuhuma hizo.

Sakata hilo lililotawala kikao cha Bunge hilo jana lilitokana na madai yaliyoibuliwa juzi na wabunge wa kupinzani unaoundwa na vyama vya CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi.

Wabunge hao Tundu Lissu (Chadema), James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Habib Mnyaa (CUF) waliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma juzi kuwa wamepata taarifa za uhakika kuwa Mahakama imeandika barua ikiritaarifu Bunge lisijadili kashfa ya uchotaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania.

Wabunge hao, walisema kuwa hatua hiyo ni kuingilia uhuru wa mhimili wa Bunge na kwamba lengo lake ni kutaka kukwamisha ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili wahusika wasichukuliwe hatua.

Msajili wa Mahakama Kuu, Amir Msumi, alipotakiwa jana na NIPASHE kuthibitisha kama Mahakama imeandika barua hiyo kwenda Ofisi ya Spika wa Bunge kuzuia suala hilo lisijadiliwe kwa kuwa kiko mahakamani, alisema yeye na wasajili wenzake hawana taarifa kuhusu kuandikwa kwa barua hiyo.

“Labda unieleze hiyo barua imeandikwa na nani na lini, kama ni Jaji au Msajili nitajie jina lake ili iwe rahisi kufuatilia, lakini hadi sasa nimepekua kwenye kumbukumbu zetu sijaona barua hiyo,” alisema Msumi.

Aliahidi kwamba jana angewasiliana na wenzake wa Mahakma ya Rufani kama kuna barua imeandikwa kutoka mahakama hiyo kwenda bungeni.

Hadi sasa hakuna mamlaka yoyote ya serikali iliyothibitisha rasmi kama kuna barua iliyoandikwa na Mahakama kwenda Ofisi ya Spika wa Bunge.
Juzi Naibu Spika,Job Ndugai, alisema kuwa ofisi ya Spika haijapokea barua hiyo.

Hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akizungumza bungeni jana kuhusiana na madai hayo, hakuthibitisha wala kukanusha kama kuna barua iliyoandikwa na Mahakama kwenda bungeni kuzuia mjadala huo, zaidi ya kusisitiza itumike busara ili kuepusha mihimili hiyo kuingiliana katika majukumu yao kwa mujibu wa Katiba ya nchi.


Chanzo: Nipashe

ha ha haaa
 

hebu tuache wendawazimu,
naibu spika aliruhusu mjadala wa barua ambayo ofisi yake haijaipokea??

Naibu spika hakuruhusu chochote kuhusu barua yoyote na ndiyo maana Tundu Lissu alirudia mara kumi "kama ipo".
 
Akina Mbatia walitaka kujichukulia umaarufu kwenye jambo hili. Hongera Mahakama kwa kuweka wazi

Mchawi ukimwambia wazi mbele za watu kuwa yeye ni mchawi basi hawezi kukuloga tena. Hiki ndicho walichokifanya akina Lissu.
 
tunataka barua hakuna cha kusema kama ipo,wasingeenda kwenye vyombo vya habari kutangaza,tunataka kujua nani muongo,waliosema kuna barua toka mahakamani na wanaokana hamna barua kutoka mahakamani. lisiwe bunge la kisanii. TRURH WILL ALWAYS PREVAIL

suala sio kama barua ipo au haipo! suala ni #BringBackOurMoney
 
Kama mna hakika kuwa barua hiyo ipo mbona hamjaiweka kwenye mtandao?

lizaboni una moyo wa chuma. pamoja na kwamba hujaonja chochote lakini bado umesimamia upande wa mapanya wanaosaga rasilimali za walalahoi. ama kweli we ninouuma na kinachokufanya ubwa..bwa.je humu ndani ni kwa kwa sababu wadau hawajui hata sura yako ikoje? maana tunaweza kufikiri tunajibizana na mtu kumbe zi..mwi..mtu acha mi nsepe tu nihamie uzi mwingine :car:
 
Serikali sasa iunde wizara ya kukanusha na prof kikwete ateue waziri wa ukanushaji!
 
Iyo mahakama yenyewe nayo inaogopa sasa kubebeshwa msalaba, Tundu lissu aliahidi kama kuna barua na muswada hautasomwa bungeni ccm wangekiona cha moto huko nje
 
Back
Top Bottom