Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!

Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!

Sijui huo ukoje ila mimi nimekopa CRDB Kwa dhamana ya ajira, mkopo ulikuwa 6,000,000/= (miaka miwili)
Makato kwa mwezi ni 285,000X24=6,840,000
Riba hapo Kwa miaka miwili ni asilimia 14
mie walinikopesha nililia na mkopo lipaaa weee mkopo hauishi nikapata vihela nikawalipa vyote, oh eti tukupe tena! Fakaoff
 
Mkopo huo uliokuwa na riba ya 18% ulielezwa na msanii huyo kama uwekezaji kwenye shughuli zake za kimuziki ikiwemo studio ya kisasa ya uzalishaji wa muziki na video, ulikuwa ulipwe ndani ya miezi 36 (miaka mitatu).
Na ulikuwa mkopo wa awamu mbili, ya kwanza ikiwa milioni 100 kisha awamu ya pili milioni 200 ambazo awamu zote alipewa na benki hiyo mwaka huohuo wa 2019.
Inaelekea hao crdb siyo makini kabisaa.

Loan manager aliyeidhinisha huo mkopo inafaa awajibishwe

Walimpa pesa ya kut#mbea kashafanya kweli, wao wanaanza kulialia, akiwalipa atahonga nini? Watulie tuli, na ndiyo wajue siyo kila mtu ni wa kukopesha
 

View attachment 3072826
View attachment 3072827

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rajabu Abdukahali Ibrahim almaarufu Harmonize ametiwa hatiani na mahakama kuu divisheni ya biashara tarehe 2 mwezi huu wa 8 kwa kushindwa kulipa kikamilifu mkopo wa kiasi cha shilingi milioni 300 alizokopa katika benki ya CRDB mwaka 2019.

Mkopo huo uliokuwa na riba ya 18% ulielezwa na msanii huyo kama uwekezaji kwenye shughuli zake za kimuziki ikiwemo studio ya kisasa ya uzalishaji wa muziki na video, ulikuwa ulipwe ndani ya miezi 36 (miaka mitatu).
Na ulikuwa mkopo wa awamu mbili, ya kwanza ikiwa milioni 100 kisha awamu ya pili milioni 200 ambazo awamu zote alipewa na benki hiyo mwaka huohuo wa 2019.

Moja ya makubaliano ilikuwa (Harmonize) kufungua akaunti ya kibiashara katika benki hiyo kisha kuiweka milioni 100 na kuifanya akaunti hiyo kuwa akaunti yake kuu katika shughuli zake za kibiashara, takwa hilo pamoja na mengine ikiwemo marejesho ya mkopo kwa kila mwezi yalishindwa kufikiwa na Harmonize.

Baada ya usumbufu uliopitiliza wa ulipaji wa mkopo huo kutoka kwa Harmonize, CRDB walifikia uamuzi wa kwenda mahakamani. Uamuzi huo ambao mahakama ilitoa wito mara kadhaa kwa Harmonize, lakini Harmonize hakufika mahakamani. Na hata mahakama ilipomuomba kutoa maelezo (Written statement of defence WSD) hakufanya hivyo.

CRDB waliendelea kumkumbusha Harmonize kulipa mkopo kila mara na kila njia hadi zikiwemo jumbe za WhatsApp, mwanzoni mwa mwaka 2022 Harmonize aliandika barua kwenda tawi la benki hiyo lililopo Mlimani City akiomba kulipa marejesho kwa kiasi cha 3.3 milioni badala ya utaratibu uliowekwa wa 10.8 milioni kila mwezi wakati huo deni la mkopo likiwa 109,731,733.46/= CRDB walikubali ombi lake hilo ila akitakiwa kulipa 3.9 milioni badala ya 3.3 milioni aliyokuwa ameomba.

Harmonize alifanikiwa kupunguza deni hilo hadi kufikia kiasi cha 103,185,755/=
Baada ya hapo hakulipa tena hadi kufikia hukumu iliyotolewa 2/08/2024 ambapo msanii huyo ametakiwa kulipa kiasi chote kilichobaki katika mkopo, gharama za kesi na fidia ya milioni 10 na nyinginezo kama mahakama ilivyoona.

Chanzo changu na mimi,

Nifah.
"......Kajala one two tena zote ni range........" kumbe bank inakudai 190m,hizi nyapu ukiziendekeza lazima kuna siku zitakupoteza.

Unaleta usela mbele ya taasisi kubwa,sasa ni mda wa kupambana na sheria na bank zinajua kudai hazinaga masihala.
 
Ila Harmonize ni mtata kwenye kulipa madeni, nakumbuka miaka kadhaa hapo nyuma amewahi kukimbia deni la kodi ya nyumba aliyokuwa akiishi huko Mbezi Beach kwa Mchagga mmoja kama 150 Milioni hivi.
Duuu na huyo Mchaga alimwachia? Naona sasa hivi yule mdangaji aliyekuwa naye Posh anatafuta namna ya kuachana nae,kwani maslay queen na njaa ni vitu viwili tofauti.
 
Mkopo huo ulikuwa wa Dhamana ya Ardhi (Nyumba) (Mortgage) au ni wa Nini hasa??? Dhamana au rehani aliweka assets gani ili kudhamini huo mkopo? Milioni 300 aliwezaje kukopeshwa na benki ya CRDB kiurahisi hivyo bila ya kuweka rehani mali yake yoyote ile? Ina maana kwamba alikopeshwa pesa nyingi kiasi hicho bila ya Mkopeshaji (Crdb) kujiridhisha Kwanza kuhusu uwezo wa mtu huyo wa kulipa marejesho ya deni lake???

Anyway, mkopo siyo sadaka, Mkopaji alipaswa kukopa kwa malengo.
Dawa ya deni ni kulipa.
Dhamana ilikuwa kajala, Sasa kajala kaingia mitini
 
Sijui huo ukoje ila mimi nimekopa CRDB Kwa dhamana ya ajira, mkopo ulikuwa 6,000,000/= (miaka miwili)
Makato kwa mwezi ni 285,000X24=6,840,000
Riba hapo Kwa miaka miwili ni asilimia 14
Chief inabidi nijifunze hizi riba za traditional banks.

6M unakaa nayo kwa miaka 2 na unarudisha 840K tu riba hii ni affordable kwa ninavyoona na bank haitatengeneza maximum profit.

Kwa hesabu ninazojua inatakiwa ulipe 7,680,000
 
Kama kijana ninafikiri harmonize is worth more than 300M ila kwa kuwa anadaiwa ni vyema akawa na team nzuri kutafuta endorsement mbalimbali, hata hapo CRDB anaweza kupata Dili la 500M

Kingine awe na mhasibu na wanasheria wamshauri vizuri.

Ukisoma hukumu alitakiwa kuwajibu kiungwana na kuomba rejesho lipunguzwe lakini alipuuzia. Kama huyo ni harmonize wasanii wetu bado Sana 😃😃Mtandale anafanyaje??
 
Back
Top Bottom