Mahakama yamuachia huru Lengai Ole Sabaya, yasema ushahidi wa Jamhuri una utata
Quality/performance wa state prosecution team leaves much to be desired compared to the team which was prosecuting Mbowe. Does this has anything to do with remunerations????
 
Form 4 mwenye ziro amepewa nafasi yakuandaa mashitaka magumu akati wamezoea kuandaa kesi zamchongo wizi kuu
 
Haiondoi jinai alizofanya bali ni procedural errors/defects tu zilizojitokeza ndo mwanya wa kushinda unapojitokeza.

Kama Jamhuri ikikata rufaa kwa kuzingatia mambo yote muhimu lazima adhabu ipo pale pale.

Hata hivyo akichomoka kwenye kesi zake zote basi amejifunza madaraka na sponsor huwa yana kikomo. Hatomtegemea binadamu mwenzake tena.

Hili ni funzo hata kwa sisi wengine. Hata leo hii apewe madaraka ya mkuu wa wilaya kama awali atakuwa na adabu na heshima sana kwa wananchi. Hatowagongelea tena misumari ya ugoko.
Endelea na imani hiyo sisi tunajua ni mtu saafi maana hajakutwa na hatia. Shida yenu mnaamini ya kusikia tu, ulimuona? Kwa nini hukjapeleka ushahidi ili ahukumiwe?
 
Hivi kwa akili yako ndogo kama Mhe Rais Samia angekuwa anaingilia mahakama na kutoa maelekezo ya nini na nani afungwe ama aachiwe huru unadhani Sabaya angetoka? Thubutu!

Mama Samia hana mpango wa kuingilia uhuru wa mahakama ndo maana unaona mambo yanafanyika kwa uwazi na yeye hana muda wa kuingilia mahakama.

Laiti Mhe Rais angesema atoe maelekezo ya Sabaya kufungwa unadhani angechomoka? Angefungwa hata miaka tisini kwa kesi zake zote ila mama ana busara anapenda kuona haki inatendeka.
😂😂 kwa hiyo hajaingilia means Sabaya ni mwema maana ni maamzi pure ya mahakama. Tusisumbue vijana mahabusu huku hatuna ushahidi kwa mashtaka yao, mlistahili kumlipa Sabaya. Mkikuta mtu alikuwa kipenzi cha rais basi rais akitoka mnataka mmtendee mabaya.
 
Yani sabaya afanye kazi nzuri ya chama then tumtose?haiwezekan
 
Hizi kesi za Sabaya naona serikali baada ya kuona Sabaya amenyoshwa kiasi sasa inaziagiza mahakama zimuachie tu huru hata hii ya Moshi nahisi itakuwa hivyo hivyo tu.

Tanzania tuliamua kuua kabisa mfumo wa mahakama na kufanya rais ndiyo awe mahakama na bunge vile vile.
 
Hatima ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi inatarajiwa kujulikana leo Juni 10, 2022.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha iliyokuwa ikisikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27/2021 imepanga kwa mara ya pili kutoa hukumu hiyo.

Awali, Mei 31, 2022. Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Patricia Kisinda aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo, alipanga kutoa hukumu lakini ilishindikana kutokana na kudaiwa kuwa nje ya kituo cha kazi kwa majukumu mengine.

Sabaya na wenzake walikuwa wakisubiri hukumu hiyo endapo wangeachiwa huru au la, kabla ya kufunguliwa kesi nyingine na wenzake watano ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Juni Mosi, 2022

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Fadhil Mbelwa akiahirisha kesi hiyo Mei 31, 2022 alisema hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo amepangiwa majukumu mengine nje ya kituo cha kazi hivyo hukumu hiyo itatolewa leo.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa baada ya kesi hiyo kusikilizwa kwa miezi saba tangu ilipoanza Julai, 2021.

Sabaya alikamatwa Mei 27, 2022, Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam na kufikishwa mahakamani Juni 4, 2021 na kufunguliwa kesi mbili tofauti.

Katika kesi ya kwanza walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, hukumu ambayo Mei 6, 2022 ilitenguliwa na Mahakama Kuu na kuwaachia huru baada ya kubaini dosari.


============================

SABAYA NA WENZAKE WAACHIWA HURU

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewaachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake sita waliokuwa wanakabiliwa na Kesi ya Uhujumu Uchumi.

Mahakama imesema ushahidi uliotolewa na Mashahidi wa upande wa Jamhuri ulikuwa na utata. Pia imeelezwa kuwa Hati ya Mashtaka ilikuwa na mapungufu ya Kisheria.

Hata hivyo, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu, John Aweyo na Nathan Msuya wataendelea kubaki Mahabusu kutokana na Kesi nyingine ya Uhujumu Uchumi waliyonayo Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.
Kina cha maji kinapimwa kwanza na kuuangalia upepo huku watanzania wakiandaliwa kisaikologia ili hatimaye waweze kupokea maamuzi ya kuachiwa huru kwa Sabaya!! mi naona aachiwe tu maana tayari tumeshaandaliwa vizuri kisaikologia!
 
Lengai Ole Sabaya bila shaka angeachiliwa huru tarehe 31 May 2022 kama hukumu yake iliyosomwa 10 June 2022 ingesomwa 31 May 2022.

Hivyo sababu ya Hakimu kuahirisha siku hiyo kusoma hukumu sio kwamba alikuwa na kazi nyingine bali ni ili kupisha na kufanikisha nia ovu ya Kweka na Ndugu zake ili kufungua kesi nyingine dhidi ya Sabaya na wenzake huko Moshi huenda wakiamini watamuumiza kwa urahisi.

Kesi yake ya pili Arusha ilikuwa ya uhujumu Uchumi, na hii ya tatu Moshi chini ya huyo huyo Naibu DPP Kweka bado ni ya uhujumu uchumi. Utafikiri Kweka alipewa hicho cheo ili kumshugulikia Bwana Sabaya.


Hadi sasa hadi kipofu anaweza ona hizi kesi hazina mzingi wowote wa kisheria bali matumizi mabaya ya madaraka anayofanya Kweka ili kutimiza malengo ya Ndugu zake wauza madawa ya kulevya, watengeneza pesa feki, majambazi, wezi wa magari.

Kweka napenda tukueleze kuwa endelea kutumika na hao ndugu zako brother ila utalipia wewe, mkeo, wanao, Wazazi wako, wakwe zako, michepuko yako, kaka na dada zako na hata chawa zako.
 
Wewe kipenzi cha jambazi wacha kupeleka lawama zako pasipohusika, mimi binafsi bado nashangaa mpaka leo kwanini jamhuri hawakukata rufaa kwa ile hukumu ya mwanzo ya miaka 30 aliyopewa Sabaya.

Ushahidi wa aina zote ulikuwepo pale, CCTV Camera, Sabaya mwenyewe kwenye utetezi wake alikiri kuingia kwenye eneo la mtu akiwa na silaha bila kibali, huu ulikuwa ni uvamizi, wewe mtetezi wa jambazi badala ya kuona Sabaya anaonewa, mshukuru huyo Kweka.
 
Wewe kipenzi cha jambazi wacha kupeleka lawama zako pasipohusika, mimi binafsi bado nashangaa mpaka leo kwanini jamhuri hawakukata rufaa kwa ile hukumu ya mwanzo ya miaka 30 aliyopewa Sabaya.

Ushahidi wa aina zote ulikuwepo pale, Sabaya mwenyewe kwenye utetezi wake alikiri kuingia kwenye eneo la mtu akiwa na silaha bila kibali
Wewe shabiki wa DJ Zero na Wachaga majambazi jueni bado tutawashugulikia.
 
Back
Top Bottom