Mahakama yaridhia kunyongwa aliyemuua Dereva Bodaboda



Mimi sio mtaalamu sana wa mambo ya sheria lakini Katika shauri hilo kuna kesi mbili, ya kwanza ni mauaji ambayo ni kubwa na ya pili ni uporaji, kesi kubwa huwa inameza kesi ndogo.

Kesi ya huyo mhusika ilikuwa ni kesi ya mauaji, hivyo ninachokiona mimi ni kwamba alishindwa kujitetea jinsi alivyopata hiyo pikipiki ndio maana katiwa hatiani hata kama hakuhusika na hayo mauaji.
 
Kwahiyo aliuziwa bila ushahidi wa watu wala wa kimaandishi ?

Aliyemwuzia si angejulikana ?
Pikipiki ya wizi kuna vibali flani inakosa na inajulikana ni ya wizi.

Mwenye pikipiki alitoa ushahidi wa vibali na wa maneno kuwa Marehemu alikuwa anatumia pikipiki kwa ruhusa yake ya kutafuta pesa. Na baadhi ya vibali alikuwa navyo.

Sasa Mjomba unanunua pikipiki kama unavyonunua Embe unategemea nini ?

Ndio maana kesi imedumu muda mrefu ni kwamba Mahakama ilitaka kujiridhisha.

Na mara zote kesi ya Mauaji mtuhumiwa anapewa Wakili wa Serikali bure ili kumsaidia kuepusha kumwadhibu mtu kwa kubahatisha.
 
Mbona umejichanganya?

Unasema wewe siyo mtaalamu wa sheria, lakini hapo hapo unasema “kesi kubwa huwa inameza kesi ndogo”

Lakini hapo hapo unataka kesi ndogo(ushahidi wa kukutwa na pikipiki), ndiyo itumike kutoa hukumu ya kesi kubwa(mauwaji)?

Kama kukutwa na pikipiki ni kesi ndogo, kwanini itumike kutoa hukumu ya mauwaji ambayo ndo kesi kubwa kwa mujibu wa maelezo yako?
 
Kwahiyo Jamaa amehukumiwa kifo kwa sababu tu alikamwatwa na Pikipiki aliyokuwa anaendesha Marehemu?

Kwamba ameua wamethibitishaje sasa?

Na amini kuna zaidi, mfano kashindwa toa maelezo ya msingi na yanayoeleweka kusema aliitoa wapi, hapo panaweza amua kama yeye ni muuwaji.

Mfano, akijaribhwu kubisha kwamba pikipiki ni yake anayo miaka mingi, na ikathibitika ni ya marehemu, kwa nini aseme uongo
 


Ni hivi; Mtu aliyeuawa (kama inavyoelezwa) aliuawa na kuporwa pikipiki, yaani sababu ya kuuawa kwake ni ili aporwe pikipiki au aliuawa katika mazingira ya kupambana ili asiporwe pikipiki, kesi hapo inakuwa ni ya Mauaji na hiyo ya uporaji inakufa kifo cha mende, Uchunguzi lazima uwe na mwanzo na mwanzo wake ndio hapo kwamba; siku ya pili TU baada ya tukio ndipo mtu kakutwa/kakamatwa na pikipiki ile ile aliyokuwanayo mtu (bodaboda) aliyeuawa, sasa ilikuwa ni jambo rahisi tu kwa huyo mtu kujibu hili swali; Pikipiki hii umeipataje?? --- bila shaka ni majibu ya swali hili ndiyo yamemtia hatiani kwenye mauaji ya dereva wa boda boda.
 
Hii ni hukumu mbovu; ultimate penalty ya kifo inatakiwa itolewe kwa ushahidi solid ukiambatana na silaha iliyotumika kufanya mauaji, sio huu wa kukutwa na pikipiki ya marehemu. Inawezakana aliiba kwa mtu mwingine bila kujua kuwa ilikuwa pia imeibiwa kwingineko.

Halafu Mzuzuri Ukiwaona ditopile alipoua dereva wa daladala hivyo kwa kumpiga risasi ya papo kwa papo kukiwa na ushahidi lukuki, eti kesi yake ilibadilika na kuwa ya kuuwa bila kukusudia; ndipo uijue jinsi haki inavyotolewa na mahakama zetu.
 
Na jamaa alitaka kuchomoka kwa kutaka izibitishwe je hyo pikipiki ndio aliyokua nayo marehemu kupitia TRA...

Sasa TRA hawajatokea hapo ushahd unaacha shaka
 
Piki piki ya kuibiwa tena kwa kuuwawa mtu haiwezi kutoroshwa kwa njia rahisi kama hiyo.
Huyo ni mnunuzi wa vitu vya deal na alikuwa hajui the extent kwamba kuna siku atanunua vitu vya tukio la mauaji ,ndo yamemkuta .
Hayoo yoote uliyoesema hakuna mahala umeonyesha kuwa mtuhumiwa ndiye muuwaji, ana kesi kadhaa za kujibu ikiwepo kununua au kukutwa na mali ya wizi , ,
 
Tuanzie hapa.
Mtuhumiwa ndio mwenye pikipiki.
Tunaomba lisiti za Ununuzi wake.

Kama huna tunamwomba mmiliki halali wa hiyo pikipiki uliyokutwa nayo
 
Suala la kuthibitisha kosa si la mtuhumiwa, ni mwendesha mashtaka au mahakama kuthibitisha kuwa mtuhumiwa ana kosa.

Ni sawa nipelekwe mahakamani kwa kosa la wizi halafu mahakama iniambie nithibitishe kama mimi siyo mwizi!
 
Umiliki wa pikipiki ulithibitishwa mahakamani?
Kama nilivyosema, labda taarifa kuhusu kesi hii iliyoletwa hapa haijakamilika.
Kulikuwa na shida gani kupata uthibitisho kutoka TRA kuhusu umuliki wa pikipiki ili ijulikane kwamba ndiyo aliyokuwa akiiendesha marehemu?
Ndiyo maana nasema labda walichukuwa ushahidi mwingine zaidi ya hiyo pikipiki na ndiyo wakautumia kutoa hiyo hukumu.
 
Na jamaa alitaka kuchomoka kwa kutaka izibitishwe je hyo pikipiki ndio aliyokua nayo marehemu kupitia TRA...

Sasa TRA hawajatokea hapo ushahd unaacha shaka


TRA wanachoweza kuthibitisha ni umiliki wa pikipiki na sio nani alikuwa anaendesha pikipiki na wakati gani.
 
Piki piki ya kuibiwa tena kwa kuuwawa mtu haiwezi kutoroshwa kwa njia rahisi kama hiyo.
Huyo ni mnunuzi wa vitu vya deal na alikuwa hajui the extent kwamba kuna siku atanunua vitu vya tukio la mauaji ,ndo yamemkuta .


Sasa ndio angesema kwamba hiyo pikipiki kanunua kutoka kwa watu au mtu fulani ili asalamike na mauaji, mbona ni jambo rahisi sana. Kinachoonekana naye alihusika moja kwa moja katika hilo tukio.
 
Kule Kenya kuna Dogo ni m anafunzi wa Chuo kikuu alikutwa na simy kumbe simu ilikuwa ya raia mmoja wa Uganda alie uwawa na kuporwa vitu, sasa dogo kanunua simu, hadi sasa yuko ndani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…