Mahakama yaridhia kunyongwa aliyemuua Dereva Bodaboda

Kama alipinga hajaua kwanini asingefunguka kila kitu akaeleza mpaka situation ilivyokuwa yeye kuipata hiyo pikipiki?

Nazani uchunguzi ungefanyika, but kitendo cha yeye kuomba rufani kwa hoja za kijinga kabisa madhara yake ndo kama hayo, linaenda kufa kipumbavu kabisa, and i bealive huyo jamaa sizani kama alikuwa mwenyewe kwenye hilo tukio.
 
Unamhukumu vipi mtu kufa kwa ushahidi wa kimazingira tu?
Nashauri akaombe Review ya Court of Appeal, anaweza akashinda
Tumia akili hakuna muuaji aue kisha abaki na ushahidi, ataua ataiba na kwenda kuiuza pikipiki. Kwa nchi zilizoendelea kwa ushahidi huo tu, huyo jamaa angekutwa na hatia tofauti, sio ya mauwaji.
Muuaji hawezi UA, akachukua pikipiki afu kesho aiendeshe maeneo hayo hayo
Acheni unaa...
 
Ndo maana twasema kuna kitu hakiko sawa.

Mtu hawezi UA afu siku ifuatayo akaitumia hiyo pikipiki
Labda tusaidie wewe bushlawyer amekutwa na pikipiki ya wizi ameulizwa ameipataje akasema ni yake hana viambata vyovyote hukumu ungetoaje
 
Kwahiyo Jamaa amehukumiwa kifo kwa sababu tu alikamwatwa na Pikipiki aliyokuwa anaendesha Marehemu?

Kwamba ameua wamethibitishaje sasa?
Ukakasi, huyu angeshtakiwa kwa kukutwa na pikipiki ya marehemu tu muuwaji waendelee kumtafuta pengine hata kumtumia huyu kusaidia polisi
 
Kama marehemu hakuwa mmiliki halali, haki iende kwa muuaji?
Tuseme kakutwa na boxer nyekundu ambayo ndio rangi ya piki piki aliyokua nayo marehemu, je boxer nyekundu ipo moja tu Tanzania so lazma ithibitishwe kuwa ndio hyo kwa marakatasi hyo ndio sheria ndio mana kuna mawakili....
 
Hapa ndipo intelligence inatakiwa kuzingatia. Mtu aibe mali ya wizi tena m'miliki wake ameuwawa halafu atembee nayo mchana kweupe.
Kuna kitu hakiko sawa mahali
 
Kwa nini hawezi? Wapo watu wenye uthubutu huo- mfano ndo huyo njemba.
Halafu kumbuka damu ya mtu haipotei kihivi-hivi. Mbona hasemi bayana aliipata-pataje hiyo pikipiki??. Wahenga walisema "anayekutwa na ngozi ndiye mwizi"
Inapotea vizuri tu, we jichanganye ndo utajua hujui
 
Mkuu, sisi humu Jf tumepata digested story tu na si mchakato mzima wa kesi ulivyokwenda.

Mchakato mzima na simulizi za mauaji, kesi, mashahidi nk nk havijasemwa hapa na ndiyo maana inakanganya na kuonekana kama huyo mtuhumiwa hawezi ua na kuitumia hiyo pikipiki kwa wakati huo huo!

Cha kuzingatia hapa ni kwamba, mpaka mtu akahukumiwe kunyongwa, maswali yote tunayojiuliza na kujijibu wana Jf, yalishaulizwa mahakamani na yakapata majibu yasiyoacha mashaka kuwa mhusika wa mauaji ndiye yeye.

Haya, kama jaji aliyemhukumu mwanzo alijikanganya, basi mahakama ya rufaa ingelibaini mianya na mapungufu ya kisheria iliyomtia hatiani mtuhumiwa.

Ukiona wamebariki "go ahead", usichukulie poa.
 
Sasa ndio angesema kwamba hiyo pikipiki kanunua kutoka kwa watu au mtu fulani ili asalamike na mauaji, mbona ni jambo rahisi sana. Kinachoonekana naye alihusika moja kwa moja katika hilo tukio.
Kuna wakati kesi inakuwa kubwa hadi watuhumiwa wanafeli utetezi ulio wa wazi kabisa, huyu jmaa keshakaa rumande muda mrefu , rumande kuna wanasheria bubu wanaweza kumis lead mtu akaogopa kusema ukweli . Akodhani atasalimika
 
Ndo maana twasema kuna kitu hakiko sawa.

Mtu hawezi UA afu siku ifuatayo akaitumia hiyo pikipiki
Nadhani hiyo ni assumption, Cha msingi alikamatwa na hiyo pikipiki. Inawezekan Kuna mtu alimchoma au walimshuku kuwa ndio muuaji.
 
Kaiba pikipiki halafu aliyeibiwa kauawa kwenye tukio, aliyeiba ndio muuaji mwenyewe.
 
Ndo maana twasema kuna kitu hakiko sawa.

Mtu hawezi UA afu siku ifuatayo akaitumia hiyo pikipiki
Usiseme hivyo kwa kua hayajakukuta, watu wanaua na wanakwenda Bank wanachukua Mali za Marehemu bila hata ya uwoga na kujimilikisha!!
 


Duh!!!!
Hatari sana hiii... yaani sababu tu alikutwa na pikipiki ndo ushahidi tosha kuwa aliuwa. Nilidhani adhabu ya kifo inatakiwa ushahidi uwe "beyond resonable doubt"? Kama ndo hivi basi kuna shida kubwa sana katika mfumo wetu wa haki. Nadhani hata aina ya upelelezi unaofanywa na polisi wetu una "reflect" hichi kitu!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…