Mahakama yatupilia mbali mapingamizi ya utetezi, maelezo ya Mohamed Lingw'enya yapokelewa na Mahakama. Kesi kuu kuendelea Des. 15, 2021

Mahakama yatupilia mbali mapingamizi ya utetezi, maelezo ya Mohamed Lingw'enya yapokelewa na Mahakama. Kesi kuu kuendelea Des. 15, 2021

Usidanganywe, Jaji kituo chake cha kazi ni Mwanza, mawakili wote wanatoka mikoani, taratibu za kiutumishi zipo wazi mkuu mtumishi asipokuwepo kwenye kituo chake cha kazi kikazi atalipwa kulingana na taratibu na miongozo ya serikali, hao wote kila siku wana lamba 120000 nje na mishahara yao pamoja na wasaidizi wao(dereva na walinzi @ 100,000)
Mkuu wewe endelea kujidanganya kazi ya uwakili wa serikali na per diem hahaha
 
Chenga Sana eti ugaidi wa laki 6 is it possible? Rasilimali pesa zinateketea kisa kukosolewa na kutaka katiba mpya
 
Naona Pius Hilla na Nassoro Katuga wameanza kuwa mwiba wa moto kwa washitakiwa. Mawakuli wa utetezi wamejaribu kila mbinu, kila janjajanja, lakini wanakwaa kisiki kama cha mpingo. Itabidi ema warudi shule au tubadilishe Wakili, hizi pingamizi za kitoto sasa zimeanza kutuchisha Wanachadema.
Lissu mwanasheria nguli rudi home umupambanie Mwenyekiti.

Au umeamua kumutosa baada ya kuona jinsi Mahakama inatenda haki,kama ilivyokufutia kesi zako?
Na wewe unajua mengi kwenye chama hata yale maandamano unajua vema lengo lake,japo hukutokea.
 
Unajua tunaweza kuongea kwa ushabiki na hisia tu! Ila watu wakumbuke Mbowe anamakandokando pia ya kuhusika na kifo cha Chacha Wangwe! Usimwamini mwanadamu huwezi kujua alivyo ndani yake! Mahakama waiache iwe huru kama kwa Sabaya!
umenena mkuu.
Ndio maana hata John Mrema alisema; "....Hatuwezi kufahamu mambo yote anayo yafanya mwenyekiti......."
waswahili wanasema; nafsi/moyo wa mtu ni kichaka.
Mbowe sio Malaika.
 
Mahakama kuu, Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na rushwa, Ubungo-Mawasiliano, DSM, 14/12/2021


Wakati washtakiwa wote wakiwa wameingia mahakamani muda huu, ingawa bado hawajapanda kizimbani na mawakili wa pande zote wameingia ndani ya mahakama.. waandishi wa habari wamemzunguka FREEMAN Mbowe na washtakiwa wenzake na wanataka picha za ‘fonti fedii’ pale…

Jaji ameingia Mahakamani

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi

Nashon Nkungu
John Malya
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata
Seleman Matauka
Edward Heche
Alex Massaba
Gaston Garubindi
Sisty Aloyce

Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani....

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kutolewa Uamuzi tupo tayari Mheshimiwa

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji, Na sisi Pia Kwa Ruhusa yako tupo tayari

Jaji anaandika Kidogo, Mahakama ipo kimya

Jaji: Shauri hili ni kweli lina kuja kwa ajili ya Uamuzi ambao ulikuwa really served

Mahakama ilielekeza Mawakili Walete Hoja zao Kwa Maandishi ambapo wameleta

Wakati shahidi namba 08 ASP Jumanne Wakati Wa Kutoa Ushahidi Wake

Alieleza Kwamba alipewa kazi ya Kuandika Maelezo ya Mshitakiwa Wa tatu, Na baada ya Kueleza hivyo aliomba Maelezo hayo ya pokelewa Mahakamani, Ambapo Upande wa Utetezi Walipinga kwa Sababu 9..

Sababu ya Kwanza ni Mshitakiwa namba tatu hakuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.. Na Haku andika Maelezo yoyote..

Sababu ya Pili Mshitakiwa Wa tatu alilazimishwa Kuweka Sahihi katika Maandishi ambapo pia Pamoja na Kulazimishwa hakupewa nafasi ya Kusoma Maelezo yake.. Alitishwa na Goodluck Minja na ASP Jumanne alimtishia Kwamba Asipoweka atateswa Kama alivyoteswa Moshi

Sababu ya 3 ni kwamba Maelezo yake yalirekodiwa Nje ya Muda, yalirekodiwa Siku ya Tarehe 09 August 2020 wakati amekamatwa 05 August 2020.

Sababu ya 4 ni kwamba Maelezo ya Onyo yalikuwa a yameandikwa kwa Sheria ya Kifungu 57((1) Ilivyofanyiwa Marejeo 2020 ambapo Sheria hiyo haipo

Sababu Nyingine NI kwamba alionywa kwa Sheria ya Kuzuia na Kupambama na Ugaidi wakati sheria hiyo haipo..

Sababu Nyingine NI Maelezo ambayo yanalengwa Kutolewa Mahakamani yapo Tofauti na yale Yaliyotolewa wakati wa Commital kwa Kutofautisha Subsection

Sababu ya Saba Hakuna Kifungu Kinachoonekana Kwamba wamechukua Maelezo na Kushitaki kwa kifungu kipi

Kutokana na Hoja zote Mbili zilizo letwa zilikuwa zinaangukia katika Sheria ya Ushahidi ambapo ilipelekea Kuwepo Kwa Kesi Ndogo

Kwa hiyo Mapingamizi hayo yalishughulikiwa kwa Njia ya Kuleta Hoja Mahakamani

Na Kwamba Baada ya Kesi Ndogo Submission ziletwe kwa Kuleta Hoja ya Kuunga Mkono kuhusu Mapingamizi Yanayo angukia Katika Sheria ya Ushahidi..

Jaji: Katika Kesi Ndogo Upande wa Mashtaka wenye Jukumu La Kuleta Mashahidi wa Kuthibitisha.. Walileta Mashahidi wanne..

ASP Jumanne
Goodluck Minja
ISSA Maulid
Msemwa

Na walileta Vielelezo, Barua ya Msajili Kama Kielelezo namba 1, Detention Register kama Kielelezo Namba 2 na Kielelezo namba 3

Jaji: Kwa Upande wa Utetezi walileta Mashahidi Watatu, Kielelezo Namba Moja Maelezo Ya GOODLUCK Minja, Nakala ya Hati ya Mashtaka , Dispatch Book, Nakala ya Hati ya Mashtaka ya Kesi namba 17/2020, Nakala ya Hati ya Mashtaka Ya Shahidi namba tatu kesi 63/2020 020

Na Kielelezo Kingine ni Diary ambayo Ulichukukiwa wakati WA shahidi Wa Mashtaka Anatoa Ushahidi Wake, Sababu Pande zote hawajazungumzia Kwa Kirefu Kielelezo Hiki basi na Mimi sitoongelea kwa akirefu Kielelezo Hiki, Mahakama haina Nia ya Kurejea Maelezo Ya Ushahidi wote

Jaji: Suala la Kutafuta Ukweli kwa Hoja namba Moja na Mbili na Hoja namba Tatu Mpaka namba Saba zilikuwa resolved Kwa submission zilizopangiwa parties Mahakamami... Ni Utaratibu wa Kawaida mambo yanayohusu Sheria Kuamuliwa kwanza..

Kwenda Kwenye Hoja za Kisheria si Sawa, Ni Vizuri kwenda Kwenye Hoja za Ushahidi Kwanza, Kwa sababu hiyo Tutaanza Mambo yanayuhusu Ushahidi kabla Mambo ya Kisheria..

Kwa Mujibu wa Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 Kifungu 57 (1) pale ambapo Utetezi wa Napinga Maelezo ni Wajibu wa Mashitaka Kuthibitisha, Pasipo Kuacha Shaka..

Kutokana na Ushahidi Wa shahidi namba Moja na Shahidi Nmab tatu ndiyo Waliokwepo Wakati Wa naandika Maelezo, Kwa Mujibu wa Ushahidi Wao walimkamata Mshtakiwa Huko Rau Madukani,

Kwamba Wakati wanawakamata Walikuwa na Mwenzao Moses Lijenje, Na Washitakiwa kwa ridhaa yao Waliongoza Zoezi la Kumtafuta Moses Lijenje Katika Maeneo ya Moshi na Wilaya ya Hai, Kwa amba Baada ya Kushindwa Kumpata Siku ya Tarehe 06 August 2020 Walianza Safari kuja Dar es Salaam

Jaji: Na wakiwa kabidhi Sehemu ya a Mapokezi na a Ada ya hapo waliondoka Kwenda Kufanya Usafi, Na Kwamba walipokelewa na DC Msemwa.. Na walirudi tena kumuhitaji Mshtakiwa Namba tatu Kuja Kumuandika maelezo..

Kwa ajili ya Kuandika Maelezo yake ya onyo na Kwamba Mshitakiwa Alitoa Maelezo yake kwa hiari yake,

Ushahidi Wake uliungwa Mkono na Shahidi namba Mbili, alieleza kwamba aliwapokea baada ya Washtakiwa Kufikishiwa Kwake na Kuwaingiza Kwenye Kumbukumbu ya DETENTION REGISTER..

Kwa Mujibu wa Ushahidi Huo yeye anashuhudia Kwapo Katika Kituo hicho, Anashuhudia kuwa pokea na Kumtoa tena kisha kumpokea tena Mshtakiwa Namba tatu.. Mshtakiwa namba tatu aliporudishwa alikuwa kwenye hali Nzuri

Na Shahidi namba Moja anaendelea Kusema Kwamba Baada ya Kumalizia Kumuandika Maelezo na Kumsomea kisha akamrudisha tena Mahabusu,

Jaji: Ushahidi huu ulipingwa na Upande Wa Utetezi ambapo Mshtakiwa Watatu alitoa Ushahidi Wake Kwamba hajawahi Kufika katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam..

Walipofikishwa Dar es Salaam Walifikia Kituo cha Polisi Tazara na Kupelekwa Mbweni

Ambapo alichukuliwa kwenye Chumba alichokuwepo Kupelekwa Chumba Kingine na kisha Kulazimishwa Kusaini Maelezo, Maelezo yoyote yanayosema Kwamba aliyatoa ni ya Uongo...

Akaendelea Kusema Kwamba Upande wa Mashtaka Umeshinda Kuthibitisha kwamba Msemwa alikuwepo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Siku hiyo...

Jaji: Hata alipoulizwa alishindwa Kusema aliwapokea zamu yake,

Shahidi wa Pili yeye alisema Kwamba alikamatwa huko Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro na Kuletwa Kituo Cha Polisi Oysterbay alimkuta Msemwa

Na Kwamba Kwa Sababu hakuwa amekula alimuagiza Afande Msemwa akamchukulie Chakula na Akaendelea Kuwa Rafiki ya Afande Msemwa..

Na Kwamba hata Baada ya Kupelekwa Mahakamani alirudishwa tena Kituo cha Polisi Oysterbay kwa Siku 19..

Kwa muda wote huo si kweli Kwamba Msemwa alikuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, Na Kwamba alipokuwa alifuatilia Kesi aligundua Kuwa Msemwa aliongopea Mahakamani Kwamba alikuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Aliwasilina na Wakili Wake kisha anapewa Utaratibu Wa a kupata Nyaraka Kwa ajili ya kuzileta Mahakamani, Alipozileta Upande wa Mashtaka Walipinga lakini Mahakama Inaona ni Busara Kuzipokea..

Jaji: Upande wa Utetezi Wakamleta tena Shahidi Wa tatu, Bwana Mhina ambaye alikamatwa huko Kwao Tabora..

Na wakati wote huko alikuwa anaulizwa kama anamfahamu Mshtakiwa namba Nne na Mshtakiwa Namba tatu..

Ambapo yeye alisema Kwamba alifanya naye kazi wakati fulani, Pamoja na Kuwaeleza Ukweli lakini waliendelea kumshikilia, Na Baadae Kashtakiwa na Kupelekwa Gerezani ambapo Alikutana na Mshtakiwa Namba tatu..

Akasema Kwamba Kwenye Hati ya Mashtaka palikuwa Pameandikwa Majina ya Washitakiwa na pembeni Gereza aliokuwa anashikiliwa.. Yeye alikuwa anashikiliwa na Mshtakiwa Namba tatu Segerea

Kwa Upande wa Utetezi walionyesha Kwamba Kwa namna gani Mshtakiwa namba tatu hakuwepo Kituo cha Polisi na Upande Wa Mashtaka walikuwa wanaonyesha Kwamba alikuwepo Kituo cha Polisi...

Jaji: Kama nilivyosema Mwanzo Upande wa Mashtaka ndiyo wanalo Jukumu la Kuthibitisha Pasipo Kuacha Shaka, Mzigo Wa uthibitishaji wa Shauri kutoka Upande Wa Mashtaka, Upande wa Utetezi Kazi yake Kubwa ni Kuonyesha mashaka ambayo yanaweza Kuwa Resolved Kwa Favour ya Mshtakiwa

Hii ni Kwa Sheria Kesi ya JOSEPH Vs JAMHURI Kesi 44 ya 1986, Jambo la Msingi Mshitakiwa Alikuwa wapi, Upande wa Mashtaka Wanasema Mshitakiwa namba tatu alikuwa katika kituoa cha Polisi Kati Dar es Salaam..

Kwa Kuleta Detention Register Kuonyesha alifika a Kituo cha Central Police, Shahidi Namba Mbili anasema Kwamba alimpokea Mshitakiwa na Kumuongoza Kwenye Kielelezo Namba 2 cha Detention Register, Kwa Msingi huo wao Ndiyo Ushahidi Wao

Jaji: Upande wa Utetezi Wao Wana kana na Ushahidi Wa kukana Umejengwa Kwa a Shahidi Namba Moja na Shahidi namba tatu, Kwamba Ushahidi Waliotoa haujaungwa Mkono na Maelezo yoyote Kwamba Kweli walikuwa Kwenye Kituo Cha Polisi Kati Dar es Salaam

Kwa uoande Wa Utetezi Wa naomba Kwa Mujibu is a PGO namba 284(4,5,6) kwa kusokekana kwa Occurance Book Kuonyesha Ni kweli Kwamba Msemwa Alikwepo kazini Siku hiyo, Hakuna Ushahidi Wa Polisi Incharge pia..

Wakaendelea Kusema hata shahidi namba Mbili alipoulizwa Maswali alishindwa Kuwataja aliwapokea zamu na hata waliompokea, Kinyume na Station Diary ambapo inatakiwa Kuonyesha Matukio yote..

Hata Kielelezo namba 2 kina Mapungufu kwa a Kutolewa kwake Kilipokuwa huko Polisi, Kwa sababu hiyo Mahakama a inatakiwa Ione Mashaka Kwamba hakija kidhi..... Kwa Kesi ya ISAYA Vs JAMHURI 115 ya Mwaka 2019

Jaji: Upande Wa Utetezi Walihitimisha Kwa Kuomba Mahakama Itizame Kwa PGO 353 Kwamba Mshitakiwa Anapo fikishwa Kituoni anatakiwa aapelekwa Kwa Daktari, Jambo ambalo lingefanyika lingeonyesha kweli Kama Mshtakiwa Namba 3 hakuteswa.

Kwa Ushahidi Ulitolewa na Shahidi namba 03, na Kwamba Walipo kutana Mahakamani na Gerezani aliambiwa na Mshitakiwa Namba tatu Kwamba Haku fikishwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Bali Tazara

Wakati napokea Vielelezo nikisema Mwisho nitaangalia na Kuona Kwamba Vielelezo hivyo ni Relevant, Niliombwa Kuangalia Kielelezo namba Mbili, Mahakama Ichunguze Ione kwamba Hapakuwa na Muunganiko Wa Kielelezo hicho na Swala la Kielelezo Kimetolewaje Mahakamani

Jaji: Ikumbukwe Kwamba Kielelezo Hiki kilisha pokelewa na Jaji Siyani Na Fikiri siyo Sawa Kuangalia Kielelezo Hicho tena Wakati Kielelezo Hicho Kilishatolewa Uamuzi wa Mahakama.. Kwa sababu hiyo Mahakama inatupilia mbali Hoja hiyo..

Kuhusiana na Hoja namba Tatu Kwamba Mshtakiwa Alikuwepo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam..

Inahusu Mashahidi Namba Moja na namba Mbili.. Namba Moja anasema Walipo toka Moshi walifika Moja kwa Moja Polisi Kati Dar es Salaam,

Na Wanaonyesha Kwamba jina la Mshtakiwa Namba tatu lipo kwenye Detention Register, Ushahidi Unaonyesha Kwamba Mshtakiwa aliingizwa Kwenye Kituo hicho.. Na Kwamba alitolewa kwa ajili ya Upelelezi..

Jaji: Swali ambalo Mahakama Inajiuliza ni Je ni Ushahidi Wa Kuaminika? Mahakama Inatizama Ushahidi huo kama Ushahidi unapaswa Kuungwa mkono.. Mahakama Katika aina ya Ushahidi unapaswa Kuungwa Mkono, Mahakama Inaona Ushahidi Unatolewa Chini ya Kiapo unapaswa Kuungwa Mkono

Kwa Mujibu wa Kesi Mvumi Mpenda Vs JAMHURI 327 ya 2016, Na Maelezo ya Marehemu wakati anafariki, Maelezo Ya Mtoto pia.. Sheria Kesi ya Frank Joseph Vs JAMHURI.. Ushahidi ambao imebase kwa Habari ya Kusikia Unatakiwa Kuungwa Mkono

Ukiangalia aina ya Ushahidi wa a Kuungwa Mkono Utaona Ushahidi Wa Shahidi namba 2 hauangukii katika Miongoni Mwa Ushahidi niliotaja, Kwa maelezo Kwamba alipofika Polisi alimkuta Shahidi Wa Pili

Mahakama Inaona Kwamba Pamoja na Kwamba Ushahidi Wa shahidi namba Mbili siyo wa Kuungwa Mkono, Basi Ushahidi Wake unaungwa Mkono na Shahidi namba Mbili..

Jaji: Kama ilivyo Kwenye kesi ya Goodluck KYANDO Vs JAMHURI ni Ushahidi ambao Unaaminika.. Kama nilivyosema Kwamba Upande wa Utetezi Jukumu lao ni Kuonyesha mashaka.. Ilikusudi waweze Kuleta Mashaka, Walitakiwa watengeneze Mashaka..

Shahidi Namba 1 Mbaye ni Mshtakiwa namba tatu anapo Sema kwamba Alikuwa Kituo cha Polisi Tazara Ndiyo Mashaka Yenyewe, Mujibu wa Sheria Jukumu la Kuthibitisha Jambo lolote ambalo Mtu a alisema inakuwa Kwake yeye labda Kwa Mujibu wa Sheria it atakiwa itihibitishwe na Mtu Mwingine

Kwa sababu hiyo Basi Mshtakiwa Alikuwa na Jukumu la Kuonyesha ni Kweli alikuwa Kituo Cha Tazara, Mzigo Huo unakuwa Mwepesi Kwake..

Wakati anapitia Ushahidi Kuhusiana na Jambo hili, Ambapo Mshtakiwa alisema Kwamba alikuwa katika kituo cha Tazara yeye na Mshtakiwa Namba Mbili

Kumbe alikuwa na Mtu aliyemuona Akiwa Kwenye Kituo cha Tazara lakini Kwa Bahati Mbaya Mshtakiwa namba tatu ameshindwa Kumuita Shahidi huyo Kutoa Ushahidi Wake Mahakamani..

Badala yake alimuita shahidi namba tatu ambaye anasema alipofika Kituo Cha Tazara Hakumkuta Kituo cha Polisi Tazara.. Lakini pia katika Ushahidi Wake Mshtakiwa Namba tatu Haikuelezea..

Jaji: Shahidi namba 3 kwa kutumia Kielelezo ambacho ni Hati ya Mashitaka ambayo inaonyesha Jina Mshtakiwa na Gereza alikuwemo.. Kwa Kuzingatia Hati hiyo Hakuna Sehemu Inayoonyesha Kwamba Walikwepo Katika Germany za la Segerea

Basi Mahakama inatilia Mashaka Ushahidi huo..

Shahidi huyo namba tatu alikabidhiwa Detention Register Ya Tazara alisema Jina lake halikwemo na Pia Jina la Mshitakiwa Namba tatu hakuwepo Katika Detention Register..

Kwa sababu Hiyo Mahakama Unapata Mashaka Kwamba Mshtakiwa namba tatu alikuwepo Kituo cha Polisi Tazara..

Na Shahidi Wa Pili alisema Kwamba Hapakuwa na Uwezekano Kwamba Msemwa alikuwa anafanya Kazi Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Na Kwa Maelezo hayo alileta Vielelezo ambapo ni Dispatch, Hati ya Mashitaka na Vingine, Ukitazama Vielelezo Vyote hivyo Hakuna Uhusiano wa Moja kwa Moja Na Kesi iliyopo Mahakamani.. Na Kwamba Mahakama Inaona Kwamba Vielelezo hivi haiwezi Kuisaidia Mahakama..

Jaji: Wote waliokuja kuzungumza wamejichanganya..

Na Juu ya maslahi kwamba ni shahidi mwenye maslahi, Ni kweli amesema kwamba amekuwa haridhiki kuanzia Kesi mpaka Kwa Jaji mwenyewe.... Mahakama inaona yeye ni Shahidi wa hisia ambaye amekuja mahakamani kutoa hisia zake

Jaji: Kwa Upande wa Mashtaka waliweza Kueleza Kwamba Shahidi Alikuwa ni Shahidi Mwenye Maslahi.. Kwamba Katika Ushahidi Wake ulikuwa wenye Kujikanganya, Hasa pale Aliposema Kwamba alimuelekeza DC Msemwa akachukue Fedha katika PPR yake Wakati Alisha Sema alipokamatwa hakuwa na Kitu chochote huko Mwanga.. Na hakutoa PPR yake hapa Mahakamani, na Hivyo ni Ushahidi Wenye Kujikanganya.. Mara ya Kwanza alisema Kwamba alitambua DC Msemwa Baada ya Kusoma Jina Lake Katika Uniform na alipoulizwa mara ya Pili alisema Kwamba alitambua anmab yake H4323

Alishindwa Kuoanisha Jina namba aliyo Sema Mara ya Pili, Kushindwa Kuonyesha Wajihi Wa DC Msemwa.. Alishindwa Kutoa Discription Nzuri ya Shahidi Huyo, Mwanzo alisema Kwamba ni Mweusi na Mnene na alipoulizwa tena akasema Kwamba anaweza Kuwa Mnene au Siyo Mnene

Mahakama ya Rufaa Iliyoketi huko Arusha inasema Kwamba Siyo Kila Mkanganyiko unafanya Mahakama Isiamini Ushahidi Huo, Mahakama Inajiuliza Kwamba Je Mkanganyiko huo ni Mkanganyiko wa Kawaida ambao Mahakama Inapaswa Kuupuuza..?

Mahakama Inaangaliwa Kuhusu Maelezo Yaliyotolewa, Katika Mazingira hayo Ukiangalia Contradiction ni Contradiction siyo Nyepesi kwa sababu hiyo Basi Mahakama inatilia Mashaka Ushahidi Wake.. Ni wazi Pia Ushahidi Unaotakiwa Kutengeneza Mashaka hautakiwi wenyewe Kutiliwa Mashaka

Jaji: Ushahidi Unatolewa ni Kuhusu Tarehe 14 May 2020 Wakati Jambo Linalobishaniwa hapa ni 07 August 2020.. Labda kama Ingekuwa shahidi huyo Alikuwapo Oysterbay Siku ya Tarehe 07 August 2020, Katika Mazingira hayo Mahakama Inaona Value yake ni ziro na haiwezi KuSaidia Mahakama

Jaji: Mahakama Inaona Kwamba Kuhusiana na Ushahidi Alikuwepo Kituo cha Polisi Oysterbay wakati Mshtakiwa namba tatu alikuwa Tazara, Mahakama Inaona kwamba Ushahidi Ulioletwa na Upande wa Mashtaka haujaweza Kutikiswa..

Na Kwa sababu Hiyo Pingamizi la Kwanza Kwamba Mshtakiwa hakuwepo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam siyo la Msingi na Mahakama inatupilia Mbali,

Jaji: Kwa Maana hiyo sasa Kwamba Mshitakiwa namba tatu aliteswa na Alilazimishwa Kuweka Sahihi yake na Kwamba aliweka Sahihi yake baada ya ASP Jumanne Kumtishia Kwamba angeteswa kama alivyoteswa Moshi, Na Kwa namna ambayo alikuwa ametishwa hakupewa Kusaini...

Ikumbukwe Kwamba Maelezo Yanayibishaniwa no Yale Yaliyotolewa alipokuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, Upande wa Mashitaka unapaswa Kuthibitisha Kwamba Hapakwepo na Mateso, Na Kwa sababu Ya Upande Wa Mashitaka Ulikuwa Jukumu hilo..

Wao wanasema Mshitakiwa Namba tatu hakuteswa na Kwamba Wao Tarehe 08 August 2020 Walipo wa kabidhi Washitakiwa Mbweni hawakurudi tena, Na Kwa Mujibu ya Maelezo Yao, Maelezo ambayo anataka ni yale aliyotatoa akiwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Jaji: Kwamba Mshitakiwa aliteswa Na Goodluck na Mahita kwa kuulizwa Maswali Juu ya Uhusiano Wake na Mshtakiwa Namba 4... Mshitakiwa anasema walimuuliza Maswali Mengi na walikuwa wanamrekodi na Baada ya hapo Walimpeleka Kituo cha Mbweni

Kitu ambacho Upande wa Mashitaka Unapinga, Wakati wa Ushahidi Wake Hakusema Alivyoteswa na alivyotishwa akiwa Kituo cha Polisi Mbweni.. Kwa maelezo yake yeye Kwamba alifikishwa Mbweni akitokea Kituo cha Polisi Tazara..

Na Kwamba Siku ya Tarehe 10 Walimpeleka Kwenye Ofisi ya Upelelezi ambapo Jumanne na Goodluck Ndiyo walimtishia.. Na Kwamba alipokuwa amekaa aligeuka akamuona Goodluck akiwa na Pistol na Kumwambia Kwamba Asipo Saini watamfanya kama Moshi

Jaji: Upande wa Utetezi hujaeleza Kwa Namna gani Upande wa Mashtaka Umeshindwa Kuthibitisha Kwamba hakuteswa.. Wakaomba Pia Mahakama Kujikimbusha PGO 353 (2) kwamba Mshitakiwa anatakiwa aku fikishwa kwa Daktari, hiyo ingeondoa Mashaka kama Mshtakiwa hajateswa

Kwa Sababu hiyo Basi Upande wa Utetezi Wakaomba Mahakama Ione kwamba Mshitakiwa alitishwa, Mahakama inalo jukumu la Kuangalia Ushahidi Wa Mtu Mmoja Mmoja na Maelezo ya Mshtakiwa..

Kwa Ushahidi Wa Mshtakiwa namba tatu Kwamba alitshwa alipokuwa Kituo cha Polisi Mbweni na Kwamba Kama Asipo Saini Mateso ya Moshi yatajirudia, Kwa sababu hiyo Maelezo yanayopaswa Kutolewa yeye hayatambui..

Wakati anatoa Ushahidi Wake, Wakili Wa Serikali Alimuuliza ni Kweli Kwamba Yeye alitshwa Tarehe 08 August 2020, Akauliza Je Kama Adamoo alitolewa tarehe 09 August 2020.. Akasema hajui itakuwaje..

Jaji: Hoja za Mawakili Zina onyesha Kwamba Shahidi Aliteswa Tarehe 09 August 2020, Na Kwamba Hoja ya tatu Ya Maelezo Yaliandikwa Nje ya amuda wao Wameandika tarehe 09 August 2020,

Ni wazi pale panapokiwa na Ushahidi Unapingana na Submission ni wazi Ushahidi unapaswa uaminike kwa sababu Submission ni Ufafanuzi wa Ushahidi, Katika Mazingira hayo Mahakama inarejea Maaamuzi yake wakati ina' resolve Mgogoro wa kwanza

Mahakama imeshindwa Ku' examine ni Tarehe gani Mshtakiwa aliteswa, Kwa sababu hiyo Basi Mahakama inabakia na Mkanganyiko

Jaji: Na Kwa PGO ya 353 ya Kuhusu Kumpeleka Shahidi Kwa Daktari haiwezi Kusaidia Kwa sababu Mahakama ipo Kwemye Dilemma. Mahakama Inaona Sababu ya 2 ya Pingamizi Inaona Upande Wa Utetezi Umeshindwa Kujenga Vizuri na Kwa sababu hiyo Mahakama ina overule na Kutupa Pingamizi hilo

Jaji: Nakuja sasa Kwenye Hoja za Kisheria Kwamba Maelezo yalichukuliwa Nje ya Muda.. Mahakama Inakubaliana Kwamba Mshtakiwa Alikamatwa Tarehe 05 August 2020 na Kwamba Maelezo Yalichukuliwa Tarehe 07 August 2020

Mahakama Inarejea Sheria Kwamba Maelezo Yanatakiwa Kuchukuliwa ndani ya masaa Manne, Na Kwamba Kinyume na hapo panapaswa kuwa na Kibali Maalum, Ni kweli Maelezo hayo yameandikwa Nje ya Muda wa Zaidi ya Masaa 40

Lakini Kifungu kichofuata kinasema Kwamba pale ambapo Mshitakiwa anakuwa amekamatwa na Taratibu Za Kiupelelezi zinaendelea basi Muda huo unapaswa uondolewe..

Kwa maelezo Kwamba Walikuwa na Moses Lijenje na Kwamba Haku kamatwa, Walitumia Siku iliyibakia ya a tarehe 05 August 2020 Walitumia Muda uliobakia Kumtafuta Moses Lijenje..

Na Kesho Yake waliendelea Kumtafuta sehemu Mbalimbali

Kwa Kubase Kwenye Ushahidi Huo Wa Upande wa Mashitaka, Upande Wa Utetezi walieleza Kwamba Yapo Mapungufu Mengi yamaonekana.. Wanasema Maelezo hayo hayaonyeshi Kwamba palikuwa na Katazo Kutoka kwa DCI kuwa fanya Wasiandike maelezo hayo Hapo Moshi..

Kwamba Zoezi La Kumtafuta Lijenje Lilijawa na Mapungufu Mengi.. Wakaomba Mahakama Izingatie Hoja zao Kwa Kutumia Kesi zifuatazo, DPP Vs James, Massa we Vs JAMHURI, Aphonce Vs JAMHURI, Hamis Chuma Vs JAMHURI

Jaji: Kwa Askari Wanaojua kazi zao asingeweza Kurelax na Kukaa bila Kumtafuta Mshtakiwa Wa tatu.. Ni wazi Kwa Upande Wa Mashitaka Ushahidi Wao Hautakiwi Kutiliwa shaka.. Ni wazi Pia Upande Wa Utetezi Wameeleza Kwamba Kifungu 50(1) ni wazi ilitumgwa kwa uwezekano wa Kuondoshwa

kwa Kuteswa kwa Washtakiwa.. Katika hali hiyo ni wazi Kwamba, Kwa Hoja ya Upande wa Utetezi Ushahidi Unatolewa na Upande Wa Mashitaka Hakuna al Mashiko kwa Kutengeneza Mashaka..

Pamoja na Hoja zao hizo za Utetezi , lakini ni wazi Kwamba Ushahidi huo wa Mashitaka Umeletwa Kwa Uzito wake siyo wa Kupuuza, Mahakama unapokuwa inataka Kuyapa Uzito Maelezo Hayo Mahakama Inapaswa kungalia Mazingira yote..

Kwa Maoni yangu hatua tuliyopo ni Hatua Ya Kupokea Maelezo Ya Onyo, Mahakama Haiwezi Kuzungumzia Uzito wake, Hoja ya Kwamba Mahakama Ione Uzito wa Maelezo Yenyewe Mahakama Inaona Imeletwa Kabla ya Wakati,

Kesi mbalimbali zinasisitiza Kwamba Yakiwepo Maelezo Ya Kutosha Yanayao Onyesha Kama a palikuwa na Sababu ya Kutosha Kuandaa Maelezo Basi Sababu hiyo inatosha Kupokea Maelezo Hayo, Maelezo ya a kwamba Shauri lilikuwa limegumguliwa Dar es Salaam basi palikuwa na Sababu ya Msingi Maelezo Kuyachukulia Dar es Salaam, Kuwasafirisha Washitakiwa Kutoka Sehemu Moja Kwenda Nyingine Mahakama Inamaoni Kwamba Kwa Namna Maelezo Yaliyotolewa, Mahakama Inaona Katika Mazingira haya ilikuwa ni sahihi itumike

Kwa sababu hiyo Pingamizi la Tatu natupilia Mbali

Jaji: Kwa Pingamizi la Tano pia Kuhusu Subsection na kunukuu Sheria ambayo haipo, Katika Kukosea kutaja Sheria, Hakufanyi Nyaraka Kukataliwa Mahakamani..

Katika Maamuzi Hayo nimezingatia Kesi ya JAMES NA SONGOROKA basi Kwa Namna hiyo pia natupilia Mbali Pingamizi hilo.

Jaji: Kwamba Kwa sasa Mahakama Ya Rufani imekuwa Unachukua Msimamo Tofauti, Kwamba Unapokuwa Umwrejea tofauti Sheria Kwamba Jambo hilo aliwezi Kupokelewa, Kesi Ya JAMES MWAMULE na SYKES Mahakama Inaona Kwamba Kurejea Kimakosa Kwenye Verification kumeathiri Haki ya Mshitakiwa kwa namna gani, Basi Kwa Sababu hiyo natupilia Mbali Pingamizi hilo..

Jaji: Kwamba Kwa sasa Mahakama Ya Rufani imekuwa Unachukua Msimamo Tofauti, Kwamba Unapokuwa Umwrejea tofauti Sheria Kwamba Jambo hilo aliwezi Kupokelewa, Kesi Ya JAMES MWAMULE na SYKES Mahakama Inaona Kwamba Kurejea Kimakosa Kwenye Verification kumeathiri Haki ya Mshitakiwa kwa namna gani, Basi Kwa Sababu hiyo natupilia Mbali Pingamizi hilo.

Jaji: Hoja ya Saba Ni kwamba Katika Kifungu cha 57 Mshitakiwa anapokuwa ameonyesha Kukiri anatakiwa kuonywa Upya, Na anapokuwa ameonywa basi Hapo Ndipo Maelezo Yanatakiwa Kuandikwa, Ni wazi Kwa Kungalia hilo aionyeshi Mshitakiwa Alihojiwa kwa Kufuata taratibu gani kati ya hizo 2.

Niseme Jambo hilo na Hoja hii Pamoja na Kwamba Ilikuwa a raised Mwanzo, Mawakili wamesema kwamba hawajazungumza.. Kwa Maana hiyo Mahakama inapata Benefit ya pekee kutoka kwa Upande wa Mashitaka.. Pamoja na Kwamba Hoja hiyo haijaelezwa na Upande Wa Utetezi lakini Mahakama ameona ni Vema Ipitie Hoja hiyo.. Kinachotakiwa ni Format tu na siyo Kifungu Kipi Kimetumika.. Kwa hiyo iwe Kwa Kifungu cha 51 au 57 kwa Kufuata Utaratibu huo Kama. Hakuna Maelezo Ya Mshtakiwa alivyoathirika.. Mahakama Inaona Hoja ya Saba haina Mashiko na naitupilia mbali.

Jaji: Hoja zote saba hazina mashiko na hasa kwenye kesi ndogo ushahidi ulioletwa na upande Wa mashtaka umeshindwa Kutingishwa... Kwa sababu hiyo Basi mapingamizi yote nayatupilia mbali..

NATOA AMRI!

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Utoe Amri tuweze Kurejeshewa Kielelezo Ambacho ni Dispatch..

Jaji: na Hivi Vingine..?

Wakili Peter Kibatala: vibakie, kwa sababu Vinaweza Kutumika hata Mahakama ya Rufaa huko Mbeleni ila hiki Kinatumika na Ofisi.
ni uhujumu uchumi au ugaidi?
 
Hivi jaji anapoandaa hukumu huwa anashirikiana na mawakili wa serikali ?.Watu tangu mwanzo walisema huyu jaji pamoja na wale wengine wawili ambao walianza na kesi hii walikuwa tayari wanayo hukumu kinachosubiriwa ni muda tu.
 
tupa kule upuuzi mtupu!
wacheni kesi ingurume.
mapingamizi ya kipuuuzi tupa kule, takataka.
 
Lissu mwanasheria nguli rudi home umupambanie Mwenyekiti.

Au umeamua kumutosa baada ya kuona jinsi Mahakama inatenda haki,kama ilivyokufutia kesi zako?
Na wewe unajua mengi kwenye chama hata yale maandamano unajua vema lengo lake,japo hukutokea.
Sasa kama mnasema Tayari jaji anayo hukumu mfukoni,hata huyo Lisu atabadilisha nini?
 
Unajua tunaweza kuongea kwa ushabiki na hisia tu! Ila watu wakumbuke Mbowe anamakandokando pia ya kuhusika na kifo cha Chacha Wangwe! Usimwamini mwanadamu huwezi kujua alivyo ndani yake! Mahakama waiache iwe huru kama kwa Sabaya!

..watoto wa Chacha wangwe ni wanaharakati na wanachama wa Chadema.

..mbowe angekuwa amemdhuru Baba yao / Chacha Wangwe, watoto wake wasingeunga mkono Chadema.

 
Hivi jaji anapoandaa hukumu huwa anashirikiana na mawakili wa serikali ?.Watu tangu mwanzo walisema huyu jaji pamoja na wale wengine wawili ambao walianza na kesi hii walikuwa tayari wanayo hukumu kinachosubiriwa ni muda tu.
Inasemekana anashirikiana na uvccm kuandika hukumu.so pata picha
 
..haya maamuzi ni MABAYA sana kwa upande wa washtakiwa.

..mimi sio mwanasheria, lakini ktk kusoma maamuzi ya leo, naona kama Jaji ameamua kwamba washtakiwa wana HATIA.

..hisia zangu ni kwamba, maamuzi ya mwisho ktk kesi hii yatafanana zaidi na maamuzi yaliyotolewa leo.

CC Nguruvi3
Uko sahihi. Mimi pia naona muelekeo ni huo.
 
Kibatala na wenzake inabidi wachague kati ya kuwa mawakili au kuwa wachekeshaji wa wanaohudhuria mahakamani. Wachague ama kuwahudumia wateja wao au wasio na kazi wanashinda mahakamani kupitisha mda.
 
Tuliaminishwa humu kibatala ndiye wakili bora kabisa hapa nchini kwa sasa?
Mbona anagaragazwa hivi sasa na wakina Wakili Kidando?
 
Kwa hiyo ndugu Jaji, unaapa kwa Muumba wako wa mbingu na nchi kwamba :-
1. Mashahidi hawakuteswa na kudhalilishwa utu wao.
2. Ukamataji ulifuata sheria za Jeshi la Police yaani GPO.
3. Maelezo yalichukkuliwa ndani ya muda wa kisheria
4. Meelezo yao waliandika kwa hiari yao wenyewe bila kutishwa wala kushurutiswa
5. Jumanne alikuwa Central na muda huo huo akawa O'bay police stations.

Sawa bwana JAJI - Hakimu wa misho hapa duniani ni mwenyezi MUNGU endelea kuketi kwenye kiti chako kuumiza wasio na hatia - kumbuka wote hao wana familia kama ya kwako, na hizo familia zao zinatoka machozi na katika ulimwengu wa kiroho yanakuwa juu yako wewe binafsi.

Mungu akubariki sana na akupe afya njema ili uendelee kuhukumu vizuri.

Acha mahubiri. Sheria ifuate mkondo.
 
Sidhani Kama atatoboa huyu mtu,maana mawakili wake unaweza sema waliishia ngumbaru[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
mawakili wa Mbowe wanapoteza na kuchezea muda wa Mahakama kwa kuleta mapingamizi yasiyo na kichwa wala miguuu ambayo kimsingi yana chelewesha haki kutendeka.

Wanajua wanacho kifanya ila mahakama isikubali kuchezewa.

Leo hii Katibu mkuu wa chadema John Mnyika ana mkejeli na kumdhihaki Jaji anaye sikiliza kesi hiyo je ni sawa hiyo?!

Mnyika na genge lake la kihuni wana lengo la kuichafua mahakama na Majaji, hilo lisifumbiwe macho,.hatua za kisheria zichukuliwe.
 
Kibatala na wenzake inabidi wachague kati ya kuwa mawakili au kuwa wachekeshaji wa wanaohudhuria mahakamani. Wachague ama kuwahudumia wateja wao au wasio na kazi wanashinda mahakamani kutipisha mda
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom