Maharage Chande aondolewa TANESCO, apelekwa TTCL. Gerson Msigwa awa Katibu Mkuu Wizara ya Michezo
Ukweli ni huu,lakini wañaukwepa:
1.Wanasiasa kwa kushirikiana na wafanyabiashara wanaumiza shirika.
2.Mikataba mibovu iliyoshinikizwa kwa maelekezo ya wanasiasa inainyonya shirika.
3.Kuwepo makampuni yanayouza umeme wa jenereta kwa Tanesco ni mtihani ambao haujapatiwa majibu mpaka leo!
4.Mahitaji ya umeme yanajulikana iweje upungufu usifanyiwe kazi mapema kuondoa adha ya mgao wa umeme.
5.Miradi ya uzalishaji umeme isiyoisha,ni njama ya kufanikisha biashara wauzaji umeme wa dhatura wamajenereta kwa Tanesco.
6.Mkakati wa kubaini hujuma,kukabiliana na upungufu unaosemwa kila siku upo wapi?
Well said Mkuu. Hizi ndizo analysis zinatakiwa na si kushangilia tu. Yaani mambo ni mengi. Nchi inaliwa mkuu. Ila saa ninajiuliza ule uzalendo wa Usalama wa Taifa upo tena? Ni kama vile Taifa linajiendesha visivyo kabisa. Je mkuu wa nchi kama nahodha mkuu naye anapata support ya kutosha kutoka key state apparatus? Hapo tumwachie ngoswe. I am out Zogwale
 
Muhongo na umeme wa Zero tarrif, unapata units 75 Kwa Elfu tisa tu.

Muhongo alitisha sana.
Ndiyo maana ninasema Muhongo arudishwe Nishati. Alipokuwepo kila kitu kilinyooka mpaka customer service 24 hours. Yaani tulisahau Shida ya umeme. Yaani awe permanent Minister kwenye hii Wizara kizungumkuti.
 
Hivi maharage ni mtoto wa Mohamed Chande Othman???
Maharage Chande ni mtoto wa Mzee Maharage Chande (baba yake aliitwa Maharage Juma Chande) wa Tanga na mtaa wa Kalenga, Upanga Dar es salaam.

Huyu Mzee Maharage Juma Chande aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga enzi za Nyerere.

Kaka yake Maharage Chande ni Balozi Mohamed Maharage Juma, alikuwa balozi UAE na Mkuu wa Itifaki.

Ukitaka kujua vizuri habari za kina Maharage mtafute Mzee Muhamed Said
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na utenguzi wa Viongozi mbalimbali kama ifuatavyo:
  1. Amemteua Ndugu Said Othman Yakubu kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Yakubu alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
  2. Amemteua Ndugu Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
    Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huo, Ndugu Msigwa alikuwa Mkurugenzi wa Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali. Nafasi
    iliyoachwa wazi ya Mkurugenzi wa Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali itatangazwa baadae.
MAKATIBU TAWALA MKOA
  1. Ametengua uteuzi wa Ndugu Abdallah Mohamed Malela, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara. Badala yake amemteua Bi. Bahati Ibrahim Geuzye kuwa katibu Tawala Mkoa wa Mtwara. Kabla ya uteuzi huu, Bi Bahati alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
  2. Amemteua Ndugu Mohamed Jumanne Gombati kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Geita. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Gombati alikuwa Mkurugenzi Msaidizi
    Sehemu ya Maafisa Waandamizi katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
WAKUU WA TAASISI
  1. Amemteua Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Aidha aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Bw. Omar Issa ataendelea na majukumu mengine aliyopangiwa katika Ofisi ya Rais - Tume ya Mipango.
  2. Amemteua Ndugu Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Chande alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
    Anachukua nafasi ya Mhandisi Peter R. Ulanga ambaye atapangiwa kazi nyingine.
  3. Amemteua Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Kabla ya uteuzi huu Ndugu Nyamo - Hanga aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
  4. Amemteua Dkt. Erasmus Fabian Kipesha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Kipesha alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (TEA).
WAKUU WA WILAYA
  1. Ametengua uteuzi wa Ndugu Hanafi Msabaha, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini na badala yake amemteua Bi. Mwanahamisi Mkunda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini. Kabla ya uteuzi huo Bi. Mkunda aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.
  2. Amemteua Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Mariam Chaurembo atapangiwa kazi nyingine.
WAKURUGENZI WATENDAJI WA HALMASHAURI (MA -DED)
  1. Amemteua Ndugu Hassan Bakari Nyange kuwa Mkurugenzi (DED) wa Mtwara TC. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Nyange alikuwa DAS Wilaya ya Namtumbo. Aidha, aliyekuwa Mkurugenzi (DED) wa Wilaya ya Mtwara TC, Kanali Emmanuel Mwaigobeko atapangiwa kazi nyingine.
  2. Ametengua uteuzi wa Bi. Tatu Said Issike, Mkurugenzi wa Mtwara DC na kumteua Ndugu Abeid Abeid Kafunda kuwa Mkurugenzi (DED) wa Mtwara DC. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Kafunda alikuwa Mwanasheria katika Ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali.
  3. Amemteua Ndugu Reuben Sixbert Jichabu kuwa Mkurugenzi (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndugu Erica Yegella atapangiwa kazi nyingine.
KATIBU TAWALA WILAYA
Amemteua Ndugu Francis George Mgoloka kuwa Katibu Tawala wa Wilaya
(DAS) ya Namtumbo. Kabla ya uteuzi huo Ndugu Mgoloka alikuwa Katibu Tarafa Mswaki - Kilindi Handeni.

Katibu Mkuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wataapishwa siku ya Jumanne saa sita mchana Ikulu, Dar es Salaam.
View attachment 2759138
View attachment 2759139
View attachment 2759157
Msigwa anajiona ameula mpaka anaandika kunshukuru Hangaya kumteua bila kujua hapo ameanza kutumbuliwa na mwisho wa siku tuhuma zote sasa zitamhusu hatimaye kutenguliwa mazima sijui atarudi TBC au ITV haijulikani.

Tabia ya kutetea uongo anatakiwa kuiacha ili alinde heshima yake
 
Hakuna umeme! Huo ni ushahidi tosha
kadakayikreationsshsikioziba-jpeg.2751314
 
WAKUU WA TAASISI
  1. Amemteua Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

18 December 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, ambapo meja jenerali Paul Kisesa Simuli sasa kuwa balozi wa Tanzania nchini Uganda


View: https://m.youtube.com/watch?v=nRngrmkf3Kg

1702959412396.png

Picha: meja jenerali Paul Kisesa Simuli
 
Back
Top Bottom