Ni kweli inatakiwa akashughulikie umeme na siyo kukaa mezani. Ni muda wa kwenda kukaa na watumishi wote kuhakikisha kuwa watanzania wanapata umeme. Watanzania wanataka umeme waendelee na shughuli zao za uchumi, kuendelea kukaa kwenye vikao badala ya kwenda kuumiza kichwa ya namna ya kulipatia Taifa umeme ni sawa na kuwatia umaskini Watanzania,Ni sawa na kuwarudisha nyuma wajasiriamali,Ni sawa na kukwamisha uzalishaji viwandani na hivyo kupelekea upungufu wa bidhaa na hivyo kupanda kwa Bei kwa Bidhaa na hivyo kumuumiza mwananchi. Ni kweli inamoasa aende akashughulikie suala la umeme ili kuliondoa Taifa na Taharuki ya umeme,ni kweli aende akashughulikie umeme ili watu wasipate hasara ya kuharibika kwa bidhaa zao kama vile samaki wabichi kwa kukosekana kwa umeme. Inatakiwa aende akakune kichwa ili watu wapate umeme.
Mh Rais anataka wananchi wake wanaompenda na kumuunga mkono kwa mamilioni yao wapate umeme wa uhakika,.hivyo anapaswa kwenda kuweka mipango ya kuhakikisha umeme unapatikana kwa njia yoyote ile. Ni kweli inatakiwa aondoke hapo kikaoni hadi kwenye mabwawa ya kufua umeme ili kujuwa nini kifanyike na hali ikoje na siyo kusubiri ripoti mezani bila kujuwa hata uhalisia.