Maharage wa TANESCO atimuliwa kwenye kikao cha Waziri Mkuu Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu Biteko. Apewa siku tatu

Maharage wa TANESCO atimuliwa kwenye kikao cha Waziri Mkuu Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu Biteko. Apewa siku tatu

Ni kweli inatakiwa akashughulikie umeme na siyo kukaa mezani. Ni muda wa kwenda kukaa na watumishi wote kuhakikisha kuwa watanzania wanapata umeme. Watanzania wanataka umeme waendelee na shughuli zao za uchumi, kuendelea kukaa kwenye vikao badala ya kwenda kuumiza kichwa ya namna ya kulipatia Taifa umeme ni sawa na kuwatia umaskini Watanzania,Ni sawa na kuwarudisha nyuma wajasiriamali,Ni sawa na kukwamisha uzalishaji viwandani na hivyo kupelekea upungufu wa bidhaa na hivyo kupanda kwa Bei kwa Bidhaa na hivyo kumuumiza mwananchi. Ni kweli inamoasa aende akashughulikie suala la umeme ili kuliondoa Taifa na Taharuki ya umeme,ni kweli aende akashughulikie umeme ili watu wasipate hasara ya kuharibika kwa bidhaa zao kama vile samaki wabichi kwa kukosekana kwa umeme. Inatakiwa aende akakune kichwa ili watu wapate umeme.

Mh Rais anataka wananchi wake wanaompenda na kumuunga mkono kwa mamilioni yao wapate umeme wa uhakika,.hivyo anapaswa kwenda kuweka mipango ya kuhakikisha umeme unapatikana kwa njia yoyote ile. Ni kweli inatakiwa aondoke hapo kikaoni hadi kwenye mabwawa ya kufua umeme ili kujuwa nini kifanyike na hali ikoje na siyo kusubiri ripoti mezani bila kujuwa hata uhalisia.
huyu maharage aliteuliwa na nani...si rais...?shida si maharage shida ni huyu mama ndo tatizo kwa nchi analea ujinga...analea wafanyakazi mzigo...
 
Boss wa TANESCO atimuliwa kikaoni. Sioni nyota njema kwake.

Kaambiwa nenda kashughulikie Umeme. Alikuwa high Table amekaa kwenye Maonesho yanayoendelea ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam

Tarehe 25 Septemba 2021, Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO akichukua nafasi ya Dkt. Tito Mwinuka

Kutokana na Mgao Mkubwa wa Umeme unaoendelea Nchini, Maharage anadai hakuna Mgao bali ni Upungufu wa umeme.

Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Maharage Chande aliwaomba Wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho kuna Upungufu wa Umeme unaosababisha baadhi ya Maeneo kuwa na Umeme na mengine kukosa Huduma hiyo

Maharage alisema "Katika Mtandao wa Umeme hitilafu huwa zinatokea mara kwa mara na pale zinapotokea Wateja wetu huwa tunawataarifu. Tunapopata upungufu sio Nchi nzima inakuwa haina Umeme ila ni kwa baadhi ya maeneo na huwa tunatoa taarifa"

Sasa baada ya kwambiwa aende kushughulikia umeme, nulijua ataenda site. Cha ajabu yupo Ofisini kwake Ubunge kaka huku tai ameilegeza, inaonekana ana mawazo sana.

Tumuombee presha yake isipande.
Huyu maharage hana sifa wala uwezo kuendesha tanesco. Tatizo hawa wahuni aliyowaamini mama wanamshauri kupeana teuzi kishikaji. Wameondoa watu waliyosimamia tanesco vizuri team ya kalemani na CEO wake wakapangana waswahili wenye kujua kupiga watoto wa mujini eti sio washamba kama kina magufuli. Team ya majaliwa na biteko wapange upya kuanzia bodi tanesco. Ujuzi itikadi sahihi na uzalendo ni muhimu. Kina gachuma majaar na barhesa yote ni maslahi tu ya wafanya biashara.
 
Kumbuka kauli ya Mh Naibu waziri mkuu kuwa Watanzania wanahitaji umeme tu.
Kwa hiyo umeme umeshikiliwa na Maharage na Staff wa Tanesco? Haya umeme umekuja? Hao Watanzania ni mburula kiasi kwamba hawawezi eleweshwa sababu wakaelewa?

Waambie Serikali watoe pesa ku diversify vyanzo sio kuleta ujinga,hizo pesa hatoi Chande Bali Biteko na wenzie huko Serikalini.
 
Ndio maana ya kutolewa kikaoni ili akafuate hela kama shida ni hela ndio aende huko akaseme anaomba hela 😄😄😄
 
Labda alikua na bifu nae si unajua wabongo kwa kulipiza

Bifu la nini wakati reality ni kwamba umeme hakuna? Badala ya kushughulikia tatizo anaendekeza projects na kufunga tai. Tai unafunga wakati unasherekea mafanikio na si wakati wa kutoka jasho. Hapo ndo shida kwa nchi yetu. Kama vipi arudi Multi-Choice tu! Tanesco is a public office ambako lazima jasho likutoke.
 
Ni kweli inatakiwa akashughulikie umeme na siyo kukaa mezani. Ni muda wa kwenda kukaa na watumishi wote kuhakikisha kuwa watanzania wanapata umeme. Watanzania wanataka umeme waendelee na shughuli zao za uchumi, kuendelea kukaa kwenye vikao badala ya kwenda kuumiza kichwa ya namna ya kulipatia Taifa umeme ni sawa na kuwatia umaskini Watanzania,Ni sawa na kuwarudisha nyuma wajasiriamali,Ni sawa na kukwamisha uzalishaji viwandani na hivyo kupelekea upungufu wa bidhaa na hivyo kupanda kwa Bei kwa Bidhaa na hivyo kumuumiza mwananchi. Ni kweli inamoasa aende akashughulikie suala la umeme ili kuliondoa Taifa na Taharuki ya umeme,ni kweli aende akashughulikie umeme ili watu wasipate hasara ya kuharibika kwa bidhaa zao kama vile samaki wabichi kwa kukosekana kwa umeme. Inatakiwa aende akakune kichwa ili watu wapate umeme.

Mh Rais anataka wananchi wake wanaompenda na kumuunga mkono kwa mamilioni yao wapate umeme wa uhakika,.hivyo anapaswa kwenda kuweka mipango ya kuhakikisha umeme unapatikana kwa njia yoyote ile. Ni kweli inatakiwa aondoke hapo kikaoni hadi kwenye mabwawa ya kufua umeme ili kujuwa nini kifanyike na hali ikoje na siyo kusubiri ripoti mezani bila kujuwa hata uhalisia.
Lucas mwashambwa acha tabia ya kuwa na double standard! Just imagine Hata huyo unayem praise sana anakufikiriaje! Ungetueleza Maharage ashughulikie tatizo kwa namna gani ukizingatia taasisi nayo ilishakuja na jibu la kwamba shortage inatokana na kuchelewa kwa mvua/upungufu wa maji. And what if kwenye hiko kikao alikuwa na alternatives za ku present. By the way hata ningekuwa mimi ningemtimua tu kwenye hiko kikao kwasababu Maharage was fulfilling his responsibilities on behalf of the one who suggested him to the appointer.
 
Zero brain Chande ndio Huwa anafuta pesa za kutekeleza miradi ya Tanesco? Toeni ujinga hapa ,pelekeni hela Tanesco
😄😄😄😄 Ndio akamfuate anayetoa hela amwambie atoe hela ili asifukuzwe tena kikaoni. Ndio maana NW mkuu akasema watanzania wanahitaji umeme,kwa hiyo ili usifukizwe kwenye vikao kwasababu ya kutokuwepo kwa umeme basi hakikisha unawatafuta wahusika mapema wakipatiwa kile kinachokwamisha upatikanaji wa umeme.
 
Back
Top Bottom