Maharage wa TANESCO atimuliwa kwenye kikao cha Waziri Mkuu Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu Biteko. Apewa siku tatu

Biteko na wenzie ndio watia hela,amfuate wapi? Toa ujinga hapa.
 
Nani anaemteua? Halafu kwani Maharage Chande ndio kaleta ukame? Maharage ndio mtoa pesa za kuanzisha vyanzo vipya? Upuuzi.

Ila Sasa Kwa Afrika Jamaa wanaodhalilisha hivi na kuongea ndio huonekana Viongozi Sasa 😁😁
Yeye ndie MD - hawezi kukimbia matatizo ya TANESCO. Ameweza kuirekebisha Customer care - iko vizuri. Sasa aangalie kuhusu upatikanaji wa huo umeme. Maana hai-make sense kuunganisha wateja wengi ambao hawapati umeme.
 
Hata Nyerere Dam ikikamilika , bado tatizo halitaisha ,kila siku watu ,/kaya za watumiaji wapya wa nishati ya umeme wanaungwa kwenye grid kwa. Kupitia REA .
Grid hii hii ambayo haina ongezeko la vyanzo vya nishati , unategemea nini ?
Ni lazima serikali iwekeze pesa za kutosha kujenga vyanzo vipya vya kufua umeme .
Maana population inaongezeka na mahitaji yanaongezeka kila kukicha .
Tuwekeze kwenye kujenga vinu vya kufua umeme kwa makaa ya mawe ,nuclear na gas .
Hamna solution zaidi ya hiyo .
Kila siku watakuwa wanatufanyia maigizo yasiyo na kichwa wala miguu kama hivyo .
 
Mkuu kwani kati ya waziri na katibu mkuu wa wizara nani anayeidhinisha na anayetoa hela?
Waziri alete pesa hakuna maneno hapa,Tanesco wanahitaji 4T Ili ku stabilize grid ,Kwa hiyo Waziri wako asikizungushe na kuleta maigizo ya kijinga.

Unachoongea wewe ni kama vile Pale Mkuranga mbunge amesema umeme umekatika mara 22 Kwa hiyo Rais amtimie Naibu Waziri pale Ili akalete umeme? Samia sio mpumbavu kama Hawa unaowatetea.
 
Kumbuka kauli ya Mh Naibu waziri mkuu kuwa Watanzania wanahitaji umeme tu.
Haya ndio Maneno...Watanzania wanataka UMEME; hayo matatizo ni ya kwao. Kuna MD, Katibu Mkuu, Naibu Waziri, na Waziri - ndio maana wapo hapo. Wakayatatue. Sasa watanzania wakiambiwa hayo matatizo - ndio waende wakakae kwenye Ofisi za Tanesco na Wizara kuyatatua?
 
Jina lenyewe Maharage akili je?
 
Nigeria wametangaza hali ya dharura ya kukosekana umeme, hapo SA umeme umeshawachezesha manyanga hadi hangaya akampa ahadi Ramaphosa kwamba atawauzia umeme wakati kwake mwenyewe anawasha kibatari, hizi nchi za kiafrika zina comedy sana........mbona haya hayaonekani ulaya?​
 
Nyerere Dam ikiisha tutapata unafuu kwa miaka 3 hivi....
Naamini kuna mipango mingi ipo ya kuongeza uzalishaji wa umeme hasa vyanzo ambavyo sio vya maji..

Bado tunahitaji Kinyerezi Three..
Kule Kilwa kunahitaji pia ujenzi wa power house
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…