Maharage wa TANESCO atimuliwa kwenye kikao cha Waziri Mkuu Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu Biteko. Apewa siku tatu

Maharage wa TANESCO atimuliwa kwenye kikao cha Waziri Mkuu Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu Biteko. Apewa siku tatu

πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ Ndio akamfuate anayetoa hela amwambie atoe hela ili asifukuzwe tena kikaoni. Ndio maana NW mkuu akasema watanzania wanahitaji umeme,kwa hiyo ili usifukizwe kwenye vikao kwasababu ya kutokuwepo kwa umeme basi hakikisha unawatafuta wahusika mapema wakipatiwa kile kinachokwamisha upatikanaji wa umeme.
Biteko na wenzie ndio watia hela,amfuate wapi? Toa ujinga hapa.
 
Maharage anadai hakuna Mgao bali ni Upungufu wa umeme.
1000037009.jpg
 
Nani anaemteua? Halafu kwani Maharage Chande ndio kaleta ukame? Maharage ndio mtoa pesa za kuanzisha vyanzo vipya? Upuuzi.

Ila Sasa Kwa Afrika Jamaa wanaodhalilisha hivi na kuongea ndio huonekana Viongozi Sasa 😁😁
Yeye ndie MD - hawezi kukimbia matatizo ya TANESCO. Ameweza kuirekebisha Customer care - iko vizuri. Sasa aangalie kuhusu upatikanaji wa huo umeme. Maana hai-make sense kuunganisha wateja wengi ambao hawapati umeme.
 
Watu wengi wanafikiri umeme unatosha nchi hii...
Umeme hautoshi na kwa kipindi kirefu hakukuwa na chanzo kipya cha umeme..

Tunasubiri Julius Nyerere Dam ikamilike..
Naona ile connection ya line kutoka Arusha kwenda Namanga inakaribia kuisha... Wanunue hata megawatts 400 kutoka Ethiopia unaopitia Kenya pengine unafuu utapatikana
Hata Nyerere Dam ikikamilika , bado tatizo halitaisha ,kila siku watu ,/kaya za watumiaji wapya wa nishati ya umeme wanaungwa kwenye grid kwa. Kupitia REA .
Grid hii hii ambayo haina ongezeko la vyanzo vya nishati , unategemea nini ?
Ni lazima serikali iwekeze pesa za kutosha kujenga vyanzo vipya vya kufua umeme .
Maana population inaongezeka na mahitaji yanaongezeka kila kukicha .
Tuwekeze kwenye kujenga vinu vya kufua umeme kwa makaa ya mawe ,nuclear na gas .
Hamna solution zaidi ya hiyo .
Kila siku watakuwa wanatufanyia maigizo yasiyo na kichwa wala miguu kama hivyo .
 
Mkuu kwani kati ya waziri na katibu mkuu wa wizara nani anayeidhinisha na anayetoa hela?
Waziri alete pesa hakuna maneno hapa,Tanesco wanahitaji 4T Ili ku stabilize grid ,Kwa hiyo Waziri wako asikizungushe na kuleta maigizo ya kijinga.

Unachoongea wewe ni kama vile Pale Mkuranga mbunge amesema umeme umekatika mara 22 Kwa hiyo Rais amtimie Naibu Waziri pale Ili akalete umeme? Samia sio mpumbavu kama Hawa unaowatetea.
 
Kumbuka kauli ya Mh Naibu waziri mkuu kuwa Watanzania wanahitaji umeme tu.
Haya ndio Maneno...Watanzania wanataka UMEME; hayo matatizo ni ya kwao. Kuna MD, Katibu Mkuu, Naibu Waziri, na Waziri - ndio maana wapo hapo. Wakayatatue. Sasa watanzania wakiambiwa hayo matatizo - ndio waende wakakae kwenye Ofisi za Tanesco na Wizara kuyatatua?
 
Boss wa TANESCO atimuliwa kikaoni. Sioni nyota njema kwake. Siku tatu zinamtosha kweli au ndo wanamkomoa baba wa watu?

Na Biteko ikaja kujua dili za Luku atamla kichwa mazima.

Kaambiwa nenda kashughulikie Umeme. Alikuwa high Table amekaa kwenye Maonesho yanayoendelea ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam

Tarehe 25 Septemba 2021, Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO akichukua nafasi ya Dkt. Tito Mwinuka

Kutokana na Mgao Mkubwa wa Umeme unaoendelea Nchini, Maharage anadai hakuna Mgao bali ni Upungufu wa umeme.

Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Maharage Chande aliwaomba Wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho kuna Upungufu wa Umeme unaosababisha baadhi ya Maeneo kuwa na Umeme na mengine kukosa Huduma hiyo

Maharage alisema "Katika Mtandao wa Umeme hitilafu huwa zinatokea mara kwa mara na pale zinapotokea Wateja wetu huwa tunawataarifu. Tunapopata upungufu sio Nchi nzima inakuwa haina Umeme ila ni kwa baadhi ya maeneo na huwa tunatoa taarifa"

Sasa baada ya kwambiwa aende kushughulikia umeme, nulijua ataenda site. Cha ajabu yupo Ofisini kwake Ubunge kaka huku tai ameilegeza, inaonekana ana mawazo sana.

Tumuombee presha yake isipande.

Baadhi ya Watanzania wamesema mgao wa umeme umekuwa ukisababisha hasara katika biashara zao mara kwa mara. Na wamelitaka shirika la umeme (TANESCO), kutoa taarifa rasmi ya jinsi mgao huo unavyoendeshwa. Je, kwa sasa Tanesco inazalisha kiwango gani cha umeme? Ni upungufu wa aslimia ngapi?
Jina lenyewe Maharage akili je?
 
Nigeria wametangaza hali ya dharura ya kukosekana umeme, hapo SA umeme umeshawachezesha manyanga hadi hangaya akampa ahadi Ramaphosa kwamba atawauzia umeme wakati kwake mwenyewe anawasha kibatari, hizi nchi za kiafrika zina comedy sana........mbona haya hayaonekani ulaya?​
 
Hata Nyerere Dam ikikamilika , bado tatizo halitaisha ,kila siku watu ,/kaya za watumiaji wapya wa nishati ya umeme wanaungwa kwenye grid kwa. Kupitia REA .
Grid hii hii ambayo haina ongezeko la vyanzo vya nishati , unategemea nini ?
Ni lazima serikali iwekeze pesa za kutosha kujenga vyanzo vipya vya kufua umeme .
Maana population inaongezeka na mahitaji yanaongezeka kila kukicha .
Tuwekeze kwenye kujenga vinu vya kufua umeme kwa makaa ya mawe ,nuclear na gas .
Hamna solution zaidi ya hiyo .
Kila siku watakuwa wanatufanyia maigizo yasiyo na kichwa wala miguu kama hivyo .
Nyerere Dam ikiisha tutapata unafuu kwa miaka 3 hivi....
Naamini kuna mipango mingi ipo ya kuongeza uzalishaji wa umeme hasa vyanzo ambavyo sio vya maji..

Bado tunahitaji Kinyerezi Three..
Kule Kilwa kunahitaji pia ujenzi wa power house
 
Back
Top Bottom