Maharage wa TANESCO atimuliwa kwenye kikao cha Waziri Mkuu Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu Biteko. Apewa siku tatu

Maharage wa TANESCO atimuliwa kwenye kikao cha Waziri Mkuu Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu Biteko. Apewa siku tatu

Yeye ndie MD - hawezi kukimbia matatizo ya TANESCO. Ameweza kuirekebisha Customer care - iko vizuri. Sasa aangalie kuhusu upatikanaji wa huo umeme. Maana hai-make sense kuunganisha wateja wengi ambao hawapati umeme.
Nimekuuliza Maharage ndio ameleta ukame?

Maharage ndio mtoa pesa za kujenga miradi Nje ya vyanzo vya maji huko Tanesco?

Alishaleta Serikalini kinachotakiwa ni swala la kina Biteko na wenzie kuleta pesa Tanesco sio kukikosha Kwa maigizo ya kijinga.

Mwisho Biteko akiwa MD wa Tanesco anaweza leta Umeme?
 
TANESCO inaendeshwa kisiasa.

Watanzania hawalipii gharama halisi za umeme, wanalipa gharama ndogo sana, halafu, wakati kawaida ni watumiaji wakubwa wa viwandani kufidia tofauti, uchumi hauna watumiaji wakubwa wa kutosha wa kulipia the difference.

Matokeo yake, it's a vicious circle of poverty.

Umeme kukosekana inadumaza uchumi, na uchumi kudumaa kunafanya watumiaji wakubwa washindwe ku support matumizi ya umeme ya general population na umeme ukosekane.

Kwa msingi huo, hawa kina Maharage, they are set to fail.

Kitu cha kwanza kinachotakiwa ni kuondoa ukiritimba wa TANESCO kuwa na monopoly kwenye umeme.

Unategemea vipi ufanisi kwenye biashara ya monopoly?

Achia kuwe na makampuni matano ya umeme yanagombea wateja, halafu angalia competition ya kibiashara unavyomaliza matatizo.

Unategemea vipi efficiency kwenye monopoly?
 
Wamechelewa sana ku engage private sector kwenye kuzalisha na kusambaza umeme, hiki chanzo cha maji tayari kimeonyesha kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo serikali kupitia monopoly ya Tanesco haitaweza tena kuzalisha na kusambaza umeme effectively in a long run.
 
Na bado wamekomaa nacho..kaazi kweli kweli.
 
Boss wa TANESCO atimuliwa kikaoni. Sioni nyota njema kwake. Siku tatu zinamtosha kweli au ndo wanamkomoa baba wa watu?

Na Biteko ikaja kujua dili za Luku atamla kichwa mazima.

Kaambiwa nenda kashughulikie Umeme. Alikuwa high Table amekaa kwenye Maonesho yanayoendelea ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam

Tarehe 25 Septemba 2021, Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO akichukua nafasi ya Dkt. Tito Mwinuka

Kutokana na Mgao Mkubwa wa Umeme unaoendelea Nchini, Maharage anadai hakuna Mgao bali ni Upungufu wa umeme.

Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Maharage Chande aliwaomba Wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho kuna Upungufu wa Umeme unaosababisha baadhi ya Maeneo kuwa na Umeme na mengine kukosa Huduma hiyo

Maharage alisema "Katika Mtandao wa Umeme hitilafu huwa zinatokea mara kwa mara na pale zinapotokea Wateja wetu huwa tunawataarifu. Tunapopata upungufu sio Nchi nzima inakuwa haina Umeme ila ni kwa baadhi ya maeneo na huwa tunatoa taarifa"

Sasa baada ya kwambiwa aende kushughulikia umeme, nulijua ataenda site. Cha ajabu yupo Ofisini kwake Ubunge kaka huku tai ameilegeza, inaonekana ana mawazo sana.

Tumuombee presha yake isipande.

Baadhi ya Watanzania wamesema mgao wa umeme umekuwa ukisababisha hasara katika biashara zao mara kwa mara. Na wamelitaka shirika la umeme (TANESCO), kutoa taarifa rasmi ya jinsi mgao huo unavyoendeshwa. Je, kwa sasa Tanesco inazalisha kiwango gani cha umeme? Ni upungufu wa aslimia ngapi?
Acha ashughulikiwe ili apate akili
 
Nimekuuliza Maharage ndio ameleta ukame?

Maharage ndio mtoa pesa za kujenga miradi Nje ya vyanzo vya maji huko Tanesco?

Alishaleta Serikalini kinachotakiwa ni swala la kina Biteko na wenzie kuleta pesa Tanesco sio kukikosha Kwa maigizo ya kijinga.

Mwisho Biteko akiwa MD wa Tanesco anaweza leta Umeme?
Kwamba kinachotakiwa ni serikali kupeleka pesa, ili zikafanye nini sasa hapo TANESCO kama kiongozi aliyepo hapo juu ni boya asiyekuwa na maono yoyote ya kuliongoza hilo shirika..?

Shida ya hii nchi sio kupeleka pesa kwenye maeneo fulani, shida ni wakina nani walioko huko zinakopelekwa? Wengi walioko kwenye mashirika na wazira mbalimbali ni wehu, wezi mabogus, wasiojua lolote. Kupeleka hela kwa aina hiyo ya watu ni UPUMBAVU usioweza kusaidia chochote.
 
Back
Top Bottom