Mahari sio lazima, ni mila potofu ya kupingwa



Sidhani kama mwanamke ana bei ambayo waweza mnunua, ni kama shukrani tu, na asante kwa Mzazi kumlea.

Hata kwa Mungu mambo yakifanikiwa huwa tunatoa shukran, sasa sijui tunanunua nini kwa Mungu?

Mtu kamlea mwanaye, Kamsomesha mpaka kafika chuo, na ajira labda kapata, kuna shida gani kushukuru?

Na mahari sio lazima, kataa kulipa, utamchukua tu mkeo, watu wakipendana hakuna wa kuwakataza.

Lakini mimi nakataa kwamba magari ni mila mbovu na ya zamani isiyofaa, lazima tuseme asante.
 

Uliwahi Kupangiwa bei na gharama za shukrani na ikaitwa shukrani?

Mahari ni Mila za kipagani, kikafiri. Shukrani MTU anatoa kadiri atakavyoona na sio Ukweni ndio wapange gharama na bei ya shukrani. Hiyo ni biashara ya kuuzana.

Mwanzo 31
14 Raheli na Lea wakajibu, wakamwambia, Je, Imebakia sehemu au urithi kwa ajili yetu katika nyumba ya baba yetu? 15 Hakutufanya kama wageni, maana ametuuza, naye amekula fedha zetu kabisa?

hao ni mabinti wa Labani wanamlalamikia Baba Yao Mbele ya mume wao Yakobo. Kumbuka Labani ni mpagani na anaishi katika Nchi za kipagani
 
Mimi hata wakitaka 50k siwapi, hawataki wachukue mtoto wao, mama Sasha mwenyewe sasa kipindi nimepewa kima akanambia achana nao wanafikiri hela zinaokotwa kafanyie mambo mengine hela zako
 
Unakuta unaambiwa mahari mil.5 usipotoa hatukuozi mwanetu....
 
Kwani huyo mzazi wa mwanaume naye si kamsomesha pia mwanae??Nae anahitaji shukrani

Na tena kwa sababu mwanaume ndio atakua na jukumu la kulea familia,ikiwepo huyo mwanamke,ningetegemea ingekua kinyume chake kwamba wazazi wa mtoto wa kike ndio watoe mahali kumpunguzia mzigo mume..
 
Hili swala la mahari tumeliona toka kwenye historia ya zamani. Mfano kwenye Biblia hili swala lipo. Unaweza jiuliza Biblia ina mda gani toka iwepo na swala hili lina maana gani. .

Tatizo lako la kutafsiri ni potovu ndio maana unalitafsiri kwa uelewa mdogo. Kama ungetambua mahari lina maana gani na kwa nini inalipwa basi usingesema una logic kubwa. Kwako wewe mahari ni kumnunua mwanamke🤣 kama ni kumnunua hata mimi napinga ila nakupa kazi nenda katafute mahari maana yake ni nini? ukishindwa njoo nikufafanulie. .

Have a blessed day...
 
Watibeli mnapatikana wapi? Maana mnaeza kuwa msaada wetu hapo mbeleni kwa suala hilo
 
Mimi hata wakitaka 50k siwapi, hawataki wachukue mtoto wao, mama Sasha mwenyewe sasa kipindi nimepewa kima akanambia achana nao wanafikiri hela zinaokotwa kafanyie mambo mengine hela zako

Huenda wanahaki.
Ungewauliza Kwa nini na inaulazima upi?
 

Kitu kikiwa kwenye Biblia au Quran au kitabu chochote hakimaanishi kitu hicho ni lazima au ni Sahihi.
Labda kitu hicho kiwe ni neno la Muumba mwenyewe, amri na sheria yake.
Na sio Mapokeo ya Watu.
Hata kwenye Biblia na Quran kuna Mapokeo ya wanadamu hicho ndicho nikisemacho.

Kula chuma hiyo;
Marko 7
7 Kuniabudu kwao ni bure. Wanafundisha watu amri zao badala ya sheria yangu.’ 8 Ninyi mmeziacha amri za Mungu na kushikilia desturi za watu.”9 Akawaambia, “Mnaepuka kwa ujanja amri za Mungu ili mpate kutimiza desturi zenu!

Mathayo 15:
7Enyi wanafiki! Isaya alitabiri sawa kabisa juu yenu:
8‘Mungu asema: Watu hawa huniheshimu kwa maneno tu,
lakini mioyoni mwao wako mbali nami.
9Kuniabudu kwao hakufai,
maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu.’”

Sasa unaweza ukatupa sheria au amri ya Mungu inayotaka Watu walipe Mahari.
Nafikiri unajua Sifa za amri na sheria za Mungu.
Karibu kwenye reference,
 
Unafahamu maana ya shukrani??
 
Hilo kabila linapatikana wapi aisee, kumbe hakuna mahari kwanza hizo PISI NI WAKALI au ndo wanazidiwa na vinyago vya kariakoo vile vya nguo

Binti yeyote utakayekutana naye anayependa Haki, ukweli, upendo, Maarifa, ambaye Kwa hakika akiwa maambo hayo atakuwa Huru. Na akiwa huru hatataka Mahari wala kujiuza, wala kuuzwa, Kwa sababu yeye ni MTU Huru. Basi jua umekutana na Binti wa Tibeli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…