Mahari sio lazima, ni mila potofu ya kupingwa

Ni kweli kabisa.

LAKINI bado tuko na wazazi wetu ambao huwaambii kitu kuhusu mahari na usipotoa hawaelewi

nadhani tuwaelimishe wanawake tunaotaka watolea mahari kwamba Tunatoa ili tu kama heshima

kwa wazazi wasituone wakaidi na si vinginevyo,kisha sisi watoto zetu tuweke misimamo ya kutotolewa

mahari, lakini kwasasa tuendelee na mfumo uliopo maaana waanzilishi wapo,ila enzi zetu zikifika sisi kuozesha

basi tufanye haya tunayotamani,hii kitu haiwezi badilishwa haraka haraka kiasi hiki,n taratbu taratbu.
 
Kila mtu na mila yake wewe shika yako na mimi nibaki na yangu
 

Ni kweli Kabisa.
Kwa Wababa wa sasa(Sisi) baadhi yetu hatutakubali kuuza Binti zetu.
 
Sijamaliza uzi wako kama kawaida yako no summary!
Kat ya faida ni;
kopimo cha
Muoaji kujituma.
Kuzuia kuachana kirahisi.
Kuweka uhusiano mwema.
Pesa hio kuhudumia sherehe.
Kuwachukulia binti yao waliomzoea na huwa msaada pale nyumbani.
Kuzuia binti asirudi nyumbani kirahisi.
Faida ni nyingi kuliko hasara.
Halafu mahali huwa haiishi ndugu ili uwe unaenda kuwasalimia unapunguza Kidogo.
Wahindi wao humlipia mwanaume mahali una maoni gani?
 
Kwa waislam mahari ni mfumo ambao upo katika dini na haikubaliki ndoa pasina mahar so kwa muislam yeyote hawez akacha kutoa mahari kwa utashi wake au usasa uliopo
 
Kwa waislam mahari ni mfumo ambao upo katika dini na haikubaliki ndoa pasina mahar so kwa muislam yeyote hawez akacha kutoa mahari kwa utashi wake au usasa uliopo
Argument from tradition plus argument from authority.

Two logical fallacies at once.
 

Kwamba Mahari ni kipimo cha Muoaji.
Kwamba Mahari inazuia Watu kuachana kirahisi?😂
Mkuu embu kuwa Serious kidogo.
 
Binti yeyote utakayekutana naye anayependa Haki, ukweli, upendo, Maarifa, ambaye Kwa hakika akiwa maambo hayo atakuwa Huru. Na akiwa huru hatataka Mahari wala kujiuza, wala kuuzwa, Kwa sababu yeye ni MTU Huru. Basi jua umekutana na Binti wa Tibeli.
Kwa hyo tibeli sio kabila
 
Kama umezaliwa na single mother, mahari ni kitu kibaya sana. Kama unaoa vyangudoa kama wale kutoka karibu na mlima mrefu sana Afrika, basi una hoja. Ila kama unaoa mke mke kweli mahari ni tunu
 
Hii ni ELIMU juu ya Mtu Mume na Mtu Mke.

Mtu Mke ni Zawadi kwa Mtu Mume tangu siku ya Kwanza.

Mwanaume asiyemchukulia Mwanamke kama Kitu cha Zawadi bado hajajua kwa nini anamuhitaji Mwanamke.

Mahari ni ishara ya ku appreciate Zawadi unayotarajia kupewa na wazazi husika!

Binti hutunzwa na wazazi tangu akiwa Mdogo akifundishwa kwamba atakuwa mtu wa Mtu Siku moja...

Atatolewa kuwa Mtu wa Mtu Mume siku moja!

Hiyo tu kwa mwanamume ni wake up call kwamba ameandaliwa mtu wa kuishi naye...ampende na Kumtunza kwa usitawi wa familia anayotarajia kuianza!

Kwanza kwa tamaduni za Kiafrika ndo na watoto wote wanatajwa kwa jina la Mwanamume..!Bado tu huoni Sababu ya kulipa Mahari?

Mahari yako kwenye jamii zote!!

Usijidanganye
Mwanamume shurti ujiandae kumpata Mke kwa kuonesha Ishara ya UPENDO na KUTHAMINI MATUNZO YA MKEWE MTARAJIWA KUTOKA KWA WAZAZI WAKE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…