Mahesabu msiyopenda kusikia kuhusu Makamu mpya wa Rais

Ulivyoandika kama msomi mbombezi kumbe mpiga umbeya tu.
 
Unapangua Kwa hekima, sio unafika unafukuza katibu, Kesho Waziri mkuu, Kesho hivi keshokutwa vile duh
Apangue kwa hekima yake yeye mpanguaji au kwa hekima za wanaopanguliwa?
 
Mchezo mchezoni.
Nae rais anaweza kuvunja bunge
 
Ile siku wanakaa kikao, wanapelekewa wajeda ili kulinda usalama wao.

Na wengine wanawekwa ndani kwa tuhuma za uhujumu uchumi

Usicheze na mtu aitwaye Amiri jeshi mkuu
Hujajua wangapi wako upande huu na wangapi upande ule, na hapo bado hujahesabu wale ndumilakuwili na "bendera-fuata-upepo"
 
Wewe ndio unadhani urais ni mtu mmoja maana unataka kutuonyesha kwamba hayo yote yakifanyika Rais kalala tu he knows nothing kinachoendelea kule bungeni.
Katika hao wa kumwambia kinachoendelea, masnitch wamo miongoni mwao. Ni mwendo wa kupotezeana ramani tu. Kama ananisikia aanze na hao before it is too late.
 
Haya yote yanafanyika huku mabaka baka wakiwa wapo tu wanaangalia mnavyocheza na amiri jeshi wao. Labda kama na wao hawamtaki.
Kwahiyo wavunje katiba? Ni utawala wa kijeshi au?
 
Elias John Kuandikwa for VP ndiyo dokezo Hilo ...!
Yuko kambi gani huyu? Tunajua kuna kambi ya marehemu (nimesikia wakiitwa 'yatima') na kuna kambi ya mamvi (imeibuka kutoka mafichoni). Wote wamempania mama. Niliwaelewa wale waliomhakikishia mama ushirikiano kwenye salamu zao jana, wanajua hana kambi na anahitaji kuungwa mkono.
 
Kwahiyo wavunje katiba? Ni utawala wa kijeshi au?
Wala. Hata kuvunja bunge ipo ndani ya katiba. Mkikaa mnawaza kupiga kura usalama unampa taarifa raisi na yeye anavunja bunge na kuitisha upya uchaguzi huku jeshi likiwa nyuma yake.

Kwa katiba yetu kuna vitu vitatu tu vinaweza mtoa raisi:
Nguvu ya uma
Jeshi lililoasi(Usalama, mabakabaka, polisi)
Kifo au ugonjwa beyond repair.
 
Hatujafikia kiwango hicho Ila itafikiwa endapo Rais ataanza kupangua Safu iliyopo kiholela holela
Wala msimtishe rais na atapangua safu na mambo yataenda kama kawaida kama alivyo fanya mtangulizi wake kwa safu aliyo ikuta maana kuiacha safu iliyopo kama ilivyo ni kukaribisha kuhujumiwa na kundi la mtangulizi wake ambalo sasa limeanza kuaminishwa kuwa mtangulizi kahujumiwa

Lakini pia kundi hilo linamikakati ya kuonesha umma kwamba hakuna rais atakaye mzidi huyo wa kwao kiutendaji na kwamba huyo alikuwa masihi na nabii mtukufu kweli kweli hawezi kutokea tena mwingine.

Ila pangua yake lazima iwe ya kimkakati kama alivyo fanya mtanguliz wake atatoka mmoja mmoja taratibu hadi wataisha wote na wqtakao baki ni wale tu ambao hawana upambe.
 
Rais akivunja bunge yeye anabaki kuwa rais.
 
Hapo kwenye kuitisha uchaguzi tena hapo wabunge hawatakubali kufika huko maana wanajua walivyo upata ubunge huo na wana hakika likitokea hilo hawata rudi tena hapo watatii tu mamlaka iliyopo.
 
Umeielewa lakni comment yangu au umekrupuka na hangover
 
Hakuna kitu kama hicho kitatokea,jeshi liko nyuma ya Raisi Samia suluhu Hassan.Unafikiri rahisi kihivyoo eeeh.
Rejea hotuba ya General Mabeyo jana.
 
Hapo kwenye kuitisha uchaguzi hapo wabunge hawatakubali kufika huko maana wanajua walivyo upata ubunge huo watatii tu.
Watamuasi spika. Uitishe uchaguzi wa ubunge upya kisha uwaite wapinzani na kuahidi free and fair election mbunge gani atataka kuangalia hilo movie la kutisha usiku akiwa mwenyewe kwenye ukumbi wenye giza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…