Mahusiano mafupi kuliko yote ushawahi kuwa nayo

Mahusiano mafupi kuliko yote ushawahi kuwa nayo

Rejea swali lake..Je one night stand nayo inahesabika?.

Ni kweli inaweza tokea watu wakawa na uhusiana labda wa mwezi but baada ya ku do ukaishia hapo.
Hii hatusemi ni ya siku moja isipokuwa yalianza mwezi mzima
Ngoja nrudi kulala nliamka tu kukojoa..
Kesho tapangua hoja
 
Huyo jamaa hajiamini yani chips na soda kwaajir ya watoto tu zimemfanya akimbie wakati watoto hawana kosa kuwapa vizawadi watoto ni jambo jema
....hapo ishu sio chips na soda, ishu ni kwamba kwa akili za mwanamke kama huyo baada ya wiki mbili si atakuambia ada ya watoto imeisha walipie... Wote wanaoacha mademu baada ya kuombwa pesa siku ya kwanza au ya pili haimaanishi hiyo pesa hauna... Ni vile tu unamuona huyu hana subira wala aibu, hakuna feeling nzur kama kumuhudumia manz bila kukuomba, sasa hauwez kukutana naye leo tu uanze kufunguka anakuchukulia danga tu, ndio maana wengi tunataka at least tufahamiane kwanza kabla ya miamala
 
Siku ya kwanza unaanza kutangaza shida. Hatujaoana unaanza majukumu ya mume. Mm ukianza kutangaza shida nakuweka kwenye blacklist kabisa
Na hizo. Nyege zenu siku ya kwanza mnazitangaza ili iweje??

Mbona mnapenda kujiona watakatifu sana,,wakati chanzo ni nyie

Ukitulia na hizo hamu hakuna atakae kuomba pesa zaidi ya dada zenu.
 
Tulikutana mgawani macho yakakutana,nikamkonyeza akanirudishia mkonyezo..!
Haikuwa rahisi kumfuata alipokaa bali nilipomaliza nilienda kwa cashier nikalipa vyake na vyangu, kisha nikatoka nje nikamsubiri
Miaka hiyo hakukuwa na boda hivyo nilikodi baiskeli ya kumsindikiza aendako(alikuwa teyari keshatangulia)

Safari yetu iliishia shamba la migomba.. Kufumba na kufumbua alishasaula na kulala chini huku kachanua miguu.. Ilinichukua sekunde chache kujua ni chizi fuleshi
Mbio nilizotimua baada ya hapo sitakaa nikimbie vile tena maana kugeuka nyuma kaniungia uchi wa mbuzi huku akipiga kelele kwamba lazima nimuoe..[emoji24][emoji24][emoji1787]
Pole
IMG_20220616_162325.jpg
 
Mimi yangu yalidumu masaa matano tu .Kuna single maza mmoja tuko nae mtaani yuko vizuri anafaa kwa matumizi, juzi tu nilimuomba namba yake ilikuwa mchana akanipatia nikamuimbisha single maza kakubali, eti jioni ananipigia simu ananiambia "watoto wako wanataka chipsi mayai na mishkaki miwili" kabla hajakata simu akaniita "mumewangu" kisha akaniambia "uwachukulie wanao na soda" akamalizia kusema "nakupenda sana mumewangu"

Ana wazimu nikamtia bloku kwenye simu mpaka duniani, hata mapenzi hayajachanganya naitwa mume na watoto nimepewa. Mgonjwa kweli huyu single maza.
[emoji23][emoji23][emoji23]sasa si ndo kuhudumia
 
Ilikuwa kama dk 25 hivi alinikubalia kwenye simu tukawa wachumba, tumeendelea kupiga story nikagundua alishatoka na rafki yangu, tukaachana apoapo
 
Na hizo. Nyege zenu siku ya kwanza mnazitangaza ili iweje??

Mbona mnapenda kujiona watakatifu sana,,wakati chanzo ni nyie

Ukitulia na hizo hamu hakuna atakae kuomba pesa zaidi ya dada zenu.
Kingine mtu anajihami kwwmba ukishakula hutaonekana ndo maana matunzo yanaombwa mapemaaa
 
Wakuu habari zenu,

Huku tukiutafuta tafuta usingizi hebu tuambiane mahusiano ambayo umewahi kuwa nayo na yakawa mafupi kuliko yote.....

Ukitoa sababu ya kwanini mlidumu muda mfupi hivyo itakuwa vizuri. Binafsi mahusiano yangu mafupi kuliko yote yalichukua week moja.

Nlijiona tu siko sehemu salama nikaamua kukatisha kwa kumtafutia sababu isiyo na kichwa wala mguu na kuendelea na yangu.

Hadi leo yule kaka ananilaumu na ile sababu niliyomtafutia hajaikubali milele.
Back then kabla sijaoa, tulitamaniana na dada mmoja ambaye alikuwa ndio kaanza ajira mpya, akiwa amepanga maeneo ya sinza kwa Remy.

Wakati wote tulikuwa tunakutana kwenye kituo cha daladala sinza kwa remy, labda yeye akiwa anashuka kwenye gari au ndio anapanda kuondoka.

Siku hiyo, nikasema na liwalo liwe. Nilipomwona tu, nikaenda kupaki gari kwa mbele. Nikamfata kwa miguu. Tukatembea hadi kwake. Tulipofika tu, akaniambia kuwa siku hiyo ilikuwa zamu yake kununua umeme-basi nikajikamua nikatoa 20k, nikampa. Baada ya stori za hapa na pale nikala tunda halafu nikaondoka.

Kesho yake asubuhi, nilipowasha simu (kwa sababu enzi hizo tulikuwa tunashauriwa kuzima simu wakati wa kulala) zikaingia msgs zake kama tatu, zote zikiwa na ujumbe mmoja, kuwa mwenye nyumba kamkumbusha kulipa kodi, na anatakuwa alipe asubuhi hiyo, kwa hiyo ananisubiri kwa kituoni kwa remy nimpe laki 8.
Basi huo ukawa mwisho wetu. Nilimwacha in less than 24hrs.
 
Back
Top Bottom