Mimi yangu yalidumu masaa matano tu .Kuna single maza mmoja tuko nae mtaani yuko vizuri anafaa kwa matumizi, juzi tu nilimuomba namba yake ilikuwa mchana akanipatia nikamuimbisha single maza kakubali, eti jioni ananipigia simu ananiambia "watoto wako wanataka chipsi mayai na mishkaki miwili" kabla hajakata simu akaniita "mumewangu" kisha akaniambia "uwachukulie wanao na soda" akamalizia kusema "nakupenda sana mumewangu"
Ana wazimu nikamtia bloku kwenye simu mpaka duniani, hata mapenzi hayajachanganya naitwa mume na watoto nimepewa. Mgonjwa kweli huyu single maza.