Mahusiano Mapya ya Mara kwa Mara ni Umalaya au Safari ya Kumtafuta Mtu Sahihi?"


Bimkubwa hapo kwenye "kukuchafua hovyo" unamananisha nini? 😊
 
Kukumbatia watu ndio kunabadili matokeo ?
Hoja yangu umeielewa nusu Madam, maana yangu ni kwamba kama kila mtu unayekutana naye unaona hajakidhi standards zako, huenda tatizo likawa siyo yeye bali ni mtazamo na matarajio yako uliyo nayo wewe.

Kifupi usifanye kila tofauti kuwa sababu ya wewe kuachana na hayo mahusiano kwa sababu kila mwanadamu ana mapungufu yake.
Kutodumu na mtu msie na mitazamo sawa sioni tatizo lolote kabisa

Kuna vitu huwezi kumbadili mtu hata iweje

Nachoona mimi ni bora sana kua na mtu walau mnaenda hata ka asilia 70 hizo 30 mtavumiliana na kujengana
Ulicho kieleza hapa chini ndiyo hasa hoja yangu.

Watu wazima huwa hatujengi mahusiano kwa kutafuta ukamilifu, huwa tunayajenga kwa kuelewana, kuheshimiana na kuvumiliana licha ya tofauti zinazokuwepo.
 
Upo sahihi crush
Ulicho kieleza hapa chini ndiyo hasa hoja yangu.

Watu wazima huwa hatujengi mahusiano kwa kutafuta ukamilifu, huwa tunayajenga kwa kuelewana, kuheshimiana na kuvumiliana licha ya tofauti zinazokuwepo.
Imeisha hiyo twin
Wewe huko yanakuendea😎
 
Kuvumilia hawala hii nayo inafikirisha

Utapigwa mawe dada 🤣🤣

Sawa mahi

Kuvumilia hawala
sasa hii nimesoma koment huko juu mtu anampima msichana wa watu miaka mitatu. hao si ni mahawara wanaouvumiliana. hawara ukiachwa unalalamikia nani???

Mi huwa naongea ukweli ambassador watu wahataki kusikia hayo mawe yatanipita pembeni
 
Kuvumilia hawala
sasa hii nimesoma koment huko juu mtu anampima msichana wa watu miaka mitatu. hao si ni mahawara wanaouvumiliana. hawara ukiachwa unalalamikia nani???
Aisee miaka 3 huo muda wa Uvumilivu then utupwe huko hii ngumu kumeza bora mambo yamwagike asubuhi
Mi huwa naongea ukweli ambassador watu wahataki kusikia hayo mawe yatanipita pembeni
Nakukubali dear hukwepeshi
 
Ndugu mdau,
mie nadhani it's nature kwamba taste ya mahusiano yoyote yale ni changamoto zinazoonekana na zisizoonekana baina ya wahusika. Mahusiano yasiyo na changamoto nadhani hua ni hatari zaidi katika kudumu kwa muda mrefu.
Umalaya kwangu mimi hua naona ni dhana tu isiyo na athari zozote, kwasababu wanaoitwa malaya mara nyingi ndio huingia kwenye mahusiano mazuri zaidi na kuwaacha kwenye mshangao waliowaita malaya.

Kuingia kwenye mahusiano ya mara kwa mara sio dhambi, bali ni namna ya bora zaidi ya kupata upendacho, japo tabia hiyo inaweza kuonekana mbaya mbele ya jamii au kukupotezea muda na asipate atakacho muhusika asipokua makini.

Mahusiano matamu ni yale ambayo yanajengwa kwenye msingi wa wahusika kuridhiana na kila moja kua tayari na kukubali kubeba madhaifu ya mwenzake na kustahimili mapungufu ya mwenzake, kwasababu hayupo alie mkamilifu chini ya jua. Hii ikimaanisha ni lazima wanaoingia kwenye mahusiano kubeba changamoto za mwenzake na zile zitakazojitokeza katika mahusiano hayo.

Hapajawahi kutokea mahusiano yasiyo na changamoto dunia hii. Kua na mahusiano ya mara kwa mara ni kujaribu kutafuta au kuonja ladha tofauti za raha na changamoto za kwenye mahusiano tu, but daima hua hakuna mapya. ukiamua kuingia kwenye mahusiano ni muhimu kujua kwamba lazima kutakua na changamoto tu, upende usipende.

Ushauri wangu kwa wadau wa Jf,
Ni muhimu sana kuzichukua na kuzibadili changamoto za kwenye mahusiano na kuzifanya kua fursa muhimu ya kua makini zaidi kwenye mahusiano mapya, kujisahihisha, kujirekebisha na hatimae kuingia kwenye mahusiano madhubuti yenye furaha na amani ya kudumu licha ya changamoto tofauti zitakazojitikeza ndani yake kwasababu za kibinadamu ambazo daima haziepukiki.

ni muhimu sana kujiepusha na utakatifu au sense of perfactions katika mahusiano mapya au ya zamani

Mungu Ibariki Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…