Ndugu mdau,
mie nadhani it's nature kwamba taste ya mahusiano yoyote yale ni changamoto zinazoonekana na zisizoonekana baina ya wahusika. Mahusiano yasiyo na changamoto nadhani hua ni hatari zaidi katika kudumu kwa muda mrefu.
Umalaya kwangu mimi hua naona ni dhana tu isiyo na athari zozote, kwasababu wanaoitwa malaya mara nyingi ndio huingia kwenye mahusiano mazuri zaidi na kuwaacha kwenye mshangao waliowaita malaya.
Kuingia kwenye mahusiano ya mara kwa mara sio dhambi, bali ni namna ya bora zaidi ya kupata upendacho, japo tabia hiyo inaweza kuonekana mbaya mbele ya jamii au kukupotezea muda na usipate utakacho muhusika asipokua makini.
Mahusiano matamu ni yale ambayo yanajengwa kwenye msingi wa wahusika kuridhiana na kila moja kua tayari na kukubali kubeba madhaifu ya mwenzake na kustahimili mapungufu ya mwenzake, kwasababu hayupo alie mkamilifu chini ya jua.
Hapajawahi kutokea mahusiano yasiyo na changamoto dunia hii. Kua na mahusiano ya mara kwa mara ni kujaribu kutafuta au kuonja ladha tofauti za raha na changamoto za kwenye mahusiano tu, but daima hua hakuna mapya.
Ushauri wangu kwa wadau wa Jf,
Ni muhimu sana kuzichukua na kuzibadili changamoto za kwenye mahusiano na kuzifanya kua fursa muhimu ya kua makini zaidi kwenye mahusiano mapya, kujisahihisha, kujirekebisha na hatimae kuingia kwenye mahusiano madhubuti yenye furaha na amani ya kudumu licha ya changamoto tofauti zitakazojitikeza ndani yake kwasababu za kibinadamu haziepukiki.
ni muhimu sana kujiepusha utakatifu au sense of perfactions katika mahusiano mapya au ya zamani
Mungu Ibariki Tanzania