Mahusiano na wake za watu yameniponza na kunirudisha nyuma

Mahusiano na wake za watu yameniponza na kunirudisha nyuma

Dah imenigusa hii japo mm ni kijana wa miaka 24 na huu umri ndo nimeanza kulala na mwanamke japo sijaoa ila nikasalitiwa na huyu mwenza wangu...Naomba Allah aniepushe na hizi tamaa mbaya Alhamdulillahi
Amiin inshaallah, Allah atakuepusha
 
Kaka hongera sana kwa story nzuri, ila kwa kuongezea, kwenye biashara unatakiwa uchague mambo 2.
Moja, biashara yako imtegemee Mungu
Pili, biashara zako imtegemee shetani.
Asante mkuu, mm nimechagua kwa Mungu, nae sitanii wala cmjaribu Mungu, naimani atanipigania
 
Kaka hongera sana kwa story nzuri, ila kwa kuongezea, kwenye biashara unatakiwa uchague mambo 2.
Moja, biashara yako imtegemee Mungu
Pili, biashara zako imtegemee shetani.
Ukitaka namba 2, nenda kwa mganga atakupa masharti na jitahidi uyatekeleze.
Ukitaka namba 1, tekeleza masharti haya 4 ndio utafanikiwa:
1. Usizini
Biashara na uzinzi havipikiki Chungu kimoja, chagua kuwa malaya au biashara. Siku utakapozini, ndio siku utakapofirisika. Kwenye ulimwengu wa roho utakuwa umefirisika, ila kimwili inaweza kuchukua Muda hata mwaka, maana mtaji huwa unapukutika kidogokidogo.
2.Usidhulumu
Sijajua kwa nini, lakini Dhuluma na kufanikiwa kwa njia za kimungu hazifungamani. Hata uwe mtoa sadaka na zaka, maombi na kukesha kanisani, kama hiyo biashara umeanza kudhulumu, jua umekaribisha roho ya kufirisika. Ni mara mia usubiri faida ndogo ndogo halali, itakuchukua Muda lakini biashara itastawi kila siku.
3. Toa sadaka na zaka
4. Sali
Hii ya kusali haiitaji kuomba kutwa makanisani, ni kuwa na mahusiano mazuri na Mungu wako kwa maana ya kumpelekea Haja zako. Kwa hiyo hata kama usipoenda kanisani, jitahidi uwe na hata nusu saa kwa siku na Mungu wako.
Note:
Hizi ni sheria za kiroho ili utoboe kibiashara kwa kumtegemea Mungu, kama hutaki kuzifuata na unataka kutoboa kibiashara please kimbilia kwa waganga. Full stop

Ikikupendeza, nitaandika masharti ya kimwili, hayo yalikuwa ya kiroho
Andika ya kimwili pia
 
mkuu Kelebe nimesoma habari yako mwanzo mpaka mwisho nimepata funzo kubwa sana sana.....tafadhali naomba tuwasiliane PM kuna jambo tushauriane, japo kwa ID hii hii..
 
Hongera na pole kwa uliyoyapitia, sitaki kuhukumu lakini ulivyohadithia yaonyesha unayafurahia sana maisha ya kutoka na michepuko na nadhani mambo yakikaa njema haswa huko mbeleni utarudia au ikiwezekana ili usirudie oa wapili tu. Kwasasa umejifunza na unaogopa kufilisika tena inasaidia kukuerka kwenye mstari.

Yote kwa yote hongera kwa kupitia mengi, mara nyingine mtu unatakiwa upitie changamoto ujifunze ili ukae kwenye mstari maana wanasema...maisha yanaanzia miaka 40....hongera zaidi kwa mkeo kuweza kuendelea kuvumilia wengine wanakimbia pesa ikikata.
 
Kuna ambaye nimemweka blacklist maana nilishamwambia usitume SMS wala kupiga simu tofauti na SAA kumi...yy haelewi

Na lalamiko lake ni hilohilo hajawahi kukojoleshwa,mbaya zaidi anapenda hela hataree
Hayo makubaliano yanawezekana siku mbili za mwanzo, siku zinazofuata ni majanga
 
Back
Top Bottom