Kaka hongera sana kwa story nzuri, ila kwa kuongezea, kwenye biashara unatakiwa uchague mambo 2.
Moja, biashara yako imtegemee Mungu
Pili, biashara zako imtegemee shetani.
Ukitaka namba 2, nenda kwa mganga atakupa masharti na jitahidi uyatekeleze.
Ukitaka namba 1, tekeleza masharti haya 4 ndio utafanikiwa:
1. Usizini
Biashara na uzinzi havipikiki Chungu kimoja, chagua kuwa malaya au biashara. Siku utakapozini, ndio siku utakapofirisika. Kwenye ulimwengu wa roho utakuwa umefirisika, ila kimwili inaweza kuchukua Muda hata mwaka, maana mtaji huwa unapukutika kidogokidogo.
2.Usidhulumu
Sijajua kwa nini, lakini Dhuluma na kufanikiwa kwa njia za kimungu hazifungamani. Hata uwe mtoa sadaka na zaka, maombi na kukesha kanisani, kama hiyo biashara umeanza kudhulumu, jua umekaribisha roho ya kufirisika. Ni mara mia usubiri faida ndogo ndogo halali, itakuchukua Muda lakini biashara itastawi kila siku.
3. Toa sadaka na zaka
4. Sali
Hii ya kusali haiitaji kuomba kutwa makanisani, ni kuwa na mahusiano mazuri na Mungu wako kwa maana ya kumpelekea Haja zako. Kwa hiyo hata kama usipoenda kanisani, jitahidi uwe na hata nusu saa kwa siku na Mungu wako.
Note:
Hizi ni sheria za kiroho ili utoboe kibiashara kwa kumtegemea Mungu, kama hutaki kuzifuata na unataka kutoboa kibiashara please kimbilia kwa waganga. Full stop
Ikikupendeza, nitaandika masharti ya kimwili, hayo yalikuwa ya kiroho