Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Tatizo lipo hapa "Mungu ni mweza ya yote, Mungu ni mwema " ama awe na uwezo asiwe na wema, au awe na wema ila hana uwezo. Kwa kuwa hakuna jibu basi nikae na amani bila wazo la Mungu.
 
Misimamo yako haina mashiko mkuu. Kwamba Hautambui Uwepo wa Mungu ila uwepo wa sheria za nchi ambazo binadamu ndio kaziweka ndio unazitambua na kuzifwata.
Kwanza onyesha uwepo wa huyo Mungu kisha umthibitishe yupo.

Binadamu yupo na anaonekana yupo na kuthibitishika
Pathetic nenda kwa mshauri upate counselling something is wrong in your head
Sema huna majibu ya kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu unayedai yupo

Kwa vile huyo Mungu ni fiction, hajawahi kuwepo hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
 
Iv Ile hali unakua umelala usiku alaf ghafla tu ukaanza kuhisi kama Kuna kitu hakipo sawa mara kidogo unajiona huna uwezo wa kutingisha kiungo chochote Cha mwili wako alaf hata ukitoa sauti ya kuomba msaada inakua kama unajiskia peke ako tu
Unakabwa Kwa dakika kama 5 iv unahangaika tu kitandan Huwa inakuaga ni nini? Nme experience hii kitu first time npo form one boarding ,nikasimulia wenzangu asubuhi Kuna baadh ya watu na wenyewe wakasema hata Mimi pia imenitokea majuzi ,
Hio kitu Huwa ni nini ?
Nightmares.
 
Lengo la mnyama 666 limetimia

Kwanza mnyama 666 anakuingizeni katika dini yake ya uongo ambayo ni ukristo

Kisha unajiongeza mwenyewe kuongeza makufuru

Hata siku Moja hauwezi kukumkuta mtoto aliyezaliwa na kulelewa katika uislam aje kusema na kuamini kuwa hakuna Mungu

Haya yanayokukuteni ni matokeo ya kudanganywa na Wazungu na ndio lengo lao

Poleni sana wakristo Jahannam inakusubirini Kwa hamu kabisa
Huyo mnyama 666 hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Mnatunga tunga dhana zenu uchwara zisizo na uthibitisho wowote ule.

Jehanam haijawahi kuwepo, haipo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Hakuna Mungu wala Shetani.

Hakuna pepo wala jehanam.
 
Mungu kajifunua kwa namna mbili au tatu:

1. Kupitia uumbaji(by default unaona kabisa viumbe vilivyo hai na visivyo hai na wewe mwenyewe ukiwemo.) Sasa sijui we unafikilia ulimwengu ulitokae wapi.
Wewe mbona hujiulizi na huyo Mungu alitokea wapi?
2. Kupitia neno (mafunuo) (kuna maandiko kwenye biblia na baadhi ya vitabu vingine hayakuandikwa na kutunwa kwa uwezo wa mwanadamu)) .

3.ROHO MTAKATIFU (ni kama mafunuo na hii ni individually) hapa ndipo ulipokwamia mkuu.
 
Hiyo nguvu inapimwa kwa kipimo gani?

Unahakikishaje ipo kweli na hizo habari si story za kuungaunga tu?

Hiyo nguvu ina uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?
Iko in kwenye ufahamu wako na inadhihirika katika mambo unayoyaona kwa macho
 
Kuzi control kivipi?
Yani mfano unaweza ukai stopisha lakini hio huwezi mpk ikuache yenyewe ,Mimi baada ya kugunduaga jinsi hio hali inavyokuja Huwa naamka kabla haijanishika vizuri 😂 naamka nawasha taa alaf natulia zangu Yani akiwa anakuja huyo mkabaji unaanza kwanza kuona Kuna hali tofauti, ila saa zingine Sasa unakuta teali umeshakamatika huna Tena uwezo wa kuikataa Ile hali matokeo yake inabidi usubiri akukabe tuu mpk hizo dakika tano af anaondoka
 
Huwezi ukastopisha ndoto, Maana ukiwa usingizini ubongo na ufahamu wako unakuwa kwenye hali ya subconscious/ unconscious mind.

Ndio maana unakuta unaota kitu ambacho huku plan kukiota ila unashtukia tu umeota kitu ambacho hukufikiria wala kuplan kuota hivyo.

Huwezi ku control subconscious mind.

Tunaweza tu, ku control conscious mind.

Mfano mwanaume ukiwa usingizini huwezi ku control uume usisimame, unashtukia tu asubuhi uume wako umesimama wenyewe.

Ila ukiwa macho hujalala, unaweza ku control uume wako usisimame,ulale tu.
 
Ile ndoto unaweza ukai stopisha kama una uzoefu nayo , mana saa zingine unaweza ukawa umefumbua macho kabisa alaf viungo unakua huwezi kuvi control ni kama vile unakua umemuwahi mkabaji kabla hajakukaba Ile yenyewe yenyewe , kiufupi ni ndoto ambayo Mimi Huwa inanipelekea kuhisi kuwa sipo peke angu hapa
 
Ukishafungua macho tu automatically, Unakuwa kwenye conscious mind.

Ukifungua macho tu tayari ufahamu unarudi kwenye uhalisia ndio maana unaanza kufikiria ulichokuwa unakiota.

Hivyo unaweza ku control chochote.
 
Mungu kajifunua kwa namna mbili au tatu:

1. Kupitia uumbaji(by default unaona kabisa viumbe vilivyo hai na visivyo hai na wewe mwenyewe ukiwemo.) Sasa sijui we unafikilia ulimwengu ulitokae wapi.

2. Kupitia neno (mafunuo) (kuna maandiko kwenye biblia na baadhi ya vitabu vingine hayakuandikwa na kutunwa kwa uwezo wa mwanadamu)) .

3.ROHO MTAKATIFU (ni kama mafunuo na hii ni individually) hapa ndipo ulipokwamia mkuu.
1. Ukiona unachoita uumbaji, unajuaje ni matokeo ya Mungu na si kingine chochote? Unathibitishaje hilo?

2. Ukiona unachoita meno, unajuaje ni matokeo ya Mungu na si kingine chochote? Unathibitishaje hilo?

3. Ukiona unachoita roho mtakatifu, unajuaje ni matokeo ya Mungu na si kingine chochote? Unathibitishaje hilo?

Hujathibitisha , hujathibitisha hata hiyo roho kwamba ipo.
 
Watu hatuna utashi huru kama wanavyodai Agustino na Akwinasi. Hatuna hata uamuzi tuzaliwe au tusizaliwe. Hatuamui tuzaliwe na nani, wapi, lini, hatuchagui vinasaba tutakavyorithi. Haya ni mambo yanayoamua kwa kiasi kukubwa maisha yetu yatakuwaje.
Nakubali kuwa ni muhimu kupata majibu wazi ya maswali yanayojikeza kuhusu Mungu kama kitivo cha hali ya juu ya kufikiri.

Hatahivyo, ni muhimu pia tunapotafuta majibu wazi ya maswali hayo kuzingatia ukweli kuwa mtu pia ana uwezo wa kufikiri unaomuezesha kujua na kujua kuamua bila kukosea.

Ni vizuri tukaelewa kuwa uwezo wa kufikiri wa mtu ni halisi na kwamba mtu ana huru wote.

Ni kweli kuwa bado hatujui mambo mengi kwa uwazi ikiwa ni pamoja na ulimwengu unatoka wapi na unaenda wapi na hata sisi wenyewe.

Lakini kusema kuwa hatuamui tuzaliwe au tusizaliwe: tuzaliwe na nani, wapi na lini na vinasaba gani, ni mawazo yasiyozingatia akili na kushindwa kuelewa vitu vilivyopo.

Wanaozaa ni wazazi sio Mungu. Uamuzi wa kuzaa au kutokuzaa ni wa wazazi. Kwa hiyo ni mtu mwenyewe ndiye anayeamua azae au asizae.

Wazazi ndio wanaosema wanataka kuzaa. Ndio wanaoamua kuzaa mtoto na hayo mengine yote.
Utashi huru ni njozi tu. Pia, utashi huru una contradict sifa ya Mungu kujua yote. Mtu kuwa na utashi huru maana yake ana uamuzi wa mwisho kuamua atafanya nini, Mungu akishajua tu mtu atafanya nini, maana yake ni kwamba mtu hana utashi huru.

Kwa maneno mwingine, ama mtu ana utashi huru na Mungu hana ujuzi wote, ama Mungu ana ujuzi wote na watu hawana utashi huru, mawili haya ni "mutually exclusive".

Ninaiweka hoja ya Epicurus, na majibu yake, likiwamo jibu la utashi huru, na jinsi majibu yake yote yasivyokidhi kimantiki, kwa njia ya picha ili nieleweke vizuri zaidi.
Aliyevumbua maarifa ya kutengeneza magari alijua kuwa madereva watakosea na wataleta matatizo. Lakini sio kwamba madereva wasiendeshe gari kwa sababu wataleta matatizo.

Katika hoja ya akili na utashi huru kuna mambo mawili ambayo wanaopinga hoja hiyo hawayaeliwi au wanayachanganya.

Jambo la kwanza ni akili na la pili ni uhuru. Akili ndio inaanza au inatangulia utashi. Ili mtu aweze kuamua anavyotaka (utashi huru) anawajibika kujua (akili). Na uhuru maana yake ni kujua.

Mungu alimuumba mtu kuwa kama Yeye. Kuwa muumbaji. Anayetaka anakuwa kama Mungu, anaumba vitu vingine vipya kwa kutumia vitu vilivyopo. Na asiyetaka anaendelea kubaki hivyo alivyochagua.

Mungu aliwaumba watu wakiwa wema. Lakini mtu anaweza kuchagua anavyotaka. Anaweza kuchagua wema au ubaya, ukweli au uongo.

Katika fizikia tunajifunza kwamba vitu vyote vilivyopo viko katika mwendo. Na Kanisa Katoliki linafundisha kwamba ulimwengu upo safarini kuelekea utimilifu.

Huo ulimwengu mtimilifu ambao Epicurus anahoji ni kielelezo kuwa hatujaelewa vitu vyote vya asili vilivyopo vinatoka wapi na vinaenda wapi.
 
Nakubali kuwa ni muhimu kupata majibu wazi ya maswali yanayojikeza kuhusu Mungu kama kitivo cha hali ya juu ya kufikiri.

Hatahivyo, ni muhimu pia tunapotafuta majibu wazi ya maswali hayo kuzingatia ukweli kuwa mtu pia ana uwezo wa kufikiri unaomuezesha kujua na kujua kuamua bila kukosea.

Ni vizuri tukaelewa kuwa uwezo wa kufikiri wa mtu ni halisi na kwamba mtu ana huru wote.

Ni kweli kuwa bado hatuji mambo mengi kwa uwazi ikiwa ni pamoja na ulimwengu unatoka wapi na unaenda wapi na hata sisi wenyewe.

Lakini kusema kuwa hatuamui tuzaliwe au tusizaliwe: tuzaliwe na nani, wapi na lini na vinasaba gani, ni mawazo yasiyozingatia akili na kushindwa kuelewa vitu vilivyopo.

Wanaozaa ni wazazi sio Mungu. Uamuzi wa kuzaa au kutokuzaa ni wa wazazi. Kwa hiyo ni mtu mwenyewe ndiye anayeamua azae au asizae.

Wazazi ndio wanaosema wanataka kuzaa. Ndio wanaoamua kuzaa mtoto na hayo mengine yote.

Aliyevumbua maarifa ya kutengeneza magari alijua kuwa madereva watakosea na wataleta matatizo. Lakini sio kwamba madereva wasiendeshe gari kwa sababu wataleta matatizo.

Katika hoja ya akili na utashi huru kuna mambo mawili ambayo wanaopinga hoja hiyo hawayaeliwi au wanayachanganya.

Jambo la kwanza ni akili na la pili ni uhuru. Akili ndio inaanza au inatangulia utashi. Ili mtu aweze kuamua anavyotaka (utashi huru) anawajibika kujua (akili). Na uhuru maana yake ni kujua.

Mungu alimuumba mtu kuwa kama Yeye. Kuwa muumbaji. Anayetaka anakuwa kama Mungu, anaumba vitu vingine vipya kwa kutumia vitu vilivyopo. Na asiyetaka anaendelea kubaki hivyo alivyochagua.

Mungu aliwaumba watu wakiwa wema. Lakini mtu anaweza kuchagua anavyotaka. Anaweza kuchagua wema au ubaya, ukweli au uongo.

Katika fizikia tunajifunza kwamba vitu vyote vilivyopo viko katika mwendo. Na Kanisa Katoliki linafundisha kwamba ulimwengu upo safarini kuelekea utimilifu.

Huo ulimwengu mtimilifu ambao Epicurus anahoji ni kielelezo kuwa hatujaelewa vitu vyote vya asili vilivyopo vinatoka wapi na vinaenda wapi.
First things first,

Umeandika

"Hatahivyo, ni muhimu pia tunapotafuta majibu wazi ya maswali hayo kuzingatia ukweli kuwa mtu pia ana uwezo wa kufikiri unaomuezesha kujua na kujua kuamua bila kukosea."

Huu si ukweli.

Mtu hana uwezo wa kufikiri unaomuwezesha kujua na kuamua bila kukosea.

Hoja zako zinajengwa kwenye msingi wa uongo.
 
Ishi upendavyo, maana hata hayo maandiko yanasema kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe...
 
Mkuu umewahi ona mtu kafa katoa macho au mdomo wazi hadi kufikia hatua ya kumwekea super glue machoni na mdomoni ili asiharibu PICHA na mkanda WA video pia asitishe waomnbolezaji?. Huyu ni mtu aliyemkataa Mungu na wakati WA kufa by surprise akaona vitu vya ajabu ajabu vikimkaribisha sehemu mbaya hivyo anabaki anashangaa ila la kufanya hana.
 
First things first,

Umeandika

"Hatahivyo, ni muhimu pia tunapotafuta majibu wazi ya maswali hayo kuzingatia ukweli kuwa mtu pia ana uwezo wa kufikiri unaomuezesha kujua na kujua kuamua bila kukosea."

Huu si ukweli.

Mtu hana uwezo wa kufikiri unaomuwezesha kujua na kuamua bila kukosea.

Hoja zako zinajengwa kwenye msingi wa uongo.
Katika mambo ambayo nimejifunza kwenye kitabu cha Philosophy of Religion ni kwamba mafundisho ya dini na dini kwa ujumla yanaweza kuwafanya watu wengi kushindwa kutumia uwezo wao wa kufikiri na hivyo kushindwa kujua ukweli na kujua kuamua au kufanya mambo bila kukosea.

Hilo linaonekana katika vipindi mbalimbali jinsi jamii za wanadamu walivyokuwa wakiamini kuhusu Mungu na au hata sababu za kutokea kwa hali mbalimbali.

Unaweza ukasema kuwa mtu hana uwezo wa kufikiri unaomuezesha kujua na kujua kuamua au kufanya mambo bila kukosea.

Lakini ninataka kukuuliza swali.

Je! Suala la uvumbuzi wa maarifa ya kujua kutengeneza magari au mitambo, uwezo huo ni wa nani?

Na uvumbuzi huo au uwezo huo una makosa gani ukiacha makosa yanayotokana na matumizi?

Na Je! Kufikiri maana yake ni nini? Na kati ya mnyama na mtu, mwenye uwezo wa kufikiri ni nani?
 
Back
Top Bottom