Ukija huku kwa tuliopo majeshini Askari ni linatumika pale mtu amefanya mafunzo yake kwa vitendo kama ni TPDF ni ameenda mafunzo ya porini na kama ni Polisi ni amefanya pia mafunzo mafunzo ya Porini (Field Craft) na Magereza vivyo hivyo ila mwanafunzi huyohuyo kama hajafanya hayo mafunzo huyo sio Askari maana yake kama ni kwa upande wa Polisi huyo huyo ni bado anasomea u-Polisi ila akienda Porini na akimaliza atakuwa anaitwa Askari Polisi, Askari Magereza na kwa TPDF kilishakosekana kiswahili fasaha cha kulitamka Jina hilo ila mara nyingi Raia wanawaita Askari Jeshi.
Nahisi pia utauliza kwanini Uhamiaji na Zimamoto sijazijumuisha, sijazijumuisha kwa sababu wao hicho kitu hawafanyi (mafunzo ya kimedani) ila ni mazoea tu na ilishazoeleka kuitwa hivyo
Ukija kwenye Uanajeshi ni kwamba Askari wa Tpdf ni mwanajeshi, Askari wa Polisi ni Mwanajeshi, Askari wa Magereza ni Mwanajeshi pia na hata kijana wa Jeshi ka Kujenga Taifa pia ni Mwanajeshi