Maisha ya Hussein Jumbe ni ushuhuda tosha kwamba jamii zetu zina wachawi, watu wenye roho mbaya sana na makatili. Tuwe na Imani kwa Mungu

Maisha ya Hussein Jumbe ni ushuhuda tosha kwamba jamii zetu zina wachawi, watu wenye roho mbaya sana na makatili. Tuwe na Imani kwa Mungu

Cha msingi kwanza elewa uchawi upo, ila achana nao Fanya yako.

Kuna stage ukiona mambo huyaelewi jiongeze.

Ukijifanya wewe ni mtu wa dini nakuhakikishia wapo wachungaji wanakwenda kwa waganga wa kienyeji, na upande wa masheikh ndio sina hata la kusema wao ndio mafundi wenyewe.
Yes, ndicho nachofanya sasa hivi nimeachana nao kabisa. Nafanya yangu. Naelewa upo na nimeshapitia huko kote, kuwaza huo uchawi kwa vitu vingi maishani mwangu.

Ila toka nimeelekezwa vizuri na si dini. Kuna makubwa sana ya kutisha niliyopitia, mtu anakwambie eeh hapo umeshachezewa. Namimi nikaamini hivyo. Ila kwasasa havina nafasi katika akili yangu. Navipotezea kama usemavyo.
 
Uchawi ukishaamini upo, kosa la kwanza, kitu kikikutokea kosa la pili. Maisha yako yote utahangaika kwa waganga na kumaliza makanisa.

Lakini tujiulize, kuna watu wamefanikiwa sana je hao wachawi hawawaoni? Wanatuona sisi tu? Hawajaamini upande huo na wanaishi raha mstarehe.
Hii Elimu ni pana sana, ukiijua hutohangaika tena maishani na mauchawi.
It's a mind game, wake up meditate & visualize you're there, Gari nyeusi, vioo vyeusi & roho nyeusi, wake up ulipokua mtoto hujawahi kukutana na jinamizi mkaba Koo?
 
Ila toka nimeelekezwa vizuri na si dini. Kuna makubwa sana ya kutisha niliyopitia, mtu anakwambie eeh hapo umeshachezewa. Namimi nikaamini hivyo. Ila kwasasa havina nafasi katika akili yangu. Navipotezea kama usemavyo.
Ni mind game km mazingaombwe, wafanya mazingaombwe wengi km wale wanaokula misumari na viwembe ni wachawi (magician) wanacheza na mind yako, usichokijua uchawi upo msikitini upo kanisani but in a good way not bad way
 
Mzee jamii zetu uchawi Wana ona dili
Hussein Jumbe alikua anasimulia kwamba alikua anafukuzwa na KUKU KISHINGO huyo kuku akawa anamdonoa miguu, sasa yeye kwenye kutaka kumfukuza si akasema huyu kuku tu acha nimtie mashuti akaanza kumpiga kumbe masikini pale alipolala ni karibu na ukuta akaanza kubamiza mguu ukutani mpaka akavunja mfupa ndio anashtuka, kupata msaada kwenda hospital

It's a mind game, usipoelewa hautoelewa kamwe ni kwanin uwe mchawi? Kuna wachawi na kuna wanaofanya uchawi bila kujua kua wanachofanya ni uchawi mfano kuwasha udi wenye harufu kali, mafusho yenye harufu kali unayachoma ndani ya nyumba ya watu wengi kila mtu anaivuta hio harufu km mpo nyumbani kwa mganga, nk ukifanya hivyo unaroga bila kujua kua unawanga, ukimpata anaejua kucheza na mind ya dereva gari na kusababisha kifo ndio utaamini kweli upo, angalia ajali ile ya Bus la Mwendo Kasi kwa makini utaelewa jambo
 
Uchawi upo acha kubisha Kiranga Komo hayajakukuta ukapigwa mashine moja ya ukumbusho gari zima chali umebaki wewe tu alafu hauna miguu yote miwili, ndio ujue uchawi upo
Katika nchi yenye watu wajinga wengi, masikini wengi, watu wengi wasio na matumaini na wanaopenda kutumia majibu rahisi, badala ya kuumiza akili na kupata majibu rahisi, uchawi ni lazima uwepo, mawazoni mwao.
 
Ni mind game km mazingaombwe, wafanya mazingaombwe wengi km wale wanaokula misumari na viwembe ni wachawi (magician) wanacheza na mind yako, usichokijua uchawi upo msikitini upo kanisani but in a good way not bad way
Wabongo hata ukiwachezea karata tatu, wasipoelea umefanyaje, watasema uchawi.

Wengi hawajishughulishi kuchambua mambo kwa kina.
 
Katika nchi yenye watu wajinga wengi, masikini wengi, watu wengi wasio na matumaini na wanaopenda kutumia majibu rahisi, badala ya kuumiza akili na kupata majibu rahisi, uchawi ni lazima uwepo, mawazoni mwao.
Uchawi upo all over the world mkuu, na dunia nyingine unaonyeshwa waziwazi na wachawi wanashindanishwa jukwaani au hujawahi kuona ? Utofauti wa uchawi wa dunia nyingine na dunia uliyopo wewe 3rd world ni kwamba wao kwao wame-develop kuliko hao wa huko kwenu unaowaita masikini, Ila wachawi matajiri unao ni sawa kuroga Ila wao ni matajiri au sio?

Km ulizaliwa ukiwa umetoka kula damu (usishangae) tumboni kwa mama yako hakuna uji wala maziwa maana muda wote ulikua unashiba damu tupu unamfyonza mama yako wewe nyonya damu, ukakatwa kitovu basi kilichofanyika kwenye hatua za awali ni uchawi ndipo wewe ukapata kuishi mpaka leo hii unapumua

Niishie hapa,
 
Uchawi upo all over the world mkuu, na dunia nyingine unaonyeshwa waziwazi na wachawi wanashindanishwa jukwaani au hujawahi kuona ?
Nimekupa nafasi ya kuthibitisha, bado unaniuliza tu au "hujawahi kuona?".

Wapi uchawi unashindanishwa jukwaani? au unachanganya mazingaombwe na uchawi?
 
Nimekupa nafasi ya kuthibitisha, bado unaniuliza tu au "hujawahi kuona?".

Wapi uchawi unashindanishwa jukwaani? au unachanganya mazingaombwe na uchawi?
Nimeshakueleza soma tena upya updates hapo juu,
 
Hawawezi kuthibitisha, kwa sababu haupo, ni mambo ya kuhadithiana, kudanganyana, kujazana ujinga tu.
Nitakuuliza swali dogo sana najua unaamini tumeumbiwa vitu vitatu mwili, nafsi na roho je! umewahi kuigusa Nafsi au Roho yako hata siku moja ukaona inagusika vipi ? (Swali fikirishi sana)
 
Juu wapi? Post namba ngapi? Unaelewa kila post ina namba yake?
Soma hapa CHINI tena soma kwa kutulia

Back
Top Bottom